Elections 2015 Tusidanganyane !! Hapa tunachagua mtu wa kuibadilisha system

Elections 2015 Tusidanganyane !! Hapa tunachagua mtu wa kuibadilisha system

meningitis

Nimependa sana maoni yako ,nadhani hayakutawaliwa na jazba ya kisiasa,nadhani hoja zako zinaweza zikawa zimesukumwa na uzalendo.Taiafa letu limefika hapalilipo si kwa bahati mbaya,bali tatizo kubwa ni Uongozi.Naukisema uongozi CCMhaiwezi kwepa lawama.Tunaposema C.C.M.haijafanya kitu tunajaribu kujiananisha na wenzetu ambao mazingira yao yanafanana sana nasisi,lakini wenzetu wanapiga hatua.Mfano watu kama Ethiopia Walipata janga kubwa sana la njaa 1985 lakini sasa wanakwenda speed kubwa kimaendeleo sisi pamoja na wimbo wetu mzuri wa AMANI NA UTULIVU tunazidi kuwa masikini kila siku.Hatusemi ndani ya CCM hakuna watu wazuri wapo lakini ndani ya mfumo waCCM hawawezi fanya vizuri.

Mfano watu walikuwa na imani sana na pinda wakati anateuliwa kuwa waziri mkuu wakasema mtoto wa mkulima, hana makandokando na anachukia sana ufisadi.Katika misa yake ya shukrani kwa kuchaguliwa kuwa PM pale stPETER'S aliapa atafanya kila liwezekanalo kuondoa ufisadi.Siku 100 baada ya kukaa ofisini alipo ulizwa amefikia wapi na vita vyake vya ufisadi alisema hii vita ni ngumu sana na ukiingia kwa pupa nchi ita waka moto.Sina Tatizo na Magufuli lakini ndani ya CCM Hakuna kitu .tuungane wote watanzania Wenye nia njema Tuungane tuondoe CCM .Baada ya hapo tujenge mfumo bora .then tupate maendele😵BAMA aliwaambia wakenya Hamuwezi kupata Maendeleo ya Dhati kama hamtakua na Demokrasia ya kweli then utawala bora then Maendeleo.TUUNGANE PAMOJA TUIKOMBOE NCHI YETU.
hatari ni kwamba ule uchafu wote uliopukutika ccm umeenda kujikusanya huko upinzani na unataka kurejea kwa gia hiyo...
..
 
Usije ukabadili ID tu.

Maana nnauhakika baada ya tarehe 25 ID nyingi humu zitayeyuka kama zilivyoyeyuka zile zilizokuwa zinamshambulia Lowassa alipokuwa CCM.
server ya Jf inazidi kujaa tu
 
Kwenye post uliyoninukuu hapo mwanzo, mimi sikuuliza. Nilitoa msimamo wangu. Wewe ndio umenialika. Sasa sijui unataka nini?
bado unaamini hawezi kuubadilisha mfumo??umeona vilio na kusaga meno kutoka kwa wale wale wa karibu??
 
bado unaamini hawezi kuubadilisha mfumo??umeona vilio na kusaga meno kutoka kwa wale wale wa karibu??

Hawezi kubadilisha mfumo hata siku moja. Vilio vya watu haina maana kuwa anabadilisha mfumo. Hata kichaa anaweza kuchukua rungu na kuwatandika watu na vilio vikasikika kila kona. Huko sio kubadilisha mfumo. Ni ugonjwa wa akili.

Na wewe akili zako kama za Koromije. Pumbavu sana. Nilifikiri najadiliana na mtu anayejitambua.
 
ni upi sasa muktadha wako wa "kubadili mfumo" hebu toa sifa za mfumo uliobadilika...matusi hayaui na hayasaidii...njoo na hoja tu.

Mimi nna akili kama "Nahum"
 
ni upi sasa muktadha wako wa "kubadili mfumo" hebu toa sifa za mfumo uliobadilika...matusi hayaui na hayasaidii...njoo na hoja tu.

Mimi nna akili kama "Nahum"
Mimi ningemwona angalau wa maana kidogo kama asingekubali kuwa Mwenyekiti wa chama. Ila alipokubali tu, nikazidi kumtoa maana.

Rais ndiye mtu mwenye mamlaka makubwa kwa mujibu wa katiba yetu. Mwenyekiti wa CCM asingekuwa Rais, anakuwa sawa na Wenyeviti wa vyama vingine. Ule urais ndiyo unampa nguvu Mwenyekiti wa CCM.

Na kama alivyojaribu kujipambanua wakati wa kampeni, tatizo la nchi hii ni CCM. Sasa mtu mwenye nia ya kubadili taifa hili anajifunga kwa chama kilichosababisha haya yote.

Angekuwa nje ya chama, angeweza kufanya mabadiliko kweli. Sasa ona hata mahakama ya ufisadi imedoda; naamini kwa kuwa makada wengi wa sasa na zamani ndiyo wangekuwa wateja. Na kuwashtaki hao kunamaanisha kwenda na wengi.
 
hapa nashindwa kukuelewa ina maana yeye kuwa mwenyekiti wa chama ndio anashindwa kuwawajibisha au ndio imekuwa kazi rahisi kuwawajibisha...
kumbuka mkakati wa kutenganisha hizi kofia mbili ulikuwa ni mkakati wa mafisadi
.
 
Anashindwa kuwawajibisha! Mafisadi ndiyo makada wenyewe, of course wakiongozwa na Magufuli mwenyewe, fisadi mwingine kutoka CCM. Kwa lugha nyingine ndani ya CCM nani ana uwezo wa 'kumfunga paka kengele?'
 
Wasalaam wanaJF !

Tukiamua kuhukumu tunatakiwa kukusanya ushahidi na kuhukumu kwa haki.

Mada hii inawaendea wote kwa maana ya Chadema asilia,wanaccm,Team lowassa na wananchi kwa ujumla.

Natangulia kusema kuwa tunachagua mtu wa kuibadilisha system iliyooza ndani na nje ya serikali!!

Tunachagua mtu muhimu wa kwenda kubeba zege la kuijenga upya Tanzania.

Tunachagua mtu jeuri kiasi cha wanaomzunguka wajue hivyo.

Nachelea kusema kuwa makosa ya Boyz 2 men kamwe hayawezi kutumiwa kumuhukumu mwana mchapakazi na askari kamili wa mwamvuli ndugu John Pombe Magufuli.

Magufuli anaibuka kivyake vyake kama mzuka ama kwa uweza wa mola ama kwa weledi wa kitengo!

Kura za watanzania zitajikita kwa kuangalia Magufuli,lowassa,Anna na wengine ni kina nani hasa katika siasa na maendeleo au ustawi wa Taifa.

Wapo wengi wanaoulaumu mfumo bila tafakari ya kina kuwa tatizo sio mfumo bali wanaopewa dhamana ya kuusimamia mfumo.

Mfumo upo tu na hata wanaolilia mabadiliko ni sehemu ya mfumo huo huo unaoitwa mchafu

utamsikia Mkurugenzi au mkuu wa taasisi akiulaumu mfumo ilihali kwenye halmashauri yake kuna uchafu unatendeka!

TATIZO NI MTANDAO

Hili ni tatizo la muda mrefu ndani ya ccm hata kabla mwalimu Nyerere hajatutoka na aligundua hili na kulikemea na kujaribu kulifuta bila mafanikio na pengine ni chanzo cha yeye kututoka!

Mtandao huu ulimea na kuota mizizi ndani ya ccm na ndani ya serikali kiasi cha kufikia dharau kubwa dhidi ya wengi na wenye mamlaka ya nchi hii.

Mzee butiku alitugusia kiasi juu ya huu mtandao na muenendo wake kwa miongo kadhaa ya ccm.

MAKOSA YA BOYZ TWO MEN

Hili ni kundi la vijana wawili walioshibana ingawa mmoja inawezekana alikuwa mjanja na kumtumia mwingine.

Ni kundi lililotuletea mtandao wa kihuni ndani ya chama na hatimaye ndani ya nchi.

Ni kundi lililokuja na style ya propaganda kupitia media hasa hasa magazeti na hatimaye likashinda na kupewa 'kiwembe' wacheze nacho ...kilichotokea sitaki kukisema.

leo hii tunapolilia mabadiliko tunalia kutokana na ukosefu mkubwa wa weledi na uwezo wa kikundi hiki cha boyz 2 men.

Tunalilia mabadiliko kutokana na kushindwa kwa mabwana hawa wawili iwe kabla ya kuhaidiana na kugeukana au kabla ya kutuzingua.

They failed us as they failed themselves!!

Ni kundi hili hili linalotuweka kwenye state ya kutojitambua sasa na kutuondoa kwenye ajenda zetu za msingi.

Ni kundi hili hili linalotufanya tujichanganye na kutojielewa ni nini hasa tunachohitaji kama taifa!

MAKOSA YA WAWILI HAWA HAYAWEZI KUTUPOFUSHA KUCHAGUA KILICHO SAHIHI

Ni maono yangu kuwa nyuma ya wananchi kuna kundi la wazalendo na wazoefu ambao walikubali kukaa chini na kutafakari na kukubali kukataa kuliona Taifa likizamishwa na wanamtandao.wazee wakaamua kuignore propaganda za media na ushawishi wa kifedha.

wazee wakaamua iwe mbaya au nzuri lakini mwisho wa vurugu za boyz two men umeshafika.

Wazee wakaamua kutuletea JOHN P MAGUFULI just from nowhere but amongst us!!

Hukumu ya Magufuli haiwezi kuchanganywa na ushahidi wa vurugu ya boyz two men.

Hukumu ya Magufuli itatokana na ushahidi wa utendaji wake na haiba yake au makosa yake yeye kama yeye.

Ni uhuni kutaka kumchanganya Magufuli na uozo uliofanywa na boyz two men.

Kwa ufupi ni kwamba tumhukumu Magufuli kama Magufuli na sio kiujumlajumla.

Hapo tutakuwa tumetenda haki.

CIAO!!
This all started with Bashite.....Just fire him how hard can it be? We love our President na tunamtakia kila la kheri....lakini BASHITE MUST GO!
 
This all started with Bashite.....Just fire him how hard can it be? We love our President na tunamtakia kila la kheri....lakini BASHITE MUST GO!
umesoma hii thread ilianzishwa lini?nadhani bado ulikuwa shuleni ambapo mlikuwa mnakatazwa kumiliki simu.by then tulishamjadili bashite,mange,gwajima na nahum moses
 
umesoma hii thread ilianzishwa lini?nadhani bado ulikuwa shuleni ambapo mlikuwa mnakatazwa kumiliki simu.by then tulishamjadili bashite,mange,gwajima na nahum moses
Uwiiii my bad but still.......point iko palepale!
 
Songa mbele askari wa mwamvuli mpaka system ibadilike
 
Back
Top Bottom