Elections 2015 Tusidanganyane !! Hapa tunachagua mtu wa kuibadilisha system

Elections 2015 Tusidanganyane !! Hapa tunachagua mtu wa kuibadilisha system

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,425
Reaction score
4,768
Wasalaam wanaJF !

Tukiamua kuhukumu tunatakiwa kukusanya ushahidi na kuhukumu kwa haki.

Mada hii inawaendea wote kwa maana ya Chadema asilia,wanaccm,Team lowassa na wananchi kwa ujumla.

Natangulia kusema kuwa tunachagua mtu wa kuibadilisha system iliyooza ndani na nje ya serikali!!

Tunachagua mtu muhimu wa kwenda kubeba zege la kuijenga upya Tanzania.

Tunachagua mtu jeuri kiasi cha wanaomzunguka wajue hivyo.


Nachelea kusema kuwa makosa ya Boyz 2 men kamwe hayawezi kutumiwa kumuhukumu mwana mchapakazi na askari kamili wa mwamvuli ndugu John Pombe Magufuli.

Magufuli anaibuka kivyake vyake kama mzuka ama kwa uweza wa mola ama kwa weledi wa kitengo!

Kura za watanzania zitajikita kwa kuangalia Magufuli,lowassa,Anna na wengine ni kina nani hasa katika siasa na maendeleo au ustawi wa Taifa.

Wapo wengi wanaoulaumu mfumo bila tafakari ya kina kuwa tatizo sio mfumo bali wanaopewa dhamana ya kuusimamia mfumo.

Mfumo upo tu na hata wanaolilia mabadiliko ni sehemu ya mfumo huo huo unaoitwa mchafu


utamsikia Mkurugenzi au mkuu wa taasisi akiulaumu mfumo ilihali kwenye halmashauri yake kuna uchafu unatendeka!

TATIZO NI MTANDAO

Hili ni tatizo la muda mrefu ndani ya ccm hata kabla mwalimu Nyerere hajatutoka na aligundua hili na kulikemea na kujaribu kulifuta bila mafanikio na pengine ni chanzo cha yeye kututoka!

Mtandao huu ulimea na kuota mizizi ndani ya ccm na ndani ya serikali kiasi cha kufikia dharau kubwa dhidi ya wengi na wenye mamlaka ya nchi hii.

Mzee butiku alitugusia kiasi juu ya huu mtandao na muenendo wake kwa miongo kadhaa ya ccm.

MAKOSA YA BOYZ TWO MEN

Hili ni kundi la vijana wawili walioshibana ingawa mmoja inawezekana alikuwa mjanja na kumtumia mwingine.

Ni kundi lililotuletea mtandao wa kihuni ndani ya chama na hatimaye ndani ya nchi.

Ni kundi lililokuja na style ya propaganda kupitia media hasa hasa magazeti na hatimaye likashinda na kupewa 'kiwembe' wacheze nacho ...kilichotokea sitaki kukisema.

leo hii tunapolilia mabadiliko tunalia kutokana na ukosefu mkubwa wa weledi na uwezo wa kikundi hiki cha boyz 2 men.

Tunalilia mabadiliko kutokana na kushindwa kwa mabwana hawa wawili iwe kabla ya kuhaidiana na kugeukana au kabla ya kutuzingua.

They failed us as they failed themselves!!

Ni kundi hili hili linalotuweka kwenye state ya kutojitambua sasa na kutuondoa kwenye ajenda zetu za msingi.

Ni kundi hili hili linalotufanya tujichanganye na kutojielewa ni nini hasa tunachohitaji kama taifa!

MAKOSA YA WAWILI HAWA HAYAWEZI KUTUPOFUSHA KUCHAGUA KILICHO SAHIHI

Ni maono yangu kuwa nyuma ya wananchi kuna kundi la wazalendo na wazoefu ambao walikubali kukaa chini na kutafakari na kukubali kukataa kuliona Taifa likizamishwa na wanamtandao.wazee wakaamua kuignore propaganda za media na ushawishi wa kifedha.

wazee wakaamua iwe mbaya au nzuri lakini mwisho wa vurugu za boyz two men umeshafika.

Wazee wakaamua kutuletea JOHN P MAGUFULI just from nowhere but amongst us!!

Hukumu ya Magufuli haiwezi kuchanganywa na ushahidi wa vurugu ya boyz two men.

Hukumu ya Magufuli itatokana na ushahidi wa utendaji wake na haiba yake au makosa yake yeye kama yeye.

Ni uhuni kutaka kumchanganya Magufuli na uozo uliofanywa na boyz two men.

Kwa ufupi ni kwamba tumhukumu Magufuli kama Magufuli na sio kiujumlajumla.

Hapo tutakuwa tumetenda haki.

CIAO!!
 
Hakuna anayeweza kusukuma gari akiwa ndani yake.

Yuko anayeweza kuamrisha gari lisukumwe wakati yeye akiwa ndani...ndio utamaduni wa dereva!!tunamuhitaji dereva wa kuamrisha watu walisukume gari wakati yeye akinyoosha usukani.
 
ccm hata kama itamteua malaika Gabriel bado itaendelea kuwa ccm ile ile iliyochoka hatuwezi kurudi nyuma. lazima watoke tu msilete porojo or huyu yesu or huyu bikra maria or huyu ibrahim that is nosense. ccm must go
heri kuwa na malaika usiyemjua kuliko kuishi na shetani unayemfahamu
waondoke tumjenge upya mama yetu Tanzania.
Magufuli atatusamehe kwa hili. akiweza atoroke aje.
 
Ukikua utarudi kuja kuchangia kwa hoja.
Hata Boyz two men huwajui!!

We umekuwa???
Boyz to men??? Nimewajua kabla yako we c juz ndio umetoka kwa baba na mama yan unatuletea ctory za zaman hapa wawe boyz to men,men to boyz watajua wao....

Tutamchagua lowassa aingie ikulu
 
We umekuwa???
Boyz to men??? Nimewajua kabla yako we c juz ndio umetoka kwa baba na mama yan unatuletea ctory za zaman hapa wawe boyz to men,men to boyz watajua wao....

Tutamchagua lowassa aingie ikulu

Majibu ya viroba hayatuondoi kwenye hoja ya msingi!
 
ccm hata kama itamteua malaika Gabriel bado itaendelea kuwa ccm ile ile iliyochoka hatuwezi kurudi nyuma. lazima watoke tu msilete porojo or huyu yesu or huyu bikra maria or huyu ibrahim that is nosense. ccm must go
heri kuwa na malaika usiyemjua kuliko kuishi na shetani unayemfahamu
waondoke tumjenge upya mama yetu Tanzania.
Magufuli atatusamehe kwa hili. akiweza atoroke aje.

Ha ha ha ha ha mkuu umetsha
Et vijana wa IT wa Masaki wanakuja na story za boyz to men mi nimewaambia hta magufuli awe girls to boy atajua yeye
 
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, MamaSamia Suluhu Hassan akimsalimia Katibu wa CCM mkoa wa MorgoroRojas Rumuli wakati wa mapokezi yake, alipowasili mkoani Morogoro kufanya mikutano ya kameni katika mkoa huo leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsalimia mgombea Ubunge Jimbo la Gairo, Sadik Murad wakati alipowasili mkoani Morogoro, kufanya mikutano ya kampeni mkoani humo.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwapungua mkono wananchi waliofika kumlaki alipowasili mkoani Morogoro leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Inocen Karogeresi
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Gairo A, kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro.
Baadhi ya wananchi wakiwa na mabango kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika jimbo la Gairo leo.
Katibu wa CCM, mkoa wa Morogoro, Rojas Romuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi Gairo A katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro
Mgombea Ubunge jimbo la Gairo Sadik Murad akihutubia wananchi atika mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika leo katika jimbo hio mkoani Morogoro
Umati wa wananchi ukiwa umefurika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Gairo A, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Gairo mkoani Morogpro
Mwananchi akionyesha bango la kumfagilia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro








 
Yuko anayeweza kuamrisha gari lisukumwe wakati yeye akiwa ndani...ndio utamaduni wa dereva!!tunamuhitaji dereva wa kuamrisha watu walisukume gari wakati yeye akinyoosha usukani.

Ok. Sasa hapo unadhani mwenye nguvu ya kufanya hilo gari bovu lisogeee ni wanaosukuma nje au magufuli aliyeko ndani kwenye usukani..tafakari chukua hatua
 
ccm saa mwaka huu sio kutoa ahadi ni kutuonyesha walichofanya nachelea kusema wewe mleta mada una maslahi na ccm ndio maana unalazimisha tumkubali mtu wenu tunataka mabadiliko nje ya ccm kwa sababu tz ni ya vyama vingi huo unazi wako wa chama kimoja hautusaidii tunahitaji changamoto na mawazo kutoka nje ccm
 
Ok. Sasa hapo unadhani mwenye nguvu ya kufanya hilo gari bovu lisogeee ni wanaosukuma nje au magufuli aliyeko ndani kwenye usukani..tafakari chukua hatua

Tafakari sana mkuu...tulipokuwa na watanzania wengi wasiokuwa na elimu hatukuamua kufukuza walimu wote au kuwahamisha wajinga tulichukua jukumu la kuelimisha !
 
ccm saa mwaka huu sio kutoa ahadi ni kutuonyesha walichofanya nachelea kusema wewe mleta mada una maslahi na ccm ndio maana unalazimisha tumkubali mtu wenu tunataka mabadiliko nje ya ccm kwa sababu tz ni ya vyama vingi huo unazi wako wa chama kimoja hautusaidii tunahitaji changamoto na mawazo kutoka nje ccm

Ni kwa mda gani basi tutakuwa tunataka mabadiliko nje ya chama tawala?
Hata nchi za kifalme zimebadilika kupitia ukoo ule ule wa kifalme...njoo na hoja ya kueleweka na sio kutaka cosmesis katika utawala.
 
Kachukue buku saba yko kwa kupost ulichoelekezwa tunashukuru msg send.
 
Mpuuuuuuuzi tukuchague wewe basi urafiki wa watu unalihusu nini taifa tunaangalia kichwan km kuko salaaama broo vp ubongo naona umembonji
 
Yuko anayeweza kuamrisha gari lisukumwe wakati yeye akiwa ndani...ndio utamaduni wa dereva!!tunamuhitaji dereva wa kuamrisha watu walisukume gari wakati yeye akinyoosha usukani.

Kwa taarifa yako ule upuuzi uliokuwa ukifanywa na wabunge wa ccm kwa kutumia wingi wao hatuko tayari kuuona. Na kwa bahati mbaya sana dalili zinaendelea hata kwenye kampeni hizi. Mbele ya Magufuli tumesikia maneno ya kipuuzi kabisa toka timu yake ya kampeni huku Magufuli akiwa kimya kabisa. Unakumbuka neni mgombea kujinyea? Upuuzi huo wa jukwaani na huku Magufuli akichekelea umeamsha makovu yetu ya jinsi wabunge wa ccm walivyokuwa kero na wasiojua wajibu wao.

Sasa ww leo unatuambia tumchague mtu anayeataka kuingia madarakani kwa kutumia kampeni za matusi, kisha wakienda bungeni waishie kuzomea na kutoa mipasho. Tutawapiga chini wote kwani tunajua tunaletewa uozo uleule kwa maneno matamu. Pole sana
 
Back
Top Bottom