Tushirikishane 'Apps' nzuri za simu za Android

Wakuu kuna app naitumia inaitwa CM security ni nzuri sana kwa kweli. Pamoja na mengine mengi inafanya yafuatayo:
1. Kulock application kama whatsapp, fb, gallery, messages n.k kwa kutumia password, hivyo hamna mtu atakaeweza kufungua bila password. NB: Mtu atakaejaribu kuingiza password isiyo sahihi mara tatu atapigwa selfie ya kimya kimya bila kujua. Mwenyewe ukija utakuta picha ya huyo intruder mpaka mda, na email utatumiwa pia.

2. Kama ukipenda ina uwezo wa kufanya mtu yeyote asipokee simu itakayopigwa, kwa maana kwamba mtu akipiga ni mpaka uweke password yako ndo hiyo call inaweza kupokelewa.

3. Inafanya kazi kama antivirus yenye kuscan simu yako, pamoja na webpages utakazokua unatembelea, na hata ukidownload kitu itakwambia kama ni salama au la.
Hayo ni machache, ila inafanya mengi kwa kweli. Binafsi nimeipenda, naamini mtaipenda pia. CM security inapatikana bure playstore
 
Jaribu hili game utalipenda sana kama unapenda soka, limetulia sana hebu lipakue playstore Dream league soccer2016
Asante,nilkua na maanisha app ambayo ntapata updates za mechi analysis,stats etc...
 
Reactions: Lee
Mwenye uelewa jinsi ya ku update Gb whatsapp anisasaidie maelekezo niki update inagoma inaleta maandsh ya kiarabu then chin panakua na neno download nikibonyeza apo inagoma
tafuta latest version Google hata Mimi ilikuwa inasumbua kila siku inaleta updates za maneno ya kiarabu nikaingia Google nikatafuta latest app yake icheki hapo mkuu http://modapk.io/apkreal/gbwhatsapp_apkreal-apk/
 
Mkuu
Mkuu hiyo app inaitwaje inahofanya yote hayo samahani?
 
Kwa mfano ukiwa unangalia bongo flavor.. Hua kuna playlist YouTube inaku suggest, sasa ukitaka kuzi download zote ki urahisi unafanyaje?
Hakuna kitu kama hicho we tumia hiyo alokuelekeza mkuu hapo kupakua moja moja tu
 
Mi naona hakuna hasara yeyote kibongo bongo maana mimi kila kifaa nachonunua ku root lazima na kikiharibika napeleka smart care na hawana hiyo taaluma ya kujua kama simu iko rooted ama laah zaidi narekebishiwa na naondoka nayo sasa sijui nani kwa uzoefu wake lishawahi mkuta kukataliwa na smart care kisa simu yake iko rooted au ni story tu
 
GBwhatsap inafanya kazi gani mkuu
Ni application kama ilivyo wattsp ya kawaida ila yenyewe ina features za ziada kama kuset rangi za theme na hata kutuma file zenye ukubwa zaidi ya watp ya kawaida
Ni mambo mengi ukiitumia utaona utofauti wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…