Tushauriane: Hawa Panya Road tunawatokomeza kwa namna gani?

Tushauriane: Hawa Panya Road tunawatokomeza kwa namna gani?

Najiliwaza na nini sasa katika hili?? Mi sijasema hawakuwepo, kwani Makonda alipata ukuu wa mkoa kipindi cha Nyerere??

Ukweli ni kwamba, yeye ndiye alitoa order kuwa akikamatwa kipanya na mzazi wake wote wawekwe ndani!! Wakati huo Kigogo imechafuka na tuliona wazazi waliokamatwa na makundi kupungua kwa kiwango kikubwa!!

Hata kama Makonda ana mabaya yake, hili ni jambo jema sana alilofanya!! Namsifia kwa hilo maana huyu Mkuu wa mkoa wa sasa keshafeli!
Mkoa wa Dar es Salaam umejaa watu wakolofi na wenye kiburi.Makonda alijitahidi kwenda nao kihuni hivyo hivyo.Ukitumia busara pekee yake kwa Dar es salaam unafeli asubuhi kweupe mapema.namkumbuka pia Lukuvu alivyojiyahidi kuutuliza mkoa wa Dar kuheshimisha idara ya Ardhi.maana hapa Dar wapo wa aina zote.Matajiri sana na maskini sana
 
Kuna kemikali unaweka kwenye chupa ya spray ukiirusha hakuna anayeona!! Naitafuta, lakini pia kuna umuhimu wa kuwa na taser, zile zinapiga shoti kali sana kwa mbali!! Napata wapi??
Sidhani Kama inauzwa kwa watu bonafsi ila Taser Tanganyika Arms zinapatikana
 
waleteni chuga basi hata sikumoko tu mshuhudie mishikaki baridi chaapu kwaharaka mazee, tatizo wanaume wa dar mmekaa kimamse sana yaani vitoto vya 13years vinawasumbua???? so sad aisee
 
Miaka ya 80 mji wa Tabora ulikuwa na ujambazi mkubwa sana hasa maeneo ya Ng'ambo na Kiloleni. Tabora ilikuwa haifai kbs saa 12 wote mnaingia ndani. Maeneo ya Kiloleni ambapo kuna jeshi hawakuweza kuingilia kati hali hii. Majambazi ambao walikuwa wakiongozwa na JACKSON KUKU walijichanganya na kuua Wanajeshi wawili maeneo ya Rufita Hotel ambao walikuwa wanakwenda kikosi cha 25KJ kujiunga nacho. Wanajeshi walivalia njuga sakata hili na kuwaonya kbs polisi wasiingilie kati, waliwasaka wezi na majambazi nyumba kila nyumba na kufanikiwa kuwapata kama 7 ama 8 na wengine wakafanikiwa kukimbia. Hawa majambazi 7 waliuwawa mbele ya wananchi na Polisi walikabidhiwa miili yao. Tokea muda huo Kiloleni ikatulia na Tabora ikawa imepoa kbs. Hawa Panya Road ni rahisi sana kama Jeshi la polisi likiwa makini na kuacha kuwa upande wa Panya Road, chukulia mfano kwanini kusiwe na operation maalum ya kutokomeza hivi vikundi, hawa askari wanaotembea na pikipiki kukamata bodaboda mchana kwanini wasifanye patro usiku kushirikiana na polisi shirikishi maana kila mtaa kuna huu ulinzi. Unajiuliza karibu sehemu kubwa Dar es Salaam kuna vituo vidogo vya polisi vinakazi gani hivi vituo. Bila kuwaua hawa watoto hata 20 tu ili iwe mfano tutarajie mikasa na matukio makubwa mbeleni.
 
Back
Top Bottom