Tusijidanganye hukuna timu yoyote ya Tanzania ikiwepo Simba yenye mafanikio kimataifa

Malata Junior

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Posts
3,104
Reaction score
2,550
Nafuatilia mjadala wa kijinga unaoendelea kwamba eti kwa nini Yanga inafeli kimataifa wakati Simba inafanikiwa!

Ili timu iwe imefanikiwa katika mashindano ni lazima ichukue ubingwa na si vinginevyo kwa hiyo timu zenye mafanikio Afrika ni Al Ahly,Zamalek,Esperance,Raja Casablank,TP Mazembe,Mamelod Sundown na nyingine chache zilizowahi kubeba vikombe vya Afrika.

Huu ujinga ndiyo unafanya timu kubweteka kisa imeingia makundi halafu inaenda kupigwa inarudi bila kombe na kubaki wasindikizaji tu! Bora hata Yanga msimu uliopita ilibeba ngao ya hisani, kombe la ligi kuu na kombe la shirikisho la Azam kuliko Simba haina kombe lolote!
 
ni kweli lkn ndo ivyo MCHUNGU KWELIKWELI aisee..
 
Usitafute faraja kupitia matatizo yako kwa kujipa matumaini kuwa hata kama jana ulilala na njaa na hauna kazi ya kukuingizia kipato cha kujikimu kimaisha.

Hivyo basi haupaswi kuhuzunika eti kwakua tu Addidas wame sign out mkataba na Kanye West na kumfanya awe bankrupted, hivyo wewe na Kanye West wote mnapitia hali sawa kwakua hata huyo Kanye west hajawahi kuwa bilionea namba 1
 
Nafuatilia mjadala wa kijinga unaoendelea kwamba eti kwa nini Yanga inafeli kimataifa wakati Simba inafanikiwa! Ili timu iwe imefanikiwa katika mashindano ni lazima ichukue ubingwa na si vinginevyo kwa hiyo timu zenye mafanikio Afrika ni Al Ahly,Zamalek,Esperance,Raja Casablank,TP Mazembe,Mamelod Sundown na nyingine chache zilizowahi kubeba vikombe vya Afrika. Huu ujinga ndiyo unafanya timu kubweteka kisa imeingia makundi halafu inaenda kupigwa inarudi bila kombe na kubaki wasindikizaji tu! Bora hata Yanga msimu uliopita ilibeba ngao ya hisani, kombe la ligi kuu na kombe la shirikisho la Azam kuliko Simba haina kombe lolote!
Kwa akili za namna hii tutaendelea kulaumu viongozi kila siku

Sio siri mnampa mzigo mkubwa sana Raisi wetu wa nchi kuwa na raia wa aina yako.
 
Alafu ukute huyu alieandika huu uzi ni baba kabisa mwenye watoto na mke.

Iko hivi, kwa vilabu vyetu kufikia japo group stage ni mafanikio makubwa sana, ikumbukwe kuwa kucheza hatua ya group stage hapa Africa ni hatua kubwa sana.

Ni kama ulaya timu kumaliza zile nafasi nne za juu ni hatua kubwa sana kucheza ile michuano mikubwa barani ulaya hata usipokuwa bingwa.

Kwa nchi za wenzetu walioendelea kufuzu tu kucheza ile michuano vilabu vinavuta mpunga wa kutosha.

Hivyo yanga wasijifiche kwenye hichi kimvuli cha kuona kucheza group stage si chochote, nakumbuka kuna mwaka yanga walifuzu kucheza group stage caf federation cup kwa furaha ya mashabiki walikisukuma basi lililokuwa limebeba wachezaji kutoka airport mpaka makao makuu ya club kwa furaha.

Yanga kwa sasa kubalini tu kwa sasa kimataifa simba wamewaacha mbali sana.
 
Nafuatilia mjadala wa kijinga unaoendelea kwamba eti kwa nini Yanga inafeli kimataifa wakati Simba inafanikiwa! Ili timu iwe imefanikiwa katika mashindano ni lazima ichukue ubingwa na si vinginevyo kwa hiyo timu zenye mafanikio Afrika ni Al Ahly,Zamalek,Esperance,Raja Casablank,TP Mazembe,Mamelod Sundown na nyingine chache zilizowahi kubeba vikombe vya Afrika. Huu ujinga ndiyo unafanya timu kubweteka kisa imeingia makundi halafu inaenda kupigwa inarudi bila kombe na kubaki wasindikizaji tu! Bora hata Yanga msimu uliopita ilibeba ngao ya hisani, kombe la ligi kuu na kombe la shirikisho la Azam kuliko Simba haina kombe lolote!
Wewe kinachokusumbua ni mwikombelenyuma ni unyafuzi kwenye ubongo~mafanikio ni pamoja na kufika hatua ya juu kwenye mashindano maana bingwa huwa ni mmoja,sasa UTO HAINA UWEZO WA KUFIKA hatua yoyote unategemea useme nini wewe timu mkosi?
 
Ndani ya Tanzania, Simba na Yanga ni giants, ila kwa nje ya Tz yanga maarufu Congo DRC tu labda.

Simba kimataifa ni brand kubwa mno, mpaka wale Queens wanafanya vzr huko.
 
Nafuatilia mjadala wa kijinga unaoendelea kwamba eti kwa nini Yanga inafeli kimataifa wakati Simba inafanikiwa! Ili timu iwe imefanikiwa katika mashindano ni lazima ichukue ubingwa na si vinginevyo kwa hiyo timu zenye mafanikio Afrika ni Al Ahly,Zamalek,Esperance,Raja Casablank,TP Mazembe,Mamelod Sundown na nyingine chache zilizowahi kubeba vikombe vya Afrika. Huu ujinga ndiyo unafanya timu kubweteka kisa imeingia makundi halafu inaenda kupigwa inarudi bila kombe na kubaki wasindikizaji tu! Bora hata Yanga msimu uliopita ilibeba ngao ya hisani, kombe la ligi kuu na kombe la shirikisho la Azam kuliko Simba haina kombe lolote!
Mwagito acha wivu.Haukusaidii zaidi ya kukutengenezea ndita kwenye paji la uso.
 
Nafuatilia mjadala wa kijinga unaoendelea kwamba eti kwa nini Yanga inafeli kimataifa wakati Simba inafanikiwa! Ili timu iwe imefanikiwa katika mashindano ni lazima ichukue ubingwa na si vinginevyo kwa hiyo timu zenye mafanikio Afrika ni Al Ahly,Zamalek,Esperance,Raja Casablank,TP Mazembe,Mamelod Sundown na nyingine chache zilizowahi kubeba vikombe vya Afrika. Huu ujinga ndiyo unafanya timu kubweteka kisa imeingia makundi halafu inaenda kupigwa inarudi bila kombe na kubaki wasindikizaji tu! Bora hata Yanga msimu uliopita ilibeba ngao ya hisani, kombe la ligi kuu na kombe la shirikisho la Azam kuliko Simba haina kombe lolote!
Sikutegemea andiko la namna hii nilikute humu jf kwenye great thinkers, kule facebook au Instagram ni kawaida ila huku mh,hivi hujiulizi kwanini caf wanatoa zaidi ya bil 1 kwa kufika makundi ?unasema sio mafanikio!bila kufika hatua hizo ungekusanya point za kupeleka timu 4?,kwa hiyo nyinyi uto mtajikuta tu mmechukua kombe bila kupita makundi wala robo fainali si ndio?bora anaebeza angekuwa kashafikia hizo hatua,lakini mmejawa na wivu tu.
 
Back
Top Bottom