Tusidanganyane; njia ya foleni kuelekea kwenye mafanikio na utajiri haina “future” kwa watoto wetu wala kizazi kijacho!

Tusidanganyane; njia ya foleni kuelekea kwenye mafanikio na utajiri haina “future” kwa watoto wetu wala kizazi kijacho!

Joined
Apr 19, 2018
Posts
83
Reaction score
115
Unafikiri ninapozungumzia habari za kuondoka kwenye njia ya foleni na kuhamia mwendokasi ninazungumzia ubinafsi wako na kupenda sifa kwako? Eti umesoma, una cheo, mtaa mzima wanakujua, kampuni yote wewe ndo wewe, na una vyeti kama vyote! Ninazungumzia habari za watoto wako na mamilioni ya kizazi kijacho walioko mashuleni hivi leo, ambao future yao, iko matatani na hakuna anayejali kuhusu hilo!

Kwa sababu wewe mwenzangu uko mbele kwenye safari hii, haujali kuhusu kundi kubwa la wadau walioko nyuma yako tena wana magari mapya(fani, ujuzi na maarifa mapya). Umezuia njia, hutaki kwenda na wanaotaka kwenda hawawezi kwa sababu wewe tayari uko mbele yao. unafikiri serikali inapotangaza nafasi za ajira 100, na wanaenda watu zaidi ya 6000 kung`ang`niana hizo post chache ni sifa? Ukiendelea kubaki hapo ni nani atakayewatengenezea ajira vijana mamilioni walioko mashuleni leo, ukiacha hao wanaozunguka mtaani na bahasha za kaki?

Sijali kuhusu wewe, ninajali watoto wako ambao hawatarithi hicho cheo chako, vyeti vyako, au sifa zako. Na pia ninazungumzia kizazi cha kesho ambao tukiendelea kuwachochea kama unavyofanya wewe kwa watoto wako ukitumia lugha ya “Kifoleni” kuwadanganya; wataishia pabaya. Unawafariji, someni kwa bidii mtapata ajira, utafikiri hizo ajira unatoa wewe. Hata kama watoto wako watapata hizo ajira, watoto wa wenzako unawaachia wapi? Nakuuliza kizazi kijacho tunawapeleka wapi?

Tuwaambie watoto wetu wasome wawe na maarifa na ujuzi ili watengeneze ajira kwa wengine, watoe mchango kwa wengine, wawaokoe wengine wanaohangaika na kukosa ajira, njaa, maradhi, majanga na vita. Hayo ndiyo matumizi sahihi ya Maarifa na ujuzi waliopata; ni kutatua matatizo ya wengine, na siyo kufikiria habari za kujaza matumbo yao wakati kuna utitiri wa wenzao wanahangaika mtaani, Lazima watoto wetu wafikirie tofauti.

Kama sasa hivi tu, tatizo la kukosa ajira liko namna hii, hiyo miaka 10 au 20 mbeleni unafikiri itakuwaje. Huyo mtoto wako unayempamba asome, akaajiriwe atakuwa salama kweli?. Acha ubinafsi wewe, akili ya namna hiyo inadidimiza kizazi kijacho. Tunawahukumu watoto wetu vifungo vya bila sababu, wakati umefika sasa tuanze kuwaambia ukweli.

Wakati huo huo sisi wenyewe kwa vitendo, tukisogeza magari yetu kutoka kwenye foleni, ili kutangulia kwa pamoja kupitia mwendokasi, kuwaandalia hizo fursa na ajira watakazo zihitaji. Kama una nia nzuri na kizazi kijacho anza kuhama sasa hivi kuingia mwendokasi, hata kama haujali habari za mtoto wa mtu, usisahau kuwa hao watoto wako hawatarithi hicho cheti, hiyo ajira unayoringia au Vyeo vyako.
NJIA YA FOLENI NA FARAJA YA MAFAO YA UZEENI (PENSION)
Watu wa njia ya foleni wanapenda sana kusikia habari za mafao ya kustaafu kazi. Sijajua, pengine ni faraja ya moyo kutokana na “Jam”, wanayopitia kwa hiyo wanaona bora kuwaza kitakachotokea mwisho wa safari yao (uzeeni). Au la, huenda wao wanafikiria njia ya foleni ni njia ambayo haina purukushani (The path of least resistance) kwao.

Sisemi kuwa mafao ni kitu kibaya, isipokuwa badala ya kusubiri; kwa nini usitengeneze fursa ukiwa bado kijana kwa ajili yako na vijana wenzako, halafu ukaanza kula hizo bata ikiwa bado mapema?. Ninajua unachoogopa, umekaa kwenye foleni wakati upande wako kulia kwako kuna njia ya mwendokasi tena tupu kabisaa,! unaogopa Risk. Unahisi ukiingia huko na kigari chako hicho kitaishia kugongwa au kuachwa mbali sana.

Ni kipi bora kwako? Kuingia kwenye njia ya mwendokasi ili ukutane na ukweli wa mambo kwamba kigari chako kibovu, hakifai, na kina spidi ndogo AU kuendelea kubaki kwenye njia ya foleni huku umejaa hofu na kujidanganya kuwa kuna wenzako wako nyuma halafu wewe umetangulia mbele?
NJIA YA FOLENI INAFICHA UDHAIFU
Njia ya foleni inaficha udhaifu mwingi ulionao.

Kwanza; gari yako hiyo (Fani, taaluma au ujuzi ulionao), haujawahi kuifanyia Upgrade tangu uinunue miaka mingi iliyopita, jambo linalopelekea wewe kuwa na spidi ndogo (Katika uzalishaji), ukilinganisha na Magari mapya yaliyoingia sasa hivi kutoka kiwandani (Vijana waliotoka kusoma na wana ujuzi mpya). Lakini kutokana na kanuni za njia ya Foleni wamekwama, hawawezi kukufikia hapo ulipo wala hawawezi kuonyesha spidi zao mpya walizotoka nazo huko. Jambo hili linapelekea wewe kujidanganya kuwa uko mbele yao na wakati kiuhalisia wote mko kwenye shimo moja.​

Pili; Unaogopa sana mabadiliko; utatafuta visingizio vya kila namna Mara ooooh..............................................................SEHEMU INAYOFUATA.
 
Hatari sana. Huu umati ulioko secondary ukiingia mtaani halafu baada ya 2025 mwendo ukawa ndio huu huu uliopo sasa sijui itakuwaje. Maana kuna wanaosubiri jamaa amalize ili wapumue kumbe kikaja chuma kingine.
 
Poor and middle class people prepare their kids to work for money but rich people have money to work for them by robert kiyosaki
 
Unakuta mtu kapata ka cheo tu anageuka motivation speaker kwa vijana"Vijana wavivu sana hamjitumi kama tulivokua sisi zamani " sawa wapo wavivu ila sio mtu akiwa na cheo ndio aanze kuwasema vibaya walio chini kama hajatoa fursa kwao
 
Mimi nashukuru sana ninapoona kumbe kuna watu wanafikiri kama mimi, huwa mara nyingine najionaga pengine mi mtu wa ajabu.
ntakupa mfano RAHISI sana.

Sasa hivi watoto wa wengi sana wanawapeleka shule binafsi ambako mtoto wa darasa la kwanza anaingia darasani saa 1.00 asubuhi, anatoka saa 10.00 jioni anarudi na homework, watu weeeengi tunaona hii ndo elimu.

Jamani mtoto asome hadi saa 5 asubuhi arudi asome maisha ya'' mtaa''. ajifunze usanii, kuimba, kukimbia , kutengeneza simu, wizi, kuendesha bodaboda, kuuza duka la baba, kupanda mahindi, kucheza mpira, hii staili tunayojidanganya nao ya kusoma masaa 24, mtakuja kuniambia !!!
 
mi nashukuru sana ninapoona kumbe kuna watu wanafikiri kama mimi, huwa mara nyingine najionaga pengine mi mtu wa ajabu.
ntakupa mfano RAHISI sana. sasa hivi watoto wa wengi sana wanawapeleka shule binafsi ambako mtoto wa darasa la kwanza anaingia darasani saa 1.00 asubuhi, anatoka saa 10.00 jioni anarudi na homework, watu weeeengi tunaona hii ndo elimu.
jamani mtoto asome hadi saa 5 asubuhi arudi asome maisha ya'' mtaa''. ajifunze usanii, kuimba, kukimbia , kutengeneza simu, wizi, kuendesha bodaboda, kuuza duka la baba, kupanda mahindi, kucheza mpira, hii staili tunayojidanganya nao ya kusoma masaa 24, mtakuja kuniambia !!!
😀😀😀 watakuja tu kusema yote!
 
mi nashukuru sana ninapoona kumbe kuna watu wanafikiri kama mimi, huwa mara nyingine najionaga pengine mi mtu wa ajabu.
ntakupa mfano RAHISI sana. sasa hivi watoto wa wengi sana wanawapeleka shule binafsi ambako mtoto wa darasa la kwanza anaingia darasani saa 1.00 asubuhi, anatoka saa 10.00 jioni anarudi na homework, watu weeeengi tunaona hii ndo elimu.
jamani mtoto asome hadi saa 5 asubuhi arudi asome maisha ya'' mtaa''. ajifunze usanii, kuimba, kukimbia , kutengeneza simu, wizi, kuendesha bodaboda, kuuza duka la baba, kupanda mahindi, kucheza mpira, hii staili tunayojidanganya nao ya kusoma masaa 24, mtakuja kuniambia !!!
Hapa ndonimekuelewa zaid. Hii ni nondo
 
Back
Top Bottom