Hili la panya road lilkuwepo miaka fulani ya hapo nyuma ila likapotea miaka ya 2015 na kuendelea. Na maeneo ya wahanga wa hili zaidi ni mkoa wa Dar es salaam
Hawa ni watoto wetu wa mitaani mwetu kabisa. Walikuwa watukutu hawataki kwenda shule, hata kule shuleni hakuna mwalimu yeyote atahangaika na mwanafunzi ambaye hafiki shule kwa sababu madarasa yenyewe ni machache. Unakuta darasa la watoto 40, lina watoto 120. Wazazi pia wakawaacha kwa kuwakatia tamaa baada ya kushindikana kuwarekebisha.
Hawa wengi wao walishia darasa la 5 mpaka kidato cha 2. Ni wachache sana waliofikia form 4, wengi wa watoto wanatoka ktk familia duni sana au familia zinazolelewa na mama wa kufikia.
Huwa wanapanga muda na maeneo ya kukutania ili kupata ulevi, ni humu humu kwenye mitaa yetu. Kwa sababu ya umri wao kuwa mdogo, kifikra huwaga wakishapanga jambo lao la kufanya uharifu huwa wanaendeshwa na mihemuko ya bange au madawa mengine ya kulevya.
Katika kila mtaa familia wanakotoka panya road zinajulikana kabisa. Mara nyingine ni za wajumbe wa nyumba 10 au ndugu wa wajumbe (wazawa). Narudia tena panya road huwezi wakuta huko Masaki, Posta au Osterbay. Ni huko huko uswahilini kwenye maisha ya hovyo hovyo hivi.
Panya Road huwa hawanaga eneo maalumu la kufanyia uharifu, popote pale na muda wowote ule wao wanafanya. Nyumba yoyote ile wanaingia, maana target yao ni kupata chochote ili kukidhi mahitaji yao ya wakati huo.
Sasa nini kifanyike:

- Kwanza ule ulinzi shirikishi upewe kipaumbele maana hawa ni watoto wa Mitaani kwetu, tunawafahamu katika ulinzi shirikishi vijana wapewe motisha kwa kushiriki ktk kufanya ulinzi
- Kila mtaa utengeneze register ya vijana walio jobless, hasa wale walioacha shule, kujua wanafanya nini. Hili si gumu ni kupitia wajumbe wa nyumba kumi
- Serikali iwe na mipango shirikishi ya muda mrefu ya kunusuru haya makundi ya vijana waliokosa fursa. Kutengeneza vikundi na kupewa shughuli za kufanya kama kuzoa taka mtaani n.k
- Ikitokea panya roads wakafanya tukio, basi kipaumbele kiwekwe kuwapata viongozi wa panyaroad maana hao mara nyingi ni vijana wenye ushawishi mkubwa katika makundi haya. Wakipatikana wadhibitiwe kabisa.
- Serikali iweke mkakati wa kudumu wa kudhibiti panyaroads kabla tatizo halijawa kubwa sababu hawa panyaroad wakikomaa ndiyo wanakuwa wale majambazi wakubwa kabisa yaani wanaweza kuwa recruited kwenye makundi makubwa ya uhalifu sababu tayari wana basics za uhalifu. Pia, ni best candidates kwenye vikundi vya kigaidi
- Inatakiwa "tone from the Top" Yaani Mkuu wa nchi aoneshe kwa vitendo kutokulipenda jambo hili. Ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kali kwa Wizara husika. Maana mara nyingi Jeshi la Polisi ni "reactive" na siyo "proactive". Yaani kukiwa shwari nao wanalala usingizi. Hakuna muendelezo wa kujifunza mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu mpya kabla ya kutokea.Mara nyingi wanajifunza mbinu mara baada ya uharifu kutokea
- Jambo la mwisho ni kuhusu wakuu wa vyombo vya usalama, yaani kuanzia IGP (akae madarakani based on performance), RPC na wakuu wa vituo vidogo pamoja na wapelelezi hawa wanakaa muda mrefu kituo kimoja bila kuhamishwa.Kiasi kwamba wanakuwa wamefahamiana na waharifu wote na baadaye wanakuwa kama ndugu.