Tusio na adui wa kudumu tunasimama na Dkt. Slaa

Tusio na adui wa kudumu tunasimama na Dkt. Slaa

Brazaj, ogopa sana watu wa aina Dr. Slaa, Bashiru, Polepole, Kabudi ......ni watu wasiyo simamia wanachokiamini. Kama ni manahodha wako tayari kutosa chombo na abiria ili wajiokoe wao peke yao wakati wa dhoruba, kama ni makamanda wanaweza kukitosa kikosi ktkt ya mapigano. Wana lugha nzuri lakini hawafai

Ninakazia:

Hatuna rafiki wala adui wa kudumu.

Hata Samia, Majaliwa, Kabudi na wote uliowataja wakinena tunayotaka hatuna taabu nao.

Lissu, Mbowe na wenzao wakighairi, tunawatupia virago.

Kauli yako inafanana na za wale waliotoa mimacho kama mijusi iliyobanwa milangoni.
 
Kwani Mbowe ametamka wapi kumhusu Slaa kama huyo ndugu?

Si tulikubaliana Kila mtu kuubeba mzigo wake? Kulikoni kumbebesha Mbowe mzigo wa huyo bwana?

Kwa mtaji huo wewe unaweza kuwa mburula kuliko huyu!
Tunamtaja Mbowe kwa sababu yeye ndiye mwenyekiti wa Chadema aliyepokea fedha za Lowassa na kumkaribisha agombee uraisi kwa tiketi ya Chadema.

Na hilo likawa chimbuko la Dk Slaa kujiondoa Chadema sababu alitamka wazi kwamba hawezi kutumika kama Dodoki ili kumsafisha Lowassa ambaye alikwisha chafuka toka kwenye list of Shame pale mwembeyanga.

RICHMOND.

Usijitowe ufahamu kwa kuuliza jambo ambalo linajulikana na kila mtanzania.
 
Usimaind bablai 🤣🤣 mi nimeuliza tu swali!!

Siwezi ku mind mjomba. Hata hivyo kwenye ukombozi hatuwezi kuzikubali kauli zenye kutaka kutuletea utengano. Adui yetu tunamjua. Huyo tutalala naye mbele uncompromisingly!
 
Labda mzalendo wa nyumbani kwenu kibaigwa
Taifa na Dunia nzima inalijua hilo na ndio maana walimuachia chap!

Huyu mzee anaheshimika kuliko Hata Lissu na Mbowe.
 
Tunamtaja Mbowe kwa sababu yeye ndiye mwenyekiti wa Chadema aliyepokea fedha za Lowassa na kumkaribisha agombee uraisi kwa tiketi ya Chadema.

Na hilo likawa chimbuko la Dk Slaa kujiondoa Chadema sababu alitamka wazi kwamba hawezi kutumika kama Dodoki ili kumsafisha Lowassa ambaye alikwisha chafuka toka kwenye list of Shame pale mwembeyanga.

RICHMOND.

Usijitowe ufahamu kwa kuuliza jambo ambalo linajulikana na kila mtanzania.

Hamna kitu hapo zaidi ya kuwa unaonekana ni katika ile mijusi mliotoa mimacho kiaina, baada ya kukandamizwa na mlango.
 
Lugha hizi ndizo tunazozielewa:

View attachment 2739972

Hizi ndiyo zile lugha za watu zikiitwa lugha za Mungu. Beberu akiziita:

"Languages of the people."

Hizi humfanya adui macho kumtoka mithili ya mjusi alobanwa na mlango.

Kwamba ni mpigania haki? Mzalendo? Mwenye kukerwa na ghiliba za majizi?

"Ushindwe vipi kumwelewa Dkt. Slaa?"

Kwamba Dkt. Slaa aliwahi kutukosea? So what? Hatuhitaji malaika hapa!

Kwao wote waliowahi kutikosea au ambao hawakuwahi kutukosea: muhimu kwetu ni nini wanafanya au kusema sasa.

"Malaika maisha ya duniani si yao. Hata Messiah hakuja Kwa wenye haki."

Bravo: Dkt. Slaa, Dkt. Nshala, Mwabukusi, Kamanda Mdude na wa namna hiyo.

Mlipo tupo!

Ninakazia:

Dhidi ya ma CCM hatuna rafiki wala adui wa kudumu ila agenda na malengo!
Nakuelewa sana tu, pia hoja zake nazielewa vyema kabisa. Tatizo ni kwamba, wakati wewe unapambana kusimamia maslahi mapana ya nchi, mwenzako anapambania nafasi.
Ni heri usimame mwenyewe, huyo mzee atakuuza.
 
CCM inataka tusimame wenyewe Ili kutudhibiti na huko ndiko kutoa kwao mimacho baada ya kubanwa na mlango. Vipi na wewe ni mwenzao?
 
Naunga mkono hoja 100%.

Nape alitamba 2015 kuwa atakanyaga haki zetu za kuchagua kwa kufunga bao la mkono. Lkn alipoonewa na kutishiwa bastola na jiwe tuliungana naye.

Kwann asiwe Dr. Slaa??
 
Ninakazia:

Hatuna rafiki wala adui wa kudumu.

Hata Samia, Majaliwa, Kabudi na wote uliowataja wakinena tunayotaka hatuna taabu nao.

Lissu, Mbowe na wenzao wakighairi, tunawatupia virago.

Kauli yako inafanana na za wale waliotoa mimacho kama mijusi iliyobanwa milangoni.
Kama huna rafiki wala adui wa kudumu, mubebe huyo Slaa umpeleke nyumbani kwako, sisi huku hatumpendi huyo msaliti. Unalialia humu tukusaidie nn?
 
CCM inataka tusimame wenyewe Ili kutudhibiti na huko ndiko kutoa kwao mimacho baada ya kubanwa na mlango. Vipi na wewe ni mwenzao?
Yeah, mimi ni CCM ingawa siyo mnazi, wala sidhibitiki, nipo huru ila ni CCM.
 
Kama tunasivyokuwa na mpango na wasiokuwa na impact. Kama mi CCM endeleeni kutokwa na mimacho pima. Tunataka matokeo siyo maridhiano.
Kuna mpango unapangwa na system kuanzisha chama kipya bosheni cha upinzani. Na chama hiki kitacheza mdundo wote unaotakiwa na upinzani,, lakini kitakuwa na ajenda za CCM nyuma ya pazia. Zingatia angalizo hili.
 
Rais na sirikali ni Waajiriwa.

Wananchi ndio Waajiri/bosses.

Rais na sirikali yake hawana mamlaka ya kikatiba KUTUPANGIA muda Gani tupate Katiba mpya.

NB; Bila tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya hapatafanyika uchaguzi wowote wa HAKI!!

Tusubiri.
 
Mimi msimamo wangu uko wazi kwa Slaa "anahongeka kirahisi"

Na huenda ametumwa aje aanzishe Movement ya kikanyaboya.

Agenda kubwa kabisa ni KATIBA MPYA sasa yeye amejifanya kukumbuka leo baada ya kuukimbia UKAWA na kuusaliti.
 
Kuna mpango unapangwa na system kuanzisha chama kipya bosheni cha upinzani. Na chama hiki kitacheza mdundo wote unaotakiwa na upinzani,, lakini kitakuwa na ajenda za CCM nyuma ya pazia. Zingatia angalizo hili.
Dr. Slaa ndiye ameandaliwa kwenye hicho Chama, na wanachofanya ni ku test mitambo kwa kwa kumuandalia matamko ya kutoa huku wakijifanya kumsumbuasumbua, lengo lao ni kumpatia airtime ili Chama hicho kiweze kupata muitikio na mapokeo.
Bahati mbaya kila wakipima u0epo wanaona hiyo project yao wanayoifanya na Dr. Slaa inaenda kuishia kuwa another Project of Zitto Kabwe like, yaani itabuma tu.
Hata wenyewe wamreona hasara sababu wameishia kuwa na wapinzani aina ya Dovutwa, Shibuda, Zitto Kabwe, Mbatia, Cheyo n.k. Wanaishia kuwalipa for nothing huku kazi kubwa wakiifanya system wenyewe, na watu zama hizi wakishanusa mtu hafai wanamuacha kama alivyom
 
Nakumbuka Mzee Slaa nilikuwa namwelewa sana kabla hajazunguka ile 2015, nikiri wazi nilimuamini zaidi ya Mbowe, nikadhani kama ni kuondoka Chadema, basi wa kwanza anaweza kuwa Mbowe kisha ndio afuate Dr. Slaa kama hiyo siku ingetokea.

I was wrong, yule niliyemwamini mwanzo ndie akawa wa kwanza kuondoka, niliumia sikutegemea, tena hasa nikikumbuka kipindi alichoondoka, alikuwa ndio anahitajika zaidi, nikamchukia, lakini baadae nikakumbuka kumbe nae Dr. Slaa ni mtu mzima, mwenye maamuzi na msimamo wake usiotakiwa kuingiliwa na yeyote, bila kujali wakati anaouchukua.

Baadae kuondoka kwake badala ya kumchukia, sasa akawa ameniachia funzo,

- La kwanza na muhimu kabisa; niamini taasisi siku zote, nisiendeshwe na mahaba ya kumfuata individual.

- Somo la pili aliloniachia, Tanganyika yangu kwanza, yeyote atakayelinda interest za Tanganyika yangu, sitamuangalia sura, sitaulizia historia yake, sitamkagua chochote kwasababu naamini hata nikifanya hiyo kazi, hayupo malaika kati yetu, hivyo huo muda wa kupoteza sina.

Hivyo, kwangu yeyote anayempuuza Dr. Slaa kwa sasa na kile anachopigania, ni adui wa Tanganyika, adui wa rasilimali za watanganyika, anayepoteza muda kutazama sura na majina ya watu, badala ya kwanza kutazama maslahi ya taifa, mshamba wakuhurumiwa aliyepitwa na wakati anayewaza yaliyopita, mjuaji asiyeamini kwenye maisha kuna kukosea na kusamehewa, huyu hatufai kama ambavyo hatufai yule msaliti aliyetugeuka na kuwakumbatia waarabu bila aibu, wote hao ni wakupiga mawe siku zote.
 
Dr. Slaa ndiye ameandaliwa kwenye hicho Chama, na wanachofanya ni ku test mitambo kwa kwa kumuandalia matamko ya kutoa huku wakijifanya kumsumbuasumbua, lengo lao ni kumpatia airtime ili Chama hicho kiweze kupata muitikio na mapokeo.
Bahati mbaya kila wakipima u0epo wanaona hiyo project yao wanayoifanya na Dr. Slaa inaenda kuishia kuwa another Project of Zitto Kabwe like, yaani itabuma tu.
Hata wenyewe wamreona hasara sababu wameishia kuwa na wapinzani aina ya Dovutwa, Shibuda, Zitto Kabwe, Mbatia, Cheyo n.k. Wanaishia kuwalipa for nothing huku kazi kubwa wakiifanya system wenyewe, na watu zama hizi wakishanusa mtu hafai wanamuacha kama alivyom
Hizi zote ni hisia tu, hazina uthibitisho wowote usioacha shaka, sioni sababu ya kuzibeba vichwani hasa kwa wakati huu.
 
Akikuelewa nistue mkuu. Nimekaa pale!

Watu kama hawa ni mzigo kwenye vyama. Bora wakaungana na kina johnthebaptist Lumumba huko.

Ni Katika wale wajumbe 8.5m+ plus wenye kulaumu watanzania kutotokea barabarani wakati wenyewe wakiwa wamefichama uvunguni.
Slaa hakusimama na wapinzani wakati wa Magufuli huku akiwa na cheo, tena kwa mambo ambayo hakupaswa kuwaumiza, je na yeye alikuwa na uadui wa kudumu? Huyo Mbatia alikubali wazi wazi kutumika na Magufuli wakati wa uchaguzi mkuu wa 2020, watu kama hao hatuwapingi kwa wanachosimamia sasa, lakini ni ujinga kuwaamini watu wanaojali maslahi yao binafsi.
 
Hizi zote ni hisia tu, hazina uthibitisho wowote usioacha shaka, sioni sababu ya kuzibeba vichwani hasa kwa wakati huu.
Kitu chochote kama kinaongelewa lakini bado hakijawa hubaki kuwa hisia, hata kama kuna tulioona lakini tunaamua kukiongea lakini bila kukitolea maelezo or proof, bado kitabaki hisia.
hivyo upo sahihi, mimi pia nipo sahihi. Subiri wakati ukifika itakapojidhihirisha ndipo ufanye maamuzi, wakati mimi sina cha kusubiri sababu nipo mbele ya wakati.
 
Back
Top Bottom