Tusemezane ya Ukweli: Ni nani humu JF ukiwa unajadiliana naye anakupeleka puta mpaka, unatamani asi ku "Quote" kwa kujawa na hofu

Tusemezane ya Ukweli: Ni nani humu JF ukiwa unajadiliana naye anakupeleka puta mpaka, unatamani asi ku "Quote" kwa kujawa na hofu

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
28,481
Reaction score
28,749
Huu uzi ni kwa ajili ya kusema yale ya moyoni, yaani kusema yale ya kweli kabisa.

Binadamu tumeumbwa kwa hali tofauti na vipawa tofauti hasa katika suala la kujadiliana mada za kielimu yaani kifani (Taaluma).

Humu JF tunajadiliana sana na kubishana mno, japokuwa kufanya mijadala na kupenda mijadala si jambo jema ila ikitokea dharura na haja basi hakuna budi.

Kwa ufupi kuna watu wanajua yaani wanajua hasa na kuna wale ambao ni kinyume chake, almuhimu tupo watu wa aina kadha wa kadha.

Kiukweli katika kujadiliana kwangu humu JF, kuna baadhi ya watu huwa nikijadiliana nao wananipa wakati mgumu sana, mpaka kuna muda napata hofu ya kuingia JF sababu huwa nahisi nikiingia nitakuta hoja nzito na kutakiwa kujibu hoja hiyo.

Basi kwa hofu hiyo huwa natamani nisikutane na swali au hoja kutoka mtu husika.

Mimi watu ambao huwa wananipa wakati mgumu katika mijadala na kunifanya nisome zaidi nitawataja kadiri ya uzi utakavyokuwa unaenda.
 
Baba Swalehe,

Nakupata vyema kaka. Nafanyia kazi hilo.

Kwenye kujifunza ndio msingi ulio nikuza,tatizo huwa mara nyingi nakutana na watu ambao yale wanayo yasimamia wao wenyewe hawa yajui. Hapa ndipo tatizo huwa linapo anzia,sababu tunasemezana ukweli na wewe ni miongoni mwao.
 
Kabisa.

Katika kudadisi mambo na kuyakubali,hivi kuna lililo juu ya haki na ukweli ?

Tatizo lenu ni kuwa mnamtuhumu fulani kuwa ni "Brainwashed" lakini ajabi hoja au maswali yake mnashindwa kujibu,bali nyiny wenyewe kutetea hoja zenu huwa ni shughuli.
 
Mara chache sanaa kuingia kwenye majibizano humu, hasaa yasiyokuwa na maana, nakupa facts nikiona bado unakaza kichwa basi nakupa ushindi wa mezani tu.

Nahofia sanaa watu wanaochukulia maisha ya JF kwa userious sanaa, 😒 Yani unawaza kabisa nikiingia JF nitakuta fulani kanichallenge, Seriously ?
 
Hawezi kubadilika,
Ni much know sana halafu ni brainwashed.
Mkuu unaweza ukawa unamwelekeza scientific phenomena flan.... Aisee

Atakavyokuja na sura za quran hapo utashangaa

Tupo hapa kufundishana kuelekezana

Lakini huyu jamaa ni too much

He knows everything.... No more knowledges he needs

Hata hapa nkimpa evidence ya kwamba dunia inazunguka jua

From... Heliocentric views.... Nkianza kumwelekeza mambo ya galaxy zna receeds.

Vtu vlyo proved na kina hubbs... Doppler effects na kadhalika

Jamaa atabisha maana havijui... Akija kwenye argument anakuja as if he knows more than you and you speak shit...

Anyway labda ndo Mungu alivyomuumba
 
Mkuu unaweza ukawa unamwelekeza scientific phenomena flan.... Aisee

Atakavyokuja na sura za quran hapo utashangaa

Tupo hapa kufundishana kuelekezana

Lakini huyu jamaa ni too much

He knows everything.... No more knowledges he needs

Hata hapa nkimpa evidence ya kwamba dunia inazunguka jua

From... Heliocentric views.... Nkianza kumwelekeza mambo ya galaxy zna receeds.

Vtu vlyo proved na kina hubbs... Doppler effects na kadhalika

Jamaa atabisha maana havijui... Akija kwenye argument anakuja as if he knows more than you and you speak shit...

Anyway labda ndo Mungu alivyomuumba

Unajua tukiamua kujadili habari za sayansi ya anga na kuzileta katika uhalisia nyingi huwa zina kataa.

Mfano wa suala la Dunia kuzunguka hakuna analiunga mkono jambo hili isipokuwa watu wa aina nne.

1. Wendawazimu
2. Wenye kufata mambo kwa ushabiki
3. Wasio hoji na kuuliza maswali juu ya kile wanacholetewa na Wanasayansi
4. Ambae milango yake fahamu haifanyi kazi.

Sidhani kama ushawahi kujiuliza au kuwauliza hao Wanasayansi kwanini wanasema uongo kwa kutuambia ya kuwa Dunia inazunguka. Ukweli ulivyo ni kuwa nadharia hiyo inawezekana kwenye majaratasi tu ila katika uhalisia hakuna kitu jama hicho. Hao kina Albert Einstein walikuwa madhabiki tu wa Nicolous Copernicus. Soma historia ya nadharia hiyo na utuambie kwanini Aistein na wenzake walimfanyia hujuma Albert Michelson aliposema ya kuwa Dunia haizunguki ? Bali wapo wanasayansi wengi wanaokubali ya kuwa Dunia haizunguki.


Nakuuliza swali,ni jaribio gani lililowahi kufaya likaonyesha ya kuwa Dunia inazunguka na lilifanyw kwa kuzingatia nini na marejeo yao ni wapi ?


Sasa kama nyinyi mnashindwa kuhoji na mnapenda kusikia habari na ngano za Wanasayansi ni nyinyi,ila sisi tunahoji na tuna hoji kweli.


Kwahiyo kwa mfano ulio utoa achilia mbali Qur'aan bali mpaka Wanasayansi wengine walithibisha hilo,na si mmoja au wawili bali ni zaidi ya wawili.

Kwahiyo nyinyi mnapishindwa kujibu hoja zeru msitutupie lawama za kuwa sisi tunajua sana,hili sio kweli hakuna mwanadamu anae jua kila kitu mzee,atakae sema anajua kika kitu ujue huyo hajui bali ana ishara za wenda wazimu.


Sasa mkitaka hii mijadala najua mnakimbia na kuishia kutuambia ooh nyinyi wajinga mara ooh nyinyi wabishi.
 
Kabisa.

Katika kudadisi mambo na kuyakubali,hivi kuna lililo juu ya haki na ukweli ?

Tatizo lenu ni kuwa mnamtuhumu fulani kuwa ni "Brainwashed" lakini ajabi hoja au maswali yake mnashindwa kujibu,bali nyiny wenyewe kutetea hoja zenu huwa ni shughuli.
Haki na Ukweli,
Shida ni kua hoja zako unapenda kuzipeleka kidini, na hata huu mjadala umeuanzisha mwisho wa siku utaupeleka kwenye dini... Bro, dunia ni pana kuliko ujuavyo na imebeba mengi kuliko ulivyovisoma, unapaswa kujua wewe una mitazamo ya kidini na mwingine hana na mwingine anayo ila sio ya imani yako,

Ishi kuendana na mahali palivyo usilazimishe wote wafate kile unacho wewe, wape nafasi na wengine wakupe kile wanacho, fungua milango ya kupokea vitu vipya kila siku, hapo itakufanya ukomae kiufahamu na itakufanya uishi katika mazingira yoyote.
 
Haki na Ukweli,
Shida ni kua hoja zako unapenda kuzipeleka kidini,

Sasa bibie kama majibu ya hoja husika na tena yenye ukamilifu yamapatikana kwenye dini unataka nitoe majibu gani ?

Tatizo ni kuwa unachukulia poa sana dini,wakati dini ndio inamfanya mtu kuwa makini na akili yake kufanya kazi katika ufanisi wa hali ya juu. Sidhani kama kuna jambo ambalo la kimaadili na tabia njema na namna ya kuishi na watu unaweza kulijibu na kupatia nje ya dini.

Dini imekuja kututoa katika hali duni kiutendaji kwenda katika hali ya juu ya kiutendaji.
 
Bro, dunia ni pana kuliko ujuavyo na imebeba mengi kuliko ulivyovisoma, unapaswa kujua wewe una mitazamo ya kidini na mwingine hana na mwingine anayo ila sio ya imani yako,

Kwa kuzingatia hilo ndio maana kunakuwepo na mijadala kama hii,ili kila upande uhudhurishe hoja zake kisha mwenye akili ataamua na kujua yupi mkweli na yupi muongo. Wala hakuna haja ya kutumia nguvu kunwa kubwa,ukweli wa jambo hujulikana kwa njia nyingi,njia moja wapo ni kuangalia namna ya uwasilishaji wa hoja kati ya pande mbili.
 
Back
Top Bottom