Mkuu punguza jazba. Si wote tunaoandikia humu tunafanana. Mimi nauliza maswali genuine kabisa. Naomba usinifananishe na mtu yeyote mwingine. Kama hukubaliani na hoja nilizotoa na zimekukera ama sema tu kwamba "si kweli" kisha toa data/hoja au ignore the whole stuff.
Maswali yangu yamelenga kwenye hoja ambazo zimekuwa zikitolewa mara kadhaa kuhalalisha uwepo wa Mbowe kwenye uenyekiti wa CHADEMA muda mrefu. Sote tunajua CHADEMA ndicho chama kinachowapa fursa Watanzania wengi wenye nia ya ya dhati ya kuikosoa serikali kwenye "madhambi" yake na kupendekeza namna mbadala ya kuhakikisha utawala bora nchini. Watanzania wa kawaida, wasomi, wafanya biashara, watumishi wa umma, viongozi wa serikali na hata wa CCM, huitegemea CHADEMA katika kuwasilisha hoja makini dhidi ya serikali na chama tawala. Hata bungeni, uwepo wake unachangamsha mijadala ipasavyo. It's a credible opposition platform or force for change. Hivi sasa gap inaonekana wazi. Akina Halima pamoja na kujitahidi kuongea point bahati mbaya hawaheshimiwi na pande zote.
Lakini CHADEMA inakabiliwa na changamoto kubwa nyingi. Imebanwa sana na serikali na kuwekwa katika mazingira hatarishi hata ya assassination ya viongozi wake. Kwa upande wake nayo wanachama na viongozi wake hawana uelewa mmoja wa mambo ya msingi na si wote wanaaminika nyakati zote. Mapambano dhidi ya usaliti ni suala genuine na la kudumu. Ama sivyo CHADEMA ingekuwa imekufa zamani sana kama baadhi ya vyama vilivyobakia vivuli tu leo hii. Sisi kama Watanzania tunapenda kuona upinzani imara unajengeka nchini.
Huwa napenda sana mawazo yako katika hoja mbalimbali lakini sio kama haya uliyotoa hapa. Ingetosha kusema Mbowe hana sifa na hafai kuwa kiongozi wa CHADEMA, ukaweka data kisha ukapendekeza mtazamo mbadala. Unaweza hata kui-dismiss CHADEMA yote kuwa si credible opposition kama mimi ninavyoiona. Inatosha. Mambo ya "sisi" kurogwa na kuwa wajinga hayahitajiki hapa.