Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Police hawezi Linda KILA mtuHili la Panya road nami nitie neno.Kwa maoni yangu Kuna udhaifu mkubwa kwa jeshi la polisi.Inawezekanaje watu wajeruhi watu takribani 20 na hakuna aliyeshikwa hata mmoja??.Intelligensia ya Polisi Iko wapi? .
Ushauri Polisi waongeze Intelligensia na doria ili kuhakikisha wahusika wanatiwa mbaroni.
Wameenda wapi siku hizi hao polisi?Polisi nawaomba radhi jamani hapo kabla nilikuwa sitambui umuhimu wenu katika hii nchi ila baada ya hawa wasengerema wanaojiita "Panya Road" kutikisa hapa mtaani kwetu nimetambua kuwa ninyi ndio mnaofanya tutambe huku mjini kwa jitihada zenu za kuimarisha usalama.
Kuna vitu vinazuiliwa kwa maslahi ya umma, kuna mikasi fulani mikubwa inakata kufuli, inakata nondo hata geti la grill, sasa wakipata wahalifu huwa nishida.Sijui kama sheria inaruhusu kuziingiza but kwa njia ya panya unaweza.
Check Amazon. Kwa panya zinafanya Kazi nzuri Sana hata waje elf moja
View attachment 2208499
View attachment 2208500
Huoni aibu kusema haya? Yani unategemea wanaume wenzio ndio wakulinde?Polisi nawaomba radhi jamani hapo kabla nilikuwa sitambui umuhimu wenu katika hii nchi ila baada ya hawa wasengerema wanaojiita "Panya Road" kutikisa hapa mtaani kwetu nimetambua kuwa ninyi ndio mnaofanya tutambe huku mjini kwa jitihada zenu za kuimarisha usalama.Natangaza rasmi nawakubali kuanzia leo.!
Mnajaribu ku-solve complex problems kwa simple solutions. Nisikilize: Unawajua bodaboda? Unawajua wamachinga? Basi hawa ni hatari kuliko panya road mara kumi. Trust me! Ni suala la muda tu na matokeo yake yataonekana.Dawa ya hawa ni kuwaua kama polisi watakuwa serious
Unajiliwaza tu na wala hujui unachosema. Panya road walikuwepo hata kipindi cha Magufuli, wakati huyu mjinga Makonda akiwa kwenye kilele chake cha unyama.Makonda alivitokomeza kirahisi sana, kipanya kikikamatwa na wazazi wake pia wanaungana nae jelA bila dhamana!! Mbona walipotea wiki tu jiji shwariiii....!
Huyu mkuu wa mkoa wa sasa sijui kazi yake nini yaan?? Yaan tunaona gaps za akili za kina Makonda sometimes kuamrisha kibabe na kufuatilia utekelezaji!!
Sawa mkuuMnajaribu ku-solve complex problems kwa simple solutions. Nisikilize: Unawajua bodaboda? Unawajua wamachinga? Basi hawa ni hatari kuliko panya road mara kumi. Trust me! Ni suala la muda tu na matokeo yake yataonekana.
Hao hawaishi mbinguni wanajulikana,subiria oparesheni mtaani siku wakibanwa mbupu na kuletwa kwenye magereza ya kulima wataisha wenyewe..Hili la panya road lilkuwepo miaka fulani ya hapo nyuma ila likapotea miaka ya 2015 na kuendelea. Na maeneo ya wahanga wa hili zaidi ni mkoa wa Dar es salaam
Hawa ni watoto wetu wa mitaani mwetu kabisa. Walikuwa watukutu hawataki kwenda shule, hata kule shuleni hakuna mwalimu yeyote atahangaika na mwanafunzi ambaye hafiki shule kwa sababu madarasa yenyewe ni machache. Unakuta darasa la watoto 40, lina watoto 120. Wazazi pia wakawaacha kwa kuwakatia tamaa baada ya kushindikana kuwarekebisha.
Hawa wengi wao walishia darasa la 5 mpaka kidato cha 2. Ni wachache sana waliofikia form 4, wengi wa watoto wanatoka ktk familia duni sana au familia zinazolelewa na mama wa kufikia.
Huwa wanapanga muda na maeneo ya kukutania ili kupata ulevi, ni humu humu kwenye mitaa yetu. Kwa sababu ya umri wao kuwa mdogo, kifikra huwaga wakishapanga jambo lao la kufanya uharifu huwa wanaendeshwa na mihemuko ya bange au madawa mengine ya kulevya.
Katika kila mtaa familia wanakotoka panya road zinajulikana kabisa. Mara nyingine ni za wajumbe wa nyumba 10 au ndugu wa wajumbe (wazawa). Narudia tena panya road huwezi wakuta huko Masaki, Posta au Osterbay. Ni huko huko uswahilini kwenye maisha ya hovyo hovyo hivi.
Panya Road huwa hawanaga eneo maalumu la kufanyia uharifu, popote pale na muda wowote ule wao wanafanya. Nyumba yoyote ile wanaingia, maana target yao ni kupata chochote ili kukidhi mahitaji yao ya wakati huo.
Sasa nini kifanyike:
Mwisho; Matukio yq uharifu wa aina hii hutokea zaidi wiki ya kuelekea sikuuu
- Kwanza ule ulinzi shirikishi upewe kipaumbele maana hawa ni watoto wa Mitaani kwetu, tunawafahamu katika ulinzi shirikishi vijana wapewe motisha kwa kushiriki ktk kufanya ulinzi
- Kila mtaa utengeneze register ya vijana walio jobless, hasa wale walioacha shule, kujua wanafanya nini. Hili si gumu ni kupitia wajumbe wa nyumba kumi
- Serikali iwe na mipango shirikishi ya muda mrefu ya kunusuru haya makundi ya vijana waliokosa fursa. Kutengeneza vikundi na kupewa shughuli za kufanya kama kuzoa taka mtaani n.k
- Ikitokea panya roads wakafanya tukio, basi kipaumbele kiwekwe kuwapata viongozi wa panyaroad maana hao mara nyingi ni vijana wenye ushawishi mkubwa katika makundi haya. Wakipatikana wadhibitiwe kabisa.
- Serikali iweke mkakati wa kudumu wa kudhibiti panyaroads kabla tatizo halijawa kubwa sababu hawa panyaroad wakikomaa ndiyo wanakuwa wale majambazi wakubwa kabisa yaani wanaweza kuwa recruited kwenye makundi makubwa ya uhalifu sababu tayari wana basics za uhalifu. Pia, ni best candidates kwenye vikundi vya kigaidi
- Inatakiwa "tone from the Top" Yaani Mkuu wa nchi aoneshe kwa vitendo kutokulipenda jambo hili. Ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kali kwa Wizara husika. Maana mara nyingi Jeshi la Polisi ni "reactive" na siyo "proactive". Yaani kukiwa shwari nao wanalala usingizi. Hakuna muendelezo wa kujifunza mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu mpya kabla ya kutokea.Mara nyingi wanajifunza mbinu mara baada ya uharifu kutokea
- Jambo la mwisho ni kuhusu wakuu wa vyombo vya usalama, yaani kuanzia IGP (akae madarakani based on performance), RPC na wakuu wa vituo vidogo pamoja na wapelelezi hawa wanakaa muda mrefu kituo kimoja bila kuhamishwa.Kiasi kwamba wanakuwa wamefahamiana na waharifu wote na baadaye wanakuwa kama ndugu.
Unajiliwaza tu na wala hujui unachosema. Panya road walikuwepo hata kipindi cha Magufuli, wakati huyu mjinga Makonda akiwa kwenye kilele chake cha unyama.