Sitasahau wakati najenga msingi, niliporudi site jioni, nikakuta wamemwaga zege kwenye nguzo na imekaa upande, nikasema mbona nguzo hii sijaielewa, fundi uchwara akaniambia ikikauka tutatindua kidogo tu inakaa squire. Nikasema hapana, nikamtafuta fundi mmoja alikuwa anajenga site nyingine jirani kabisa na kwangu, tukakubaliana tubomoe inawezekana chini hakusuka kitako na kumwaka zege la uji, kufukua tukakuta jamaa kakunja nondo akaizamisha kwenye udongo dadeki!! Nikampigia fundi akaja kuona uozo wake, nilimfyatua na mkanda begani akainama nikalala naye chini alikula kipigo cha mbwa Koko hatasahau.