Wakati wa utawala wa Magufuli, baada ya kusikia kuwa alielekeza kuwa taasis zote za kidini zinazoingiza magari zilipe kodi isipokuwa za wakatoliki wa Roma, eti kwa sababu taasisi za dini nyingine huwa ni wadanganyifu, wanayapeleka.magari waliyoingiza kwa msamaha kwenye matumizi binafsi,niliandika.kulaani jambo hilo. Mimi ni Mkatoliki wa Roma (RC).
Katika kulipinga hilo, nilieleza kuwa watawala wabaya huwa wanapenda kujishikamanisha na makundi makubwa ya jamii fulani ili watetewe na makundi hayo kwenye uovu wao. Ni blackmailing. Marehemu alifanya kila jitihada kujishikamanisha na wakatoliki kwa kuwa ni kundi kubwa la kidini, alijishikamanisha na wasukuma, japo hakuwa msukuma, kws sababu ni kabila kubwa, alijishikamanisha na kanda ya ziwa kwa sababu ni kanda yenye watu wengi, alijishikamanisha kwa kauli na maskini kwa vile maskini ni wengi ( licha ya kwamba mwanzoni aliwatimua kutika kwenye mitaa yote ya mijini, baadaye akawahadaa kwa kuwaruhusu wassmbae kila mahali ilihali hakufanya jitihafa zozote za maana za kuwaondoa kwenye umaskini).
Viongozi wa namna hiyo, wanataka wanapolalamikiwa kwa uongozi mbaya, wayageukie makundi yale na kusema, mnaona, nalaumiwa kwa sababu nawatetea ninyi wakati hakuna chochote cha pekee anachofsnya kwaajili yenu.
Tukifuatilia, kwa mtu mmoja mmoja, marehemu alisemwa zaidi na wakristo wenzake kuliko hsta wa dini tofauti, walioonja shubiri ya marehemu zaidi ni wakristo wenzake. Ben Sanane ni mkristo, Azory Gwanda ni mkristo; Mbowe, Msigwa, Mdee, na wengine wengi walikuwa Wakristo. Na ule waraka wa kulaani utawala mbaya unaopoteza watu ulitoka TEC, siyo BAKWATA.
Kwa vyovyote vile, tusikubali watawala kutufanyia mbinu ya kutugawa ili tusiwanyoshee vidole wanapofanya vibaya. Tujiulize, hivi kwa sababu Makamu mwenyekiti au mwenyekiti wa wazazi CCM ni waislamu, wana msaada gani kwa wale waislamu wa Ujiji au Same? Maisha yao yarabadilika?
Sote ni wamoja katika mazuri au madhira. Umeme ukikatika hauchagui nyumba ya muislam au mkristo. Matatizo ndiyo yatuunganishe zaidi kuliko kunyosheana vidole.
Tena katika hili, waislamu ndio wapaze sauti zaidi dhidi ya blackmailing hii ya kidini ili watawala wasijilinde kwa kutumia ngao ya udini, ukabila au eneo. Ngao yao kubwa iwe uongozi bora wenye maono, na unaozingatia usawa na haki.