Tusiokunywa Pombe Njooni Tuelezane Vinywaji Vya Kuagiza Tukiwa Bar

Tusiokunywa Pombe Njooni Tuelezane Vinywaji Vya Kuagiza Tukiwa Bar

watu msokunywa ni wambea sana heri muwe mnabaki nyumbani, mkitoka muende sehemu za bites mle sambusa na juice
 
Salaaam wakuu.

Mimi sio mlevi wa pombe ila Nina kilevi changu, na kuacha haiwezekani.[emoji14]

Back to topic.

Nmekua mtembeleaji mzuri wa bar ila sasa napata shida linapokuja suala la kuagiza kinywaji hasa ninapokua na marafiki zangu ambao wengi ni wanywaji.

Sasa nmeona haya maji na juice vimekua common kila "out" juice tuuuu. Maji tuuuu. Mpaka najikuta natengwaaa.

Hebu tupeane uzoefu kuna kinywaji ambacho sio kilevi kinaweza kua mbadala wa juice na maji hata kama ni expensive? Achilia hizi common Bavaria...?
Togwa dadeq
 
2018 pombe nimeshaipiga teke kwa upande wangu naiona haina faida kwa sasa japo nateseka sana katika kipindi hichi kifupi lakini najipa moyo nitashinda tu ya ni mwendo wa ceres juice mpaka nifanane nazo
Mi pia mwaka huu naiweka kando
 
Kunywa hata juice za box achana na energy drinks si salama. Zamani nakumbuka kulikuwa na kinywaji kinaitwa Alvaro ilikuwa nzuri sana na flavors tofauti sijui ikapotelea wapi.
 
Mi nakunywa Safari Lager tu hizi pombe mi stumiagi kabisa. Hata soda, juisi sipendi sana mana kuna kisukari, presha low libido etc
 
Mi nakunywa Safari Lager tu hizi pombe mi stumiagi kabisa. Hata soda, juisi sipendi sana mana kuna kisukari, presha low libido etc
mkuu sasa kama unaogopa sukari mbona hizo bia ndo zina sukari nyingi mno tena ile yenyewe natural sugar ambayo wataalamu wanasema ndo inasababisha kisukari fasta,,au hujawai skia kwamba wanywaji wa bia ndo wapo kwenye htr kubwa yakupata kisukari
 
Back
Top Bottom