Tusidanganye, Rest in Peace (RIP) haipatikani bure; lazima uishi maisha mema kwanza

Tusidanganye, Rest in Peace (RIP) haipatikani bure; lazima uishi maisha mema kwanza

Kama ulimwengu ungekuwa umetokea pasipo kujulikana basi amini nakwambia pasingekuwapo kitu kinachoitwa lugha kwa wanadamu tungekuwa kama wanyama tu, hebu angalia lugha za jamii tofauti tofauti za wanadamu zilivyo na mpangilio halafu tafakari vizuri ujiulize ni nani alizipangilia hizi lugha, na kwanini wewe kuna lugha unazijua na zingine huzijui.
Kwa hiyo mimi kujua Kiswahili sijui Kireno ni uthibitisho Mungu yupo?

Unaelewa hata uthibitisho ni nini?

Unahakikisha vipi suala la lugha tofauti halijatokana na watu tofauti kukaa sehemu tofauti tu?
 
Kwa hiyo mimi kujua Kiswahili sijui Kireno ni uthibitisho Mungu yupo?

Unaelewa hata uthibitisho ni nini?

Unahakikisha vipi suala la lugha tofauti halijatokana na watu tofauti kukaa sehemu tofauti tu?
nilikwambia tunamtambua Mungu kupitia ishara zake. Ukasema nikupe moja ya ishara zake nikakupa moja ya ishara ni hiyo umeikataa. Umesema kwamba suala la lugha tofauti limetokana na watu tofauti kukaa sehemu tofauti tu, Je nani alizianzisha hizo lugha?
 
Acheni kiburi cha uzima, mwabuduni Yesu Kristo. Siku za mwisho zipo karibu. Hapa duniani tunapita. Miaka ya kuishi ya mwanadamu ni 60 hadi 80, baada ya hapo anakufa.

Baada ya kifo, ndio mwanzo wa hukumu unaanza hapo. Rest in Peace haipatikani bure; lazima mtu aingie gharama ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu aliyeziumba mbingu na nchi. Maisha yale aliyoyaishi Yesu Kristo. Huwezi kuacha dhambi bila kumfuata Yesu Kristo. Huwezi kuacha dhambi kwa kujiongoza mwenyewe.

Dini za Kiafrika zilikosa sifa ya maisha matakatifu, haziwezi kumpeleka mwanadamu kwenye Rest in Peace. Tubuni ingali bado ni wazima wa afya. Msijifanye welevu wakati hata siku za kuzaliwa kwenu mlikuwa hamzijui. Je, mlijua mtazaliwa lini? Tumwabudu Yesu Kristo.

Yesu ndio njia ya kweli na uzima. Ndiye atakayekufanya mawazo yako yawe mazuri na matakatifu, maneno yako yawe mazuri na matakatifu, na matendo yako yafae mbele za Mungu aliyeziumba mbingu na nchi. Ndiye pekee atakayekufanya uingie peponi, mahali penye amani. Mtu anayestahili Rest in Peace ni mtu yule aliyefanikiwa kufuata maisha ya Yesu Kristo pekee.

Mbali na hivyo, mtu huyo lazima aende kuzimu, kwenye giza na mateso, huku akisubiri hukumu yake ya mwisho. Tuache kiburi. Ukweli ndio huo. Kazi kwako; kupanga ni kuchagua.
Kiranga
 
nilikwambia tunamtambua Mungu kupitia ishara zake. Ukasema nikupe moja ya ishara zake nikakupa moja ya ishara ni hiyo umeikataa. Umesema kwamba suala la lugha tofauti limetokana na watu tofauti kukaa sehemu tofauti tu, Je nani alizianzisha hizo lugha?
Lugha zimeanzishwa na watu. Uanzishwaji na ukuaji wa lugha ni sehemu ya asili ya watu kutumia akili zao, hiki halihitaji Mungu.

Kwa nini unaona lugha ni lazima iwe inaonesha uwepo wa Mungu?

Kwanza kabisa, lugha ina mapungufu mengi sana kuelezea uhalisia (sehemu nyingine tunahitaji hesabu kuelezea mambo), Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo na angekuwa ndiye kaanzisha lugha, tungekuwa na lugha nzuri zaidi ya hii.
 
Ok, kwa unavyo ona wewe basi tuambie sisi binadamu chanzo chetu nini?
 
Mfupawasokwe Kwa maongezi ya kisomi kuhusu lugha ilivyoanza soma kitabu cha Steven Pinker "The Language Instinct: How The Mind Creates Language".
 
Back
Top Bottom