Uchaguzi 2020 Tusimuache Lissu atuahidi yasiyowezekana

Uchaguzi 2020 Tusimuache Lissu atuahidi yasiyowezekana

Ahadi za TL ni sawa na ahadi za mlevi wa Konyagi, kama wameshindwa kujenga hata ofisi ya chama chao wataweza ya kuwajengea Watanzania mahitaji yao? Ruzuku ya 320+ millioni kila mwezi pamoja na michango ya wabunge wao wameshindwa kuwa na ofisi miaka zaidi ya 20 tangu hiki chama kianzishwe na baba mkwe wa mlevi wa konyagi.
Tuambie ccm waliwahi kujenga ofisi wapi ktk Tanzania hii labda umezaliwa kwenye miaka ya themanini kuja tisini. Ungekaa tu kimya maanake hakuna unachojua.
 
Ahadi za TL ni sawa na ahadi za mlevi wa Konyagi, kama wameshindwa kujenga hata ofisi ya chama chao wataweza ya kuwajengea Watanzania mahitaji yao? Ruzuku ya 320+ millioni kila mwezi pamoja na michango ya wabunge wao wameshindwa kuwa na ofisi miaka zaidi ya 20 tangu hiki chama kianzishwe na baba mkwe wa mlevi wa konyagi.
Ofisi iliyopo inatosha kwani kupitia ofisi hiyo hiyo ndipo chadema anaogopwa na na CCM mpaka kubambikiwa kesi kupigwa risasi, je? Chadema wangekuwa na ofisi kubwa zaidi si wangepigwa na Ndege za kivita? Ruzuku ya chadema inatumika kuimarisha chama na pia inatumika kujihami dhidi ya Kesi kesi za wana chadema Nchi nzima walizobambikiwa na CCM ya kishetani, pesa nyingi ya chadema hutumika kujihami dhidi ya hujuma za CCM,
 
TUSIMWACHE LISU ATUAHIDI YASIYOWEZEKANA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kwenye kampeni za Lisu ana Mambo makubwa mawili anayowaomba watanzania wamchague nayo. Moja ni malalamiko yake ya kupigwa risasi hii Kwake Ni Kama Kete ya kuwaomba watanzania wamuonee huruma aingie Ikulu. Jambo la Pili ni Sera zake anazotakiwa awashawishi nazo watanzania ili wamchague kuwa Rais.

Nilishawahi kusema kuwa hakuna siku nitambeza Lisu kwa kupigwa Kwake Risasi na Wala sintoongea nikimuona analalamika kuwa mwili wake una machuma kila Mahali. Kama watanzania wataamua kumchagua kwa kuwa tu aliwahi kushambuliwa na watu wasiojulikana Hilo nimewaachia. Mimi nitajikita kwenye Sera zake ambazo kwangu ndio kipimo Cha kutoa kura yangu kumchagua Kiongozi katika ngazi zote iwe udiwani, Ubunge, au Urais nitazipima Sera kabla ya kuchagua.

Nimesikikiza Sera za mgombea urais Lisu anayo Mambo makuu matatu anayowaahidi watanzania kubwa kabisa ni kila mtanzania kumiki bima ya Afya, kupunguza Makato ya Wanufaika wa Bodi, kuleta maendeleo ya watu badala ya vitu. Haya ndio anayoyarudia kila Mara anaposhika kipaza sauti Leo tuongele moja kesho tutaongele lingine na leo tuanze na Bima ya Afya kwa kila mtanzania.

BIMA BURE

Nimejaribu ku survey nchi nyingi duniani, Ni nchi ipi yenye uwezo wa kuwapa wananchi wake wote Bima BURE sikuona.

Marekani ilijaribu kupitia Obama Care lakini baada ya Muda mfupi walishindwa na Obama care ikafa. Sababu kubwa Ni gharama za uendeshaji. Kutokana na U.S Census Bureau taifa la Marekeni lina watu milioni 28.1 tu ya wasiokuwa na Bima. Hivyo Obama care ilidhamiria kufanya Coverage ya watu milioni 28 tu kuwalipia huduma za Afya lakini wameshindwa kutokana na gharama zake. Hili ni taifa tajiri kuliko yote duniani limeshindwa kuwalipia watu milioni 28 tu je kwa Tanzania wenye Bima hawafikii milioni kumi je milioni Arobaini iliyobakia wanaofanya kazi wataweza kuwalipia gharama hizo?

Sababu nyingine ya wamarekani kukataa Obama care ni kuwa Kama itafanya kazi Kodi ingelipanda sana nchini marekani hivyo wakaamua kuitupilia mbali. Kuna nchi zinazotajwa kuwa na unafuu wa Bima Duniania lakini sio bure naomba kuzitaja:-

1.Ujerumani.

Ujerumani ndio taifa linaloonekana Kama Bima yake angalau Ina unafuu kwa wananchi wake. Lakini pia sio wajerumani wote ambao Wana Bima ya afya. Wafanyakazi wote nchini ujerumani wanalipia Bima zao kwa kushirikiana na waajiri. Wengine waliobakia wanalipia kiasi kidogo Bima zao.

2. Singapore

Singapore wao Wana mfumo wa Bima unaoitwa Medshield ambao serikali kwa asilimia kubwa ndio inabeba gharama za matibabu lakini kila mtu nchini Singapore anatakiwa alipie asilimia 10 ya kipato chako kwenye mfuko huo. Kama ni Mkulima wanakupigia mahesabu asilimia 10 ya unachokipata ulipie kwenye mfuko wa bima, Kama ni mfanyakazi vivyohivyo pamoja na kuwa unaonekaba kuwa mfumo Bora kuliko yote duniani lakini bado unalipiwa na wenye kipato kikubwa bado wanaumia sana kukatwa asilimia 10 kwa ajili ya Bima.

3. Japani

Japani wao Wana mfumo wa Bima unaoitwa SHIS mfumo huu nao watu wanatakiwa kujiandikisha na kulipia.

4. Uingereza.

Wao ndio kwa asilimia kubwa wamefanikiwa kwa kuwa hospital asilimia kubwa zinamilikiwa na serikali na wafanyakazi wote hulipwa na Serikali. Mfumo wao wa Bima wa NHS gharama zake zote hutolewa na Serikali. Ila bado una changamoto na mtu akitaka kutibiwa private ambako Kuna huduma nzuri na za haraka unatakiwa kulipia mwenyewe.

Hizo Zina unafuu Duniania Soma unafuu wake halafu tulinganishe na Tanzania.

Tanzania.

Tuna Bima ya NHIF ambayo huangaika na watumishi wa Umma na wategemezi wao. Huu tunauchangia asilimia Kama mataifa mengine yanavyouchangia. Tena asilimia tatu tu tofauti na mataifa Mengi sana Duniania.

Tuna mfuko mwingine iCHF (Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ulio Boreshwa), huduma hii ya Bima ni kwa gharama nafuu kabisa kwa Watanzania wote katika Sekta ya Afya kwa Familia ya watu sita yaani Baba, Mama na watoto wanne kwa Tsh. 30,000/- tu kwa mwaka mzima. Una pata huduma zoote za matibabu kuanzia kituo kidogo cha Afya mpaka Hospital ya Mkoa.

Serikali Ina mpango pia wa kuleta Sheria Bungeni ya kuwataka watanzania wote kuingizwa kwenye mfuko wa Bima ya Afya.

Mimi nataka kufahamu Lisu anataka kuifanyaje hiyo Bima yake. Sio kwamba nambeza la hasha nataka kufahamu Bima yake anayoihubiri Ina nini ndani na itakuwa inafanana na ya nchi gani.

Tusimwache Lisu atudanganye Kuna haja ya kuchambua haya yanayoongelewa na wanasiasa. Kesho tutachanbua Sera ya Lisu nyingine.

Hoja yangu CHADEMA naomba muwaeleweshe watanzania hiyo Bima yenu ina package gani?

Ole Mushi
0712702602
Uzoefu wangu unaniambia hivi,ccm kwa kujua wamewanyima watanzania elimu kwa maana ya ujuzi na maarifa,ccm kwa kujua kuwa watanzania ni mafukara sana hivyo hawana uwezo wa kutoka nje ya Tanzania,kila Jambo jema kwa nchi yetu huwa wanalipiga sana na watanzania huwaamini Ila baada ya miaka mitano ccm huja na Jambo lile lile walilolipinga kwa nguvu zote five years ago Obama Care was excellent,Trump ameipiga chini kwa akili mbovu zake sawa na huyu kichaa wetu anavyofanya kwa miradi iliyoachwa na mtangulizi,lakini pia siyo kila kilichofeli USA lazima kifeli hapa? mbona kwenye Corona hujilinganishi na USA?
 
Tuambie ccm waliwahi kujenga ofisi wapi ktk Tanzania hii labda umezaliwa kwenye miaka ya themanini kuja tisini. Ungekaa tu kimya maanake hakuna unachojua.
Point. CCM hawajawahi kujenga ofisi. Zote zilijengwa na serikali chini ya chama kimoja. Hivi vitoto vya Instagram ilibidi viombwe hata birth certificates kabla ya kuungwa JF. Unaweza kukuta mwingine kamaliza clinic mwaka juzi leo anaparamia JF.Utaumia, huku kuna think tanks. Hawa wanastahili FB na Insta

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Ahadi za TL ni sawa na ahadi za mlevi wa Konyagi, kama wameshindwa kujenga hata ofisi ya chama chao wataweza ya kuwajengea Watanzania mahitaji yao? Ruzuku ya 320+ millioni kila mwezi pamoja na michango ya wabunge wao wameshindwa kuwa na ofisi miaka zaidi ya 20 tangu hiki chama kianzishwe na baba mkwe wa mlevi wa konyagi.
hii 8000000 ni kupelekana peponi ukiwa unaua
0AE689BC-572A-4051-98CF-12A437491AA7.jpeg
Hiyo je
 
Navyoo fahamu ahadi ya UCHAGUZI sio lazima itekelezeke kwa mwaka mmoja
Inaweza kuwa mchakato wa muda mrefu ila lengo kuuu likiwa nikuhakikisha Kila mtanza napata BIMA YA AFYA nazani LISU amesema na nimemsikia hapa Arusha kwamba Kila MTANZANIA atapata bima kwa gharama nafuu Tena shaba ikiwa Kila MTANZANIA kupata bima nazani nisera nzuri usikimbilie kuwaza KUSHINDWA na pia naaamini tukichukulia sera za wagombea positive itasaidia ata serekali itakayo ingia madarakani kuanagali Kama nijambo jema ikalichukua na kutekeleza watanzania tukanufaika
Hi nchi niyetu sote wazo lakujenga niletu sote
KAMA ELEIMU BURE ILIKUWA YA UPINZANI LEO INATEKELEZWA NA CCM
NA MAMBO YANENDA VIZURII
KUWA MTANZANIA WEKA TANZANIA MBELE USIBABAIKE NA VYAMA JALI SERA KWA MASILAHI YA TAIFA TUSONGE MBELE
SIASA ZA KUPINGANA KWENYE MAENDELEO ZITATURUDISHA NYUMA BADALA KWENDA MBELE
SAWA KADA MTIIFU
 
CCM bwana., Sasa Kama hajui hata package ya bima itakuwaje unasemaje kuwa Ni uongo na haitekelezeki?
Chuoni tunalipia 50,000/= na tunapata Huduma karibu zote labda kama una una kansa ya ubongo na au inahitaji upasuaji mkubwa. Lakini Huduma za afya za kawaida zinapatikana Kama kawaida.
ikabili hoja hapo juu inatekelezeka vip bila jaziba bali kisomi zaidi kwa data na uwaledi bila matusi wala dhiaka
 
Ahadi za TL ni sawa na ahadi za mlevi wa Konyagi, kama wameshindwa kujenga hata ofisi ya chama chao wataweza ya kuwajengea Watanzania mahitaji yao? Ruzuku ya 320+ millioni kila mwezi pamoja na michango ya wabunge wao wameshindwa kuwa na ofisi miaka zaidi ya 20 tangu hiki chama kianzishwe na baba mkwe wa mlevi wa konyagi.
Ofisi za CCM ni ofisi za chadema na vyama vingine CCM warejeshe ofisi za wapinzani waache kumiliki majengo viwanja vya vyama vyote, CCM hawana ofisi zao bali wamevamia na kumiliki ofisi za vyama vyote, baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza rasmi mwaka 1991 ilipaswa majengo ya CCM yote viwanja vyote na mali zote zigawanywe kwa vyama vyote, cha ajabu mpaka sasa CCM wanaishi na kutumia majengo ya chadema na vyama vingine kinyume cha katiba na Sheria, ruzuku ya CCM haitumiki kwa maendeleo ya CCM bali inatumika kuidhoofisha chadema kuu vyama vingi kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwatengenezea propaganda mbalimbali kwa kuwalipa cyprian Musiba na Le mutuz mabilioni
 
Back
Top Bottom