Kiutani GENTAMYCINE nawacheka mno Yanga SC na nimefurahi sana kwa Kufungwa Kwako ki 'Beauty Beauty' Goli ( Bao ) Mbili za Vipers FC ila tukiondoa Utani Wetu wa Simba na Yanga kwa ninavyowajua Waganda, walivyowekeza katika Soka na kuwa very Serious hata Simba SC yangu ingecheza nao Leo nayo ( nasi ) tungefungwa vile vile na huenda hata kwa Magoli zaidi ya Waliyofungwa Yanga SC ( Watani zetu )
Kwanini Yanga SC leo imefungwa na Timu za Tanzania kuanzia ya Taifa ( Taifa Stars ) na hata Simba SC yangu huwa zinafungwa mno na Uganda ( Klabu za Uganda ) ni kwamba Sisi Tanzania Soka letu tumeliwekeza zaidi katika Siasa, Majungu, Utapeli ( Uwongo ) na Propaganda wakati Uganda ( Waganda ) Wao Soka lao wameliwekeza zaidi katika Ufundi, Utaalam, Mikakati na Maandalizi ya Kimsingi ya Kukuza Vipaji vya Wachezaji wao tokea Ngazi za Shule za Msingi, Upili na hata Vyuo Vikuu.