Uchaguzi 2020 Tusimuache Lissu atuahidi yasiyowezekana

Uchaguzi 2020 Tusimuache Lissu atuahidi yasiyowezekana

Kwani yale madege yaliyopaki na yanayokuja pesa zake au zile 1.5Tr/- zilizopotea zilitoka wapi?

Je yule bibi wa kijijini ni lini ata feel impact ya hayo madege?

Acheni kujifanya kuwa pesa za kuliwa au za madege uchwara zipo lakini za kufanyia jamii tija hazipo.

Umeona pesa zitakako toka?
Umetumia akili kuuliza swali au makalio?
Hayo madege yaliyopaki yalipatikana kwa kukusanya kodi na impact yake kwa bibi yako huko kijijini ni kupata maji, barabara, na huduma za afya kwa pesa zitokanazo ma wewe kwa kupanda hizo mdege.

Sisi kama nchi tunahitaji ukusanyaji wa kodi kufikia tirioni tatu hadi tano kwa mwezi ili tuondokane na utegemezi,
Sasa kwa hali ilivyo kwa sasa bado hali hailidhishi kwa makusanyo hayo na ndo maana tunakopa kujazia mahitaji yetu na kulipa kutokana na makusanyo hayo.

Sasa lisu atakapo punguza hiyo kodi ili apate wawekezaji wa nje na aweke mahusiano na hizo nchi, je pesa itapatikanaje maana kiwango cha mapato kitapungua?
Mmekuwa mafundi wa kusema taifa linadaiwa pesa nyingi, je nyie hamtakopa?

Na kwa kuwa deni ni kubwa, sasa hiyo pesa ya kujaza hayo mapengo mtatoa wapi?
Na kama mtakopa ina maana hamjielewi vichwani mwenu mnacho kisimamia?
Hatuwezibkumpa lisu nchi kwa majaribio
Kwa kuwa wawekezaji anao wataka lisu ni wale wa kutunyonya hivy tuaingia utmwani na azima ya ushoga itatimia.
 
Kuandika upuuzi mbele ya jamii ya watu wenye upeo ni kujidhalilisha!Unahisi umeandika cha maana lakini watu timamu tunakuona mpumbav ambaye hujapevuka!JF sio size yako,hamia facebook upeleke mipasho yako!
Tuonyeshe basi matumizi ya hizo pesa, zimefanya nini kama una akiri?
 
Hivi mtaongeza au kupunguza Ajira milioni 8?

Maana miaka 5 ajira zinapungua tu. Au bado hamjaridhika mnataka zipungue zaidi?

Bado tunasubiria 50m hapa.
 
Kuandika upuuzi mbele ya jamii ya watu wenye upeo ni kujidhalilisha!Unahisi umeandika cha maana lakini watu timamu tunakuona mpumbav ambaye hujapevuka!JF sio size yako,hamia facebook upeleke mipasho yako!
Mmezidiwa na CUF amabayo kwa sasa ni ACT wana majengo yao zanziba na hwajawahi kupata ruzuku kama yenu.
 
Bakini kushangilia hata vitu vya kijinga kwa kuwa akili mmemkabidhi T Lisu, kwa hiyo anawaona maboya tu
Kama umeumia basi kunywa dawa utulize maumivu!Karne ya 21 hii na hapa ni JF,msidhani mnaweza kumpangia upande mtu!Tunaojitambua hizi propaganda mfu tunazipuuza!
 
Kwa Hii habari ya chama kikongwe na habari ya kuzalisha ajira milioni 8 ndiyo leo nimeshtuka CCM si wakweli hata kidogo!Mlistahili zaid ya hapa kwenye uhalisia
 
Umetumia akili kuuliza swali au makalio?
Hayo madege yaliyopaki yalipatikana kwa kukusanya kodi na impact yake kwa bibi yako huko kijijini ni kupata maji, barabara, na huduma za afya kwa pesa zitokanazo ma wewe kwa kupanda hizo mdege.

Sisi kama nchi tunahitaji ukusanyaji wa kodi kufikia tirioni tatu hadi tano kwa mwezi ili tuondokane na utegemezi,
Sasa kwa hali ilivyo kwa sasa bado hali hailidhishi kwa makusanyo hayo na ndo maana tunakopa kujazia mahitaji yetu na kulipa kutokana na makusanyo hayo.

Sasa lisu atakapo punguza hiyo kodi ili apate wawekezaji wa nje na aweke mahusiano na hizo nchi, je pesa itapatikanaje maana kiwango cha mapato kitapungua?
Mmekuwa mafundi wa kusema taifa linadaiwa pesa nyingi, je nyie hamtakopa?

Na kwa kuwa deni ni kubwa, sasa hiyo pesa ya kujaza hayo mapengo mtatoa wapi?
Na kama mtakopa ina maana hamjielewi vichwani mwenu mnacho kisimamia?
Hatuwezibkumpa lisu nchi kwa majaribio
Kwa kuwa wawekezaji anao wataka lisu ni wale wa kutunyonya hivy tuaingia utmwani na azima ya ushoga itatimia.
Unadhan katumia makalio kuuliza au Wewe ndo umetumia makalio kufikiri na kujibu? Staha muhimu!
 
Yapo mengi sana waliyo tudanganya hasa lile la walimu kupewa laptop.

Hili ni bomu la kutega ambalo litalipuka muda wowote na wana ccm watalia kilio cha ngamia
Chadema bhana kwa kujipa matumaini😂😂, ilihali mnajua kabisa hamuwezi kushika kukanyaga ikulu😁.
 
Ahadi za TL ni sawa na ahadi za mlevi wa Konyagi, kama wameshindwa kujenga hata ofisi ya chama chao wataweza ya kuwajengea Watanzania mahitaji yao? Ruzuku ya 320+ millioni kila mwezi pamoja na michango ya wabunge wao wameshindwa kuwa na ofisi miaka zaidi ya 20 tangu hiki chama kianzishwe na baba mkwe wa mlevi wa konyagi.

Wewe naona ni mgeni hapa nchini kama ni suala la ofisi hata CCM hawana , nenda vijijini utakuta wamekaa kwenye maghala ya ushirika kama ofisi zao.

Jiulize wana miaka mingapi wanapata ruzuku na bado hawana ofisi tangu Uhuru.
 
Wewe naona ni mgeni hapa nchini kama ni suala la ofisi hata ccm hawana , nenda vijijini utakuta wamekaa kwenye maghala ya ushirika kama ofisi zao.
Jiulize wana miaka mingapi wanapata ruzuku na bado hawana ofisi tangu Uhuru.

Atleast they have a main office, nchi ni kubwa atleast ruzuku wanazitumia znaonekana, karibia ofisi zao nyingi zna hadhi ni sehem chache tu zmebaki ila sasa cdm ata main office mtu anaweza dhan ni gesti
 
atleast they have a main office, nchi ni kubwa atleast ruzuku wanazitumia znaonekana, karibia ofisi zao nyingi zna hadhi ni sehem chache tu zmebaki ila sasa cdm ata main office mtu anaweza dhan ni gesti
Approximately a century now and it is atleast as you said , for how long should they remain primitive.
 
Hiyo millioni 50 imezaa zahanati na umeme wa REA kila kijiji..kumbuka kujiungia umeme ilikuwa 170,000 na sasa ni elf 27 tu..upewe nini?
Hivi nyie kichwani kuna nini? REA kaleta Magu? aliahidi hilo? zahanati kila kijiji ni kazi ya wizara ya afya na sio mpaka rais atoe ahadi kwenye kampeni.
 
Hiyo millioni 50 imezaa zahanati na umeme wa REA kila kijiji..kumbuka kujiungia umeme ilikuwa 170,000 na sasa ni elf 27 tu..upewe nini?
Huo ni uongo mtupu, walioko barabara kuu ndio wanapata umeme tu, nyumba ya 10 kutoka barabarani ni gharama za kufa mtu.
 
Chadema bhana kwa kujipa matumaini[emoji23][emoji23], ilihali mnajua kabisa hamuwezi kushika kukanyaga ikulu[emoji16].
Kwani CCM nyinyi ndiyo mna leseni ya kwenda ikulu? Wacheni kujidanganya
 
TUSIMWACHE LISU ATUAHIDI YASIYOWEZEKANA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kwenye kampeni za Lisu ana Mambo makubwa mawili anayowaomba watanzania wamchague nayo. Moja ni malalamiko yake ya kupigwa risasi hii Kwake Ni Kama Kete ya kuwaomba watanzania wamuonee huruma aingie Ikulu. Jambo la Pili ni Sera zake anazotakiwa awashawishi nazo watanzania ili wamchague kuwa Rais.

Nilishawahi kusema kuwa hakuna siku nitambeza Lisu kwa kupigwa Kwake Risasi na Wala sintoongea nikimuona analalamika kuwa mwili wake una machuma kila Mahali. Kama watanzania wataamua kumchagua kwa kuwa tu aliwahi kushambuliwa na watu wasiojulikana Hilo nimewaachia. Mimi nitajikita kwenye Sera zake ambazo kwangu ndio kipimo Cha kutoa kura yangu kumchagua Kiongozi katika ngazi zote iwe udiwani, Ubunge, au Urais nitazipima Sera kabla ya kuchagua.

Nimesikikiza Sera za mgombea urais Lisu anayo Mambo makuu matatu anayowaahidi watanzania kubwa kabisa ni kila mtanzania kumiki bima ya Afya, kupunguza Makato ya Wanufaika wa Bodi, kuleta maendeleo ya watu badala ya vitu. Haya ndio anayoyarudia kila Mara anaposhika kipaza sauti Leo tuongele moja kesho tutaongele lingine na leo tuanze na Bima ya Afya kwa kila mtanzania.

BIMA BURE

Nimejaribu ku survey nchi nyingi duniani, Ni nchi ipi yenye uwezo wa kuwapa wananchi wake wote Bima BURE sikuona.

Marekani ilijaribu kupitia Obama Care lakini baada ya Muda mfupi walishindwa na Obama care ikafa. Sababu kubwa Ni gharama za uendeshaji. Kutokana na U.S Census Bureau taifa la Marekeni lina watu milioni 28.1 tu ya wasiokuwa na Bima. Hivyo Obama care ilidhamiria kufanya Coverage ya watu milioni 28 tu kuwalipia huduma za Afya lakini wameshindwa kutokana na gharama zake. Hili ni taifa tajiri kuliko yote duniani limeshindwa kuwalipia watu milioni 28 tu je kwa Tanzania wenye Bima hawafikii milioni kumi je milioni Arobaini iliyobakia wanaofanya kazi wataweza kuwalipia gharama hizo?

Sababu nyingine ya wamarekani kukataa Obama care ni kuwa Kama itafanya kazi Kodi ingelipanda sana nchini marekani hivyo wakaamua kuitupilia mbali. Kuna nchi zinazotajwa kuwa na unafuu wa Bima Duniania lakini sio bure naomba kuzitaja:-

1.Ujerumani.

Ujerumani ndio taifa linaloonekana Kama Bima yake angalau Ina unafuu kwa wananchi wake. Lakini pia sio wajerumani wote ambao Wana Bima ya afya. Wafanyakazi wote nchini ujerumani wanalipia Bima zao kwa kushirikiana na waajiri. Wengine waliobakia wanalipia kiasi kidogo Bima zao.

2. Singapore

Singapore wao Wana mfumo wa Bima unaoitwa Medshield ambao serikali kwa asilimia kubwa ndio inabeba gharama za matibabu lakini kila mtu nchini Singapore anatakiwa alipie asilimia 10 ya kipato chako kwenye mfuko huo. Kama ni Mkulima wanakupigia mahesabu asilimia 10 ya unachokipata ulipie kwenye mfuko wa bima, Kama ni mfanyakazi vivyohivyo pamoja na kuwa unaonekaba kuwa mfumo Bora kuliko yote duniani lakini bado unalipiwa na wenye kipato kikubwa bado wanaumia sana kukatwa asilimia 10 kwa ajili ya Bima.

3. Japani

Japani wao Wana mfumo wa Bima unaoitwa SHIS mfumo huu nao watu wanatakiwa kujiandikisha na kulipia.

4. Uingereza.

Wao ndio kwa asilimia kubwa wamefanikiwa kwa kuwa hospital asilimia kubwa zinamilikiwa na serikali na wafanyakazi wote hulipwa na Serikali. Mfumo wao wa Bima wa NHS gharama zake zote hutolewa na Serikali. Ila bado una changamoto na mtu akitaka kutibiwa private ambako Kuna huduma nzuri na za haraka unatakiwa kulipia mwenyewe.

Hizo Zina unafuu Duniania Soma unafuu wake halafu tulinganishe na Tanzania.

Tanzania.

Tuna Bima ya NHIF ambayo huangaika na watumishi wa Umma na wategemezi wao. Huu tunauchangia asilimia Kama mataifa mengine yanavyouchangia. Tena asilimia tatu tu tofauti na mataifa Mengi sana Duniania.

Tuna mfuko mwingine iCHF (Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ulio Boreshwa), huduma hii ya Bima ni kwa gharama nafuu kabisa kwa Watanzania wote katika Sekta ya Afya kwa Familia ya watu sita yaani Baba, Mama na watoto wanne kwa Tsh. 30,000/- tu kwa mwaka mzima. Una pata huduma zoote za matibabu kuanzia kituo kidogo cha Afya mpaka Hospital ya Mkoa.

Serikali Ina mpango pia wa kuleta Sheria Bungeni ya kuwataka watanzania wote kuingizwa kwenye mfuko wa Bima ya Afya.

Mimi nataka kufahamu Lisu anataka kuifanyaje hiyo Bima yake. Sio kwamba nambeza la hasha nataka kufahamu Bima yake anayoihubiri Ina nini ndani na itakuwa inafanana na ya nchi gani.

Tusimwache Lisu atudanganye Kuna haja ya kuchambua haya yanayoongelewa na wanasiasa. Kesho tutachanbua Sera ya Lisu nyingine.

Hoja yangu CHADEMA naomba muwaeleweshe watanzania hiyo Bima yenu ina package gani?

Ole Mushi
0712702602
Hivi alisema kuwa na bima bure au kuwa na bima ya matibabu kwa kila mwananchi?
 
Back
Top Bottom