Tuseme ukweli, uchaguzi wa CCM uliofanyika una viashiria vya udini

Status
Not open for further replies.
Ngoja nikuongezee, Mwenyekiti wa Ccm Dar ni Abbas Mtemvu Mwislamu pia.

Ni hivi Wakristo tuna roho mbaya sana, natamani waislamu waongezeke kwenye uongozi kwa sababu ushahidi uko wazi waislamu hawapendi dhiki na dhulma.

Utawala wa Wakristo ni chuki tupu, roho mbaya na kuuwa watu, waislamu wameprove utu kwenye utawala wao ukianzia Mwinyi, Kikwete na Samia.

Mkapa na Magufuli ni mfano wa shetani.
Hao ni wakatoriki, jaribuni wengine
 
Katika hao uliowanukuu, hakuna aliyekemewa sababu ya dini yake, bali sababu ya matendo yake. Tofauti na waaanzisha mada hizi za leo, hawa hawaangalii utendaji wa mtu bali wanataka watu wawe disqualified sababu ya dini zao. Kwamba kwa kwa kuwa waislamu wamepatapata vinafasi, wanatamani wawe wachache zaidi au eti tubalance, wakati huko zamani wakati Magufuli anawajaza Wakiristo wenzao serikalini walikaa kimya hawakumkemea Magufuli kwa teuzi zilizokuwa zomejaa taswira ya udini.

By the way, hawa watu wa sasa wamepigiwa kura na wana CCM wenyewe, hawajateuliwa na mtu!
Katika hawa waliochaguliwa ni nani aliyekemewa kwa sababu ya dini yake? Watu wanachokifanya ni kuhoji idadi yao na sio kila mtu mmoja mmoja katika nafasi yake. Watu wanahoji itakuwaje katika jiji kama Dar es Salaam nafasi za juu zote zishikwe na waislamu? Ni kama vile watu wangehoji kama nafasi zote za juu wangechaguliwa watu wa kabila moja au jinsia moja au hata wakristu watupu. Ni hoja ambayo inapaswa kubebwa na kuthibitishwa kuwa haina mashiko kwa matendo yao kama viongozi. Wasiwasi wangu ni kuwa watu kama wewe mtakingia kifua hata pale watakapoonekana kuwa wanapwaya kwa kisingizio kuwa wanakosolewa kwa sababu ni waislamu.

Hebu tumzungumzie Magufuli ambae unasema teuzi zake zilijaa taswira ya udini. Uchaguzi wa 2017 ulikuwa hivi:
1. Mwenyekiti Kheri James (Mkristu).
2. Makamu Mwenyekiti Thabia Mwita ( Muislamu Mzanzibari)
3. Mwakilishi wa UVCCM katika UWT Dotto Nyirenda ( Mkristu)
4. Mwakilishi wa UVCCM katika Jumuia ya Wazazi Amir Mkalipa (Muislamu)
5. Wawakilishi wa UVCCM katika Baraza Kuu la CCM Rose Manumba ( Mkristu), John Katarahiya ( Mkristu), Seki Boniventure Kasuga ( Mkristu)
6. Wajumbe wa UVCCM kwenda kwenye Halmashauri Kuu Sophia Kizigo ( Mkristu), Mussa Mwakitinya ( Muislamu) na Khadija Taya ( Muislamu).

Hapo pia kuna wajumbe wa UVCCM kutoka Zanzibar wawili kwenda kwenye Baraza Kuu na wawili kwenda kwenye Halmashauri Kuu, wote wanne walikuwa waislamu ( tunasahau kuwa kuna wakristu Zanzibar). Kwa hesabu zangu wakati wa JPM kulikuwa na wajumbe 6 wakristu na 3 waislamu kutoka bara. Ukijumlisha na wazanzibari idadi inakuwa waislamu wanane ( Makamu Mwenyekiti, Mwakilishi katika Jumuia ya Wazazi, wajumbe wawilikwenda kwenye Halmashauri Kuu na wanne kutoka Zanzibar) na wakristu sita.

Huo udini wa JPM hapo uko wapi?

BTW, chaguzi zetu nyingi ni uteuzi maana wajumbe ( sio wana CCM wote) wanawapigia kura watu walioteuliwa na vyombo vilivyopewa mamlaka ya kufanya hivyo.

Amandla...
 
Ngoja nikuongezee, Mwenyekiti wa Ccm Dar ni Abbas Mtemvu Mwislamu pia.

Ni hivi Wakristo tuna roho mbaya sana, natamani waislamu waongezeke kwenye uongozi kwa sababu ushahidi uko wazi waislamu hawapendi dhiki na dhulma.

Utawala wa Wakristo ni chuki tupu, roho mbaya na kuuwa watu, waislamu wameprove utu kwenye utawala wao ukianzia Mwinyi, Kikwete na Samia.

Mkapa na Magufuli ni mfano wa shetani.
Matola umejawa upumbavu mwingi sana. Mara nyingi siku hizi unaandika hoja zilizojaa uchonganishi na upuuzi mtupu. Unafaa kupuuzwa.
 
Orodha ya hapa chini ni mifano halisia

Mwenyekiti Taifa - Samia Suluhu Hassan

Makamu Mwenyekiti Bara - Abdalhaman Omari Kinana

Makamu Mwenyekiti Zanzibar - Ali Mohamed Shein anafuata Hussein Ali Mwinyi

Mwenyekiti Wazazi - Fadhili Rajabu Maganya

Makamu Mwenyekiti Wazazi - Doto Iddi Mabrouk

Mwenyekiti Vijana Taifa - Mohammed Ali Mohammed

Makamu Mwenyekiti Vijana Taifa - Rehema Sombi Omary

Orodha nyingine inakuja
Duuuh aiseee
 
Kwa jinsi uchaguzi wa CCM ulivyofanyika kwenye mikoa yote Tanzania watanzania tuache unafiki uvccm na CCM kwa ujumla Kuna udini.

Angalia viongozi waliochaguliwa kuanzia halimashauri kuu, Uvccm mpaka ngazi ya kata ni udini mtupu.

Kama huu uchaguzi umefanyika kumlridhisha Rais basi watu wamempaka matope Rais.

Tanzania sio nchi ya kidini huu uliofanyika ni uchaguzi ambao unaacha maswali mengi sana sana.
CCM ni Chama sio Dola.
Tuliani mnyolewe tulisema bila katiba mpya Kuna siku hii nchi itaendeshwa kidikteta au kikabila au kidini au kirafiki mkapuuza.

Kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
Kama waliopiga kura ni wajumbe halali wa CCM basi waliochaguliwa ni halali na wamechaguliwa kama wanachama wa CCM sio kama waumini wa dini yoyote. Tuache udini. Haya yote yanatokana na Vyombo vya Dola kushindwa kupambanua kuwa CCM ni Chama kama vyama vingine na wanaokiongoza ni watu kama watu wengine matokeo yake ni wao vyombo vya Dola kujipendekeza CCM , Mashekhe kujipendekeza CCM, mapadri ,maaskofu, manabii na Mitume kujipendekeza CCM na kumweka Mwenyekiti wa CCM kwenye kiti Cha Enzi kama mungu wao awapaye riziki yao na familia zao.

Tulieni dawa itaingia taratibu mkizinduka.
 
Kama uligombea ukapigwa za uso usilete ujinga wa kutafuta excuses za kipumbavu.

Waliopiga Kura walikuwa Waislam pekee? Mimi Mkoa niliko 3/4 ya wapiga kura Ni Wakristo na wamechagua Viongozi wa dini ya Kiislamu maana ndio waligombea na kushinda Sasa sijui unatakaje.
Pamoja na kugombea kuna kuteuliwa, mteuzi kama hakutaki jina lako halitaonekana kwa wapiga kura.
 
CCM ni Chama sio Dola.
Tuliani mnyolewe tulisema bila katiba mpya Kuna siku hii nchi itaendeshwa kidikteta au kikabila au kidini au kirafiki mkapuuza.

Kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
Kama waliopiga kura ni wajumbe halali wa CCM basi waliochaguliwa ni halali na wamechaguliwa kama wanachama wa CCM sio kama waumini wa dini yoyote. Tuache udini. Haya yote yanatokana na Vyombo vya Dola kushindwa kupambanua kuwa CCM ni Chama kama vyama vingine na wanaokiongoza ni watu kama watu wengine matokeo yake ni wao vyombo vya Dola kujipendekeza CCM , Mashekhe kujipendekeza CCM, mapadri ,maaskofu, manabii na Mitume kujipendekeza CCM na kumweka Mwenyekiti wa CCM kwenye kiti Cha Enzi kama mungu wao awapaye riziki yao na familia zao.

Tulieni dawa itaingia taratibu mkizinduka.
Wajumbe uletewa majina
 
CCM siyo jumuia, kigango, Parokia wala Jamaati. wanachama wa CCM wamechagua viongozi wanaowataka.

By the way wakati Magufuli anajaza Wakiristo serikalini mbona hizi kelele hatukuzisikia?
Nyerere aliwahi sema wewe unaweza mcharaza mke wako bakora lkn isiwe news kubwa kwa siku hiyo lkn yeye Nyerere akimcharaza mke wake bakora nchi nzima italipuka.
 
Usichokijuwa ni kwamba Magufuli ni zao la Mkapa, na Mkapa ndio alisimama Kidete kwenye vikao vya Ccm kuhakikisha Magufuli ndio anateuliwa kuwa mgombea wa Ccm.
Unazungumza usiyoyajua. Labda unasikia tu juu juu.

Ukweli ni kwamba:

Mkapa hakusimama kidete kwaajili ya Magufuli.

Wajumbe wengi wa Mkutano Mkuu walikuwa wamejiandaa kumchagua Lowasa. Wajumbe walipoona jina la Lowasa halipo wakaanza kuimba kuwa wana imani na Lowasa.

Jina la Lowasa liliondolewa kwa sababu kwa uwepo wa jina la Lowasa, Membe asingeweza kushinda. Hivyo zikafanywa figisu jina la Lowasa lisiwepo. Wakaamua libakie jina la Membe na wengine wawili ambao kwa vyovyote wajumbe hawawezi kuwachagua. Mgufuli ndiye aliyeonekana kuwa kamwe wajumbe hawawezi kumchagua.

Wajumbe waliojipanga kumchagua Lowasa walipoona jina la Lowasa halipo, wakaamua kutoka nje ya ukumbi. Waliobakia ukumbini idadi yao haikuwa inafikia hata 40%. Ndipo Kikwete akampigia simu Mkapa akimweleza hali ilivyo, na kuomba ushauri wafanye nini. Mkapa akasema kuwa kura zinazohesabika ni za watu waliopiga kura, hivyo waliobakia ukumbini waendelee na zoezi la kupiga kura. Wale watu wa Lowasa wakati huo wakiwa nje walikuwa wakijadili wafanye nini. Ndipo akaja mjumve mmoja toka ukumbini akawaambia kuwa wenzao waliobakia ukumbini wameanza kugawiwa karatasi za kupigia kura. Ndipo wakakubaliana wote kwa pamoja kuwa ili kumkomesha Kikwete, wote wakampe yule asiyetakiwa, ambaye alikuwa ni Magufuli. Kwa hiyo, kura alizopata Magufuli zilikuwa ni kura za chuki za watu wa Lowasa dhidi ya Kikwete.
 
Acha uongo Mwenyekiti Baraza la wazee ni Muislam

Mwenyekiti BAWACHA ni Sharifa Suleiman Muislam

BAVICHA uchaguzi uliopita
Makam mwenyekiti Moza Ally Muislam
Katibu mkuu Nusrat Hanje Muislam
Hapo sijataja naibu mwenyekiti na naibu Katibu kwa upande wa Zanzibar ambao nao wote ni waislam.

So Mkristo alikua Kaunya na Pambalu peke Yao kwenye nafasi almost 8 za Bavicha kitaifa!!!
Sisi tunazungumzia uongozi wa juu kitaifa, achana na hao wanaoendesha chama kwa kufuata maagizo kutoka kwa mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu nk.
 
Tanzania miaka mi5 mbeleni haitakuwa sehemu salama ya kuishi tena.
Kama haulo kwenye 'system' nashauri utafute mpango wa kuhama makazi
 
Katika hao uliowanukuu, hakuna aliyekemewa sababu ya dini yake, bali sababu ya matendo yake. Tofauti na waaanzisha mada hizi za leo, hawa hawaangalii utendaji wa mtu bali wanataka watu wawe disqualified sababu ya dini zao. Kwamba kwa kwa kuwa waislamu wamepatapata vinafasi, wanatamani wawe wachache zaidi au eti tubalance, wakati huko zamani wakati Magufuli anawajaza Wakiristo wenzao serikalini walikaa kimya hawakumkemea Magufuli kwa teuzi zilizokuwa zomejaa taswira ya udini.

By the way, hawa watu wa sasa wamepigiwa kura na wana CCM wenyewe, hawajateuliwa na mtu!
Hawa jamaa mimi nawaona wanafq tu
Malalamiko yao huyatoa kipindi cha waislam
Wakikaa wakristo wenzao hufunga midomo yao, zile nyaraka ndefu ndefu Hua hazionekani kipindi hicho
Wanajikuta watakatifu, jau sana Hawa watu
 
Kwa jinsi uchaguzi wa CCM ulivyofanyika kwenye mikoa yote Tanzania watanzania tuache unafiki uvccm na CCM kwa ujumla Kuna udini.

Angalia viongozi waliochaguliwa kuanzia halimashauri kuu, Uvccm mpaka ngazi ya kata ni udini mtupu.

Kama huu uchaguzi umefanyika kumlridhisha Rais basi watu wamempaka matope Rais.

Tanzania sio nchi ya kidini huu uliofanyika ni uchaguzi ambao unaacha maswali mengi sana sana.
Sibitisha angao kidogo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom