Tusifunge mjadala, Mshahara wa Mbunge kwa mwezi ni 12,892,000

Mi nadhani wangelipwa kipindi tu cha mikutano maana pasipo mikutano ya bunge mbunge anafanya kazi gani zinazompa stahiki hizo?
Mfanyakazi wa umma anafanya kazi masaa 8 kila siku na average ya mshahara kwa siku ni shilingi 22,000-46,000 kwa ofisa na daktari huku mbunge ( hata asiyesoma) akilipwa shilingi 409,700 kwa siku ikiwa ni mara 20 na 10 kwa ofisa na daktari anaefanya kazi saa 8 kila siku.
This is totaly not equitable.
 
Hivi mmerogwa? Si umetuonyesha scale na mshahara wa mbunge sasa posho zinakuwaje mshahara?
Labda afute neno mshahara na badala yake aweke neno kipato Cha Mbunge kwa mwezi kutokana na ubunge wake hata hivyo maana itabaki pale pale kuwa wao wanapata kikubwa kuliko wengine na hawakatwi kodi Kama wengine
 
Nafurahi umelileta hili suala la mishahara ya wabunge kwa mjadala.
Kwenye kipindi cha Cyberlaunge kilichokuwa kinajadili kitabu chake alichokizindua juzi Tundu Lissu aliulizwa swali na Dr Lwaitama kuhusu mishahara ya wabunge. Jibu alilolitoa ni kama ilivyoelezwa hapa yaani mishahara ya watumishi na matumizi mengine ya kiofisi yamewekwa humo ndiyo maana inaonekana mikubwa. Ninamheshimu sana Tundu Lissu kutokana na msimamo wake juu ya masuala mbalimbali lakini kwa hili lazima nikiri tuko mithili ya usiku na mchana. Yeye anasema badala ya Watanzania kulalamikia mishahara ya wabunge wailalamikie serikali iwaongezee mishahara watumishi wengine ili ifanane na ya wabunge. Swali langu ni kwa uchumi gani? Hebu fikiria madaktari na walimu na kada zingine zenye majukumu muhimu ya kitaifa wangelipwa kiasi hicho hela hiyo ingetoka wapi? Na je kuna uhalali gani wa mbunge aliyetumikia nchi kwa miaka 5 kulipwa million 200 na daktari aliyetumikia kwa miaka 30 kulipwa sehemu tu ya kiasi hicho tena wakati mwingine kwa kuchelewa? Inapofika hapo mimi huwa nachelea na kujiuliza hivi hao wanaoonekana kutetea wananchi wanafanya hivyo kwa maslahi ya wananchi kweli ama maslahi yao ya mrefu na mfupi?
 
Hivi mmerogwa? Si umetuonyesha scale na mshahara wa mbunge sasa posho zinakuwaje mshahara?
Wewe acha ubwege. Wamezichomoa kwenye mshahara,wakazipachika kwenye maposho posho kama hayo,ili mjinga kama wewe usishtukie (ndio kama hivi kweli umelala bado). Waambie wampatie na mwalimu na nesi na doctor maposho posho kama hayo na kisha mshahara. Maana hao wana kazi kubwa kuliko hayo mandiooooo
 
Ficha upumbavu wako- sasa kama imechomolewa wewe bado unaendelea kuzungusha-si ndio wehu huo.
 
Ndio maana issue ya mishahara ilipwe kodi wanaweza wakasema sawa na wakashusha mishahara hadi elfu 50 kwa mwezi alafu kisiri siri bila kujua wakaongeza posho kwa milioni kadhaa...

Hawa jamaa hata idadi yao tu ni kansa kwa taifa....
 
Nasimamamia hoja ya kwamba Mshahara ni 4,600,000/=. Unless hatujui maana ya "mshahara" ndio inakuwa 12,892,000/=.
 
Nyongeza tu ni kwamba mbunge baada ya miaka 5 anapewa hizo mil.200+ wakati hakuwa nakatwa PSSF wakati mwalimu, daktari na watumishi wengine wanalipwa kiinua mgongo kinachotokana na makato ya PSSF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…