Tusidanganyane :Sioni uwezekano wa watu kuandamana 7/7.

Niko naandamana zangu kitambaa cheupe na Serengeti Zangu.

Kesho nalala kama mpumbavu.
 
Haya mambo ya maandamano 90% yanasikika mitandaoni tu ila tukija kwenye uhalisia wa maisha halisi hakuna mtu anayezungumzia kabisa.

Zimebaki siku chache lakini sioni kabisa uwezekano wa kuandamana.

Hii itakuwa ni sawa na ile 9 December.
Hakuna anayeandamana tena hii nchi baada ya MO29. Hakuna na hatakuwepo tena.
 
Na AFCON ndio imefanya haya maandamano ya sasa yasifanikiwe maana Kwasasa Wanalinda kwa kadri wawezavyo PICHA YA NCHI ISICHAFULIWE

Maana ikichafuka AFCON ikighairishwa kuchezewa TANZANIA ikaishia kwa majirani

Na yale mahela yanayotumika kuandaa ule uwanja pale ARUSHA...aseee itakua mbayaa

Kwahiyo naamini kama kuna MUDA NA KIPINDI MAGEREZA YAMEFURIKA WATU ni utawala wa huyu mama.

Hada Hasa nyakati hizi... Ukijiona upo Uraiani unatembea tuna comment huku Mtandaoni JUA hatuna madhara.

Wenye madhara WOTE washadhibitiwa wamebaki wachache wasio nchini na wachache sana walio wazidi watawala akili.

Lakini Kama kuna mtu wamehisi tu ni hatari wamemchukua yupo keko na Upanga uko.

HIii NCHI tuitazame hv hv lakn kuna yanayoendelea kimya kimya sio poa.

Yote kwa yote Tunaweza kushangazwa PIA hata ya 29th oct tulisikia TOKENI MKAPIGE KURA MRUDI, watu wakatoka wengine mpka wakarudi majumbani saa 4 saa 5 asubuhi kilipoanzia hamna ajuae ilianzia wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…