Tusio na magari tukutane hapa

Tusio na magari tukutane hapa

Ngoja nimalizie kujenga ndiyo nitakuja kwenye magari.
Jamani tusikate tamaa ipo siku tutapata magari yetu.

Vyuma vikikaza nasi tunakaza mwendo ili tuendane na speed.
Mwisho tutatusua tu.
Mungu tusaidie
 
Raha na karaha ya ngoma ni kuingia kucheza, Raha na karaha ya ndoa ni kuingia kwenye ndoa...
Ukitaka kujua karaha za kumiliki gari basi miliki gari kwanza. Wenye magari hawawezi kukwambia ukweli wa hizo karaha kwa sababu umiliki wao wa gari ndio umetengeneza status zao kwenye jamii, hivyo watajitahidi kuonyesha kuwa ni watu wenye furaha ili kulinda status. Ni sawa sawa na ndoa. Wanandoa nao wana hiyo tabia.

Ulishawahi kuwaza haya...
1/Motor vehicle insurance.
2/Kodi ya mapato.
3/Bei za Diseal na Petrol.
4/Car Parking fee.
5/Bei za kuoshewa gari.
6/Mafundi Garage.
7/Faini za barabarani.
8/Bei za oil, Filter, Plug.
9/Kuziba pancha.
10/Kusukuma gari.

Miliki gari yako ndio utayajua hayo na utajua gharama zake zikoje na kwa vipi zinaathiri maisha ya mtu ya kila siku.
[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
 
kwa mwanamke kumiliki gari ni gharama vinginevyo yakupasa uwe na
1. mkoba au hand bag ya maana
2. mavazi yalokwenda shule
3. uwe na reserve ya kutosha ya saloon
4. nk
i.e namaanisha kumiliki gari kunataka uwe na hadhi. usikurupuke, vinginevyo kama ww ni mfanyakazi litaishia kutembea mwisho wa mwezi hadi mwisho mwingine wa mwezi. Pia usinunue gari kwa kukurupuka au kwa sababu marafiki zako wanayo, Nunua kwa sababu unaona una ulazima wa kuwa nalo. Hata hivyo haya ni mawazo yangu kwani kila mmoja ana mtizamo wake.
 
Ngoja nimalizie kujenga ndiyo nitakuja kwenye magari.
Jamani tusikate tamaa ipo siku tutapata magari yetu.

Vyuma vikikaza nasi tunakaza mwendo ili tuendane na speed.
Mwisho tutatusua tu.
Mungu tusaidie
Amina [emoji4][emoji4]
 
Back
Top Bottom