Tushirikishane 'Apps' nzuri za simu za Android

Tushirikishane 'Apps' nzuri za simu za Android

Wakuu kuna app naitumia inaitwa CM security ni nzuri sana kwa kweli. Pamoja na mengine mengi inafanya yafuatayo:
1. Kulock application kama whatsapp, fb, gallery, messages n.k kwa kutumia password, hivyo hamna mtu atakaeweza kufungua bila password. NB: Mtu atakaejaribu kuingiza password isiyo sahihi mara tatu atapigwa selfie ya kimya kimya bila kujua. Mwenyewe ukija utakuta picha ya huyo intruder mpaka mda, na email utatumiwa pia.

2. Kama ukipenda ina uwezo wa kufanya mtu yeyote asipokee simu itakayopigwa, kwa maana kwamba mtu akipiga ni mpaka uweke password yako ndo hiyo call inaweza kupokelewa.

3. Inafanya kazi kama antivirus yenye kuscan simu yako, pamoja na webpages utakazokua unatembelea, na hata ukidownload kitu itakwambia kama ni salama au la.
Hayo ni machache, ila inafanya mengi kwa kweli. Binafsi nimeipenda, naamini mtaipenda pia. CM security inapatikana bure playstore
 
Jaribu hili game utalipenda sana kama unapenda soka, limetulia sana hebu lipakue playstore Dream league soccer2016
Asante,nilkua na maanisha app ambayo ntapata updates za mechi analysis,stats etc...
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Mwenye uelewa jinsi ya ku update Gb whatsapp anisasaidie maelekezo niki update inagoma inaleta maandsh ya kiarabu then chin panakua na neno download nikibonyeza apo inagoma
tafuta latest version Google hata Mimi ilikuwa inasumbua kila siku inaleta updates za maneno ya kiarabu nikaingia Google nikatafuta latest app yake icheki hapo mkuu http://modapk.io/apkreal/gbwhatsapp_apkreal-apk/
 
Mkuu
Wakuu hiyo app ni zaidi hapo unavyo iona, zipo picha nimezi edit kwahiyo app ila kuziweka hapa siwezi.
2.Kuhusu kukuelekeza ningependa na wewe uwe mbunifu pia, sina hakika kama naeleweka. wapo nilio waelewesha baadhi ya njia za kutumia hiyo app, njia nyingine ni wewe mwenyewe kulingana na wazo ulilonalo kichwani kuhusu picha ikae ikae vipi.
Na lamsingi kabisa ni kujua kila kipengele mule kwenye hiyo app kina maana gani.

Hizi ni faida za hiyo App
-Kubadili rangi zapicha yako
-kubadili background ya picha yako
-Kuweka au kutengeneza maandishi kwenye picha
-Kubadili sura au sehem yoyote ya mwili wako na kuweka vya mtu mwingine
-Kutengeneza logo/badge mbali mbali
-ku invert, crop, nk
-kubadili picha au maandishi uliyoyaweka ktk mfumo wa picha kuwa pdf.
-unaweza itumia kama video play na uka cupture picha kutoka kwenye hiyo video unayotazama
-Ku unganisha picha yako na mtu mwingine mkaonekana mlipiga pamoja.
- Kutengeneza animation GIF
- Ku compress to zip picha zako

Matumizi ni mengi sana kulingana na wewe unataka picha yako iweje.
Mkuu hiyo app inaitwaje inahofanya yote hayo samahani?
 
Kwa mfano ukiwa unangalia bongo flavor.. Hua kuna playlist YouTube inaku suggest, sasa ukitaka kuzi download zote ki urahisi unafanyaje?
Hakuna kitu kama hicho we tumia hiyo alokuelekeza mkuu hapo kupakua moja moja tu
 
Wakuu msaada tafadhali. Katika kupitia faida za ku root device nimegundua ni nyingi mno kuliko hasara. Risk kubwa nliyoiona ni kua device inakua vulnerable to malicious attacks kama hamna antivirus nzuri. Ila naamini wale ambao tayari mtakua mmeroot mna fahamu vizuri hilo. Je, ni install antivirus gani (ya free) ambayo itakua msaada sana kwangu device yangu itakapokua rooted. Device nnayotaka kuiroot ni tablet, galaxy note 10.1 (2014 edition)
Mi naona hakuna hasara yeyote kibongo bongo maana mimi kila kifaa nachonunua ku root lazima na kikiharibika napeleka smart care na hawana hiyo taaluma ya kujua kama simu iko rooted ama laah zaidi narekebishiwa na naondoka nayo sasa sijui nani kwa uzoefu wake lishawahi mkuta kukataliwa na smart care kisa simu yake iko rooted au ni story tu
 
Wakuu tuambizane katika experience ya apps zipi ambazo unaona bila hizo huwezi kuona thamani ya simu yako...

Mi naanza na mobdro app noma sana
Link ya kudownload MOBDRO
Charlie mobdro.apk
============
kwangu inakataa inaniandikia hivi:-
95bdb443ed92a4c2f2ccb093ba5571f5.jpg
 
GBwhatsap inafanya kazi gani mkuu
Ni application kama ilivyo wattsp ya kawaida ila yenyewe ina features za ziada kama kuset rangi za theme na hata kutuma file zenye ukubwa zaidi ya watp ya kawaida
Ni mambo mengi ukiitumia utaona utofauti wake
 
Back
Top Bottom