Tusiogope au kuona aibu kutumia Kiswahili.

Tusiogope au kuona aibu kutumia Kiswahili.

Tanzania?


  • Total voters
    1
  • Poll closed .

Nelibaba

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2023
Posts
290
Reaction score
386
Hivi kwanini viongozi wetu wa kitaifa wanakionea aibu Kiswahili? Tumeshuhudia viongozi wetu wakienda uko nje na wakati mwingine tukipata wageni kutoka nje kuja Tanzania, viongozi wetu wanakisaliti Kiswahili na kutukuza lugha ya mkoloni! Hii sio sawa na inatuuma sana sisi wazalendo wa Kiswahili!

Eti! jamani, pamoja na teknolojia ya ukalimani iliyopo duniani leo na wakalimani lukuki tulio nao,kwanini tuendekeze lugha za nje katika kuwasilisha hotuba zetu? Kwanini tusiwe huru kuzungumza lugha yetu? Hivi Kwa muktadha huu,tutaweza kujitawala kweli?

Nadhani Kuna faida kuu mbili za viongozi wetu kuchagua kutumia Kiswahili katika majukwaa ya kimataifa;
Mosi, kuendeleza na kukuza Kiswahili ndani na nje ya nchi kutokana na ushawishi walionao. Vilevile, wataonesha utaifa na kwamba Tanzania ni taifa huru lililojengwa katika misingi ya tunu mbali mbali kikiwemo Kiswahili.

Tusiwe wanyonge dhidi ya Kiswahili chetu na tuachane na propaganda za watu na tawala za kimagharibi. Leo niishie hapa, ila nitaandaa Uzi maalum utakaochimba kwa mapana na marefu ya nafasi na umuhimu wa lugha yetu pendwa "Kiswahili" katika uwanda wa kimataifa.
 
" Muda ni mali " kama wote wanao uwezo wa kuzungumza lugha moja kwanini wasizungumze ili kuokoa muda??
 
Back
Top Bottom