Pre GE2025 Tusidanganyane, Tanzania hakuna Mtu yeyote anayeweza kuzuia Kufanyika kwa Uchaguzi mkuu

Pre GE2025 Tusidanganyane, Tanzania hakuna Mtu yeyote anayeweza kuzuia Kufanyika kwa Uchaguzi mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kimsingi Tundu Lissu asijidanganye kujipa matumaini ya kuwa eti siku moja atakuwa Rais wa Tanzania. ASIJIDANGANYE kabisa, maana tulikuwa na watu WAROPOKAJI na maarufu kuliko yeye na waliishia kuiona Ikulu wakiwa wanakatiza kwenye ferry au wakienda wizara ya elimu pale Magogoni. Mfano ni Christopher Mtikila, Agustino Lyatonga Mrema, Edward Lowassa, Maalim Seif Shariff Hamad etc
Tundu Lissu, ni msomi na anjua fika kuwa ni very unrealistic yeye kuja kuwa Rais wa JMT
 
Dola tulivu hulindwa kwa njia yoyote iwayo.....

Sudan hapakaliki.....
DRC ndiyo hivyo.....

Wabelgiji wale wa KONGO ya zamani leo wamekuja na mbinu mbadala.... DEMOKRASIA ya rafiki wa Brussels ndg.Tundu Lissu.....

Tanzania ndio "shockabsorber" ya utulivu wa maeneo yetu haya.....wameamua kutuingiza katika matatizo ili kuikomesha hiyo "shockabsorber"....

Demokrasia gani ya kuziingiza nchi katika matatizo makubwa na yenye gharama kubwa?!!

Tuwapuuze wajinga na wapumbavu.....

#Nchi Kwanza !!
Sio wizi wa kura kwanza? Au nchi maana yake ni ccm kukaa madarakani kwa shuruti?
 
Ukisikia ubwege ni kama huu ulioandika.

Yaani unashindwa kujua kuwa katiba yetu inatamka wazi kuwa ni jukumu la kila raia kuzuia uhalifu unapoonekana ni dhahiri.

Wananchi wote wenye akili timamu na wazalendo wa kweli, tuungane kuzuia ushetani wa Mwenyekiti wa CCM na CCM.
Sasa uchaguzi wa Kikatiba ni uhalifu?!
 
wizi wa kura ni pambio la excuses , kama chama majimbo waliyoshinda hayafiki hata 50 % ya 1/3 ya viti vyote, ndyo unaamini urais alishinda pia? 😎
Kama ni excuse kwanini CCM hawataki kusikia uundwaji wa tume huru ya uchaguzi na upatikanaji katiba mpya itakayoweka migawanyo kwenye mihimili ya utawala kuwa huru?
 
Kimsingi Tundu Lissu asijidanganye kujipa matumaini ya kuwa eti siku moja atakuwa Rais wa Tanzania. ASIJIDANGANYE kabisa, maana tulikuwa na watu WAROPOKAJI na maarufu kuliko yeye na waliishia kuiona Ikulu wakiwa wanakatiza kwenye ferry au wakienda wizara ya elimu pale Magogoni. Mfano ni Christopher Mtikila, Agustino Lyatonga Mrema, Edward Lowassa, Maalim Seif Shariff Hamad etc
Ni kweli, rais wa Tanzania ni yule unayemtaka ww.
 
Hilo la Lisu kuwa Rais linawezekana kwa sababu Mkapa na Magufuli Hakunaga Mtu aliamini wangekuwa Marais 😄😄

Wapiga Kura wa Tanzania humchagua Mtu yoyote yule Ndio sababu Babu Tale yuko Bungeni
Mkapa na Magufuli ni watu wa low profile ndiyo maana walipata. Nchi hii wanaoutaka uRais sana huwa hawapati. Ndiyo hoja yangu
 
Kama ni excuse kwanini CCM hawataki kusikia uundwaji wa tume huru ya uchaguzi na upatikanaji katiba mpya itakayoweka migawanyo kwenye mihimili ya utawala kuwa huru?
jitahidini kufanya kazi kwenye mazingira magumu ili mukomae kisiasa
 
Ndio uondoe ujinga wako wakusema Tanzania inaongozwa kwa misingi ya sheria chini ya katiba.

Katiba inarepiwa blatantly.
Uzuri ni DOLA iko makini kuilinda Katiba na hii siyo kwa Uhuni wa Wapinzani tu bali hata alipokufa Shujaa Magufuli CDF alihakikisha anailinda Katiba ya JMT ya 1977 na marekebisho yake 🐼
 
Uliamini Halima Mdee aliibiwa Kura Kawe? 😂😂😂
Unataka kusema hapa alijiibia?

Na kwanini shujaa uchwara alizima internet kuanzia siku ya uchaguzi hadi kuapishwa?
images (36).jpeg
 
jitahidini kufanya kazi kwenye mazingira magumu ili mukomae kisiasa
Mifumo ya kidemokrasia ipo kuondoa hilo ombwe la mazingira magumu kila kitu kinakaa kwenye sehemu yake na mipaka inakuwepo.
 
Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya Sheria Chini ya Katiba ya JMT

Tanzania haina kifungu cha Katiba wala Sheria kinachoruhusu MTU au Kikundi Cha Watu kuzuia Uchaguzi mkuu

Msikubali Kudanganywa Kibwege bwege

Ahsanteni sana 😄
Fear fools. Especially when they band together.

Watawala wengi wenye nguvu wanaondolewa madarakani siyo kwa kukosa nguvu au vyombo vya dola. Ni kwa sababu ya kiburi kwamba watatumia dola kubaki madarakani. Fatal mistake!!!!
 
Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya Sheria Chini ya Katiba ya JMT

Tanzania haina kifungu cha Katiba wala Sheria kinachoruhusu MTU au Kikundi Cha Watu kuzuia Uchaguzi mkuu

Msikubali Kudanganywa Kibwege bwege

Ahsanteni sana 😄
Wananchi wote kugoma kwenda kupiga kura Oktoba 2025 kutokana na elimu wanayopata kutoka kwa viongozi wa Chadema hii tayari ni mbinu ya kuzuia uchaguzi . Ccm mnaweza kulazimisha ushindi kwa wizi wa kura lakini wananchi watakuwa hawamtambui rais na serikali.Pia jumuiya ya kimataifa itakuwa hawamtambui rais.Muda ni mwalimu mzuri na huu ni wakati wa Lissu.
 
CCM mnajicganya au ndio mmepoteza ufahamu, kwani Lissu amekwisha tangaza nia ya kugombea urais, au kupitishwa na Mkutano mkuu wa Chadema?
 
Wananchi wote kugoma kwenda kupiga kura Oktoba 2025 kutokana na elimu wanayopata kutoka kwa viongozi wa Chadema hii tayari ni mbinu ya kuzuia uchaguzi . Ccm mnaweza kulazimisha ushindi kwa wizi wa kura lakini wananchi watakuwa hawamtambui rais na serikali.Pia jumuiya ya kimataifa itakuwa hawamtambui rais.Muda ni mwalimu mzuri na huu ni wakati wa Lissu.
Ati wananchi wote duh ! nimecheka sana, wewe jamaa unaishi Bongo kweli ? Elimu gani ambayo wabongo unaweza kuwaschool na kuwafool kifala.
 
Hao wabunge wengi wanapatikanaje bila tume huru? Ndivyo mnavyojidanganya?
Kwanza tume huru sio jambo la kuikalili tu,hiyo tume huru haigozwi na Malaika wa mbinguni wala Ummoja wa nchi za Ulaya au Marekani. Tume huru ni kundi la watu tena Watanzania wanaongoza taasisi ya serikali.Hakuna jambo jipya mpaka hapo.
Je nani atapima weledi wa tume hiyo kama si mahakama zetu?
Huko Kenya walijitambulisha kama wametunga katiba mpya na kuunda tume huru.
On paper tuliwaona wapo juu licha kucopy na kupaste katiba ya Marekani.
Lakini ebu twende reality check ni ngumi,mapambano ni maadamano ya kumwaga damu kwa maefu kila uchaguzi mkuu.
Ni vurungu kwa jina la tume huru,ni kusweka ndani na kuzota jela,ni kesi zisizoisha mahakama kuu kila uchaguzi na latest ni vurugu za Gen Z zilizopoteza maefu ya maisha na kupotea au kuangamiza mali za wananchi.
Hakuna tofauti ya mlalamika na mlalamikiwa,wote wakipata nafasi ni chumia tumboni,bora mimi akina pangu pakavu.Mwisho wamehamia makanisani kutumia nyumba za Mungu kuhubiri ukabila,umimi na uzandiki,ndio Kenya ya leo ambayo anadaiwa hadi kiama.
Ni siasa za kilaghai kwa jina la demokrasia.

Kwa kumalizia kutaja tu tume huru bila componets zake kuzipima kuona mapungufu yake,ndio mambo ya kila mara kuunda tume akina Warioba ambazo by the end of day hazifanyi kazi ni wastage of public monies.
Wake up.
 
Back
Top Bottom