Acheni kiburi cha uzima, mwabuduni Yesu Kristo. Siku za mwisho zipo karibu. Hapa duniani tunapita. Miaka ya kuishi ya mwanadamu ni 60 hadi 80, baada ya hapo anakufa.
Baada ya kifo, ndio mwanzo wa hukumu unaanza hapo. Rest in Peace haipatikani bure; lazima mtu aingie gharama ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu aliyeziumba mbingu na nchi. Maisha yale aliyoyaishi Yesu Kristo. Huwezi kuacha dhambi bila kumfuata Yesu Kristo. Huwezi kuacha dhambi kwa kujiongoza mwenyewe.
Dini za Kiafrika zilikosa sifa ya maisha matakatifu, haziwezi kumpeleka mwanadamu kwenye Rest in Peace. Tubuni ingali bado ni wazima wa afya. Msijifanye welevu wakati hata siku za kuzaliwa kwenu mlikuwa hamzijui. Je, mlijua mtazaliwa lini? Tumwabudu Yesu Kristo.
Yesu ndio njia ya kweli na uzima. Ndiye atakayekufanya mawazo yako yawe mazuri na matakatifu, maneno yako yawe mazuri na matakatifu, na matendo yako yafae mbele za Mungu aliyeziumba mbingu na nchi. Ndiye pekee atakayekufanya uingie peponi, mahali penye amani. Mtu anayestahili Rest in Peace ni mtu yule aliyefanikiwa kufuata maisha ya Yesu Kristo pekee.
Mbali na hivyo, mtu huyo lazima aende kuzimu, kwenye giza na mateso, huku akisubiri hukumu yake ya mwisho. Tuache kiburi. Ukweli ndio huo. Kazi kwako; kupanga ni kuchagua.