Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Hoja zako ni nzito na umezunguka sana, lakini tatizo lako kubwa ni hawa watu, Polepole, Mange na Sarungi, na siyo Tanganyika. Huo ni mtazamo wa kiupotoshaji na kumanipulate.
 
Mzee nimekuelewa japo umeiweka kimafumbo..!!
 
This is a clandestine strategy to undermine those figures, be careful Tanzanian
 
Tatizo ni wanaume wa Tanganyika, wote sasa wamekua kama wanaume wa Dar
 
Naam!

Naunga mkono
 
"Magufuli alifanya kosa kudhani watabadilika" amenukuliwa akisema hivyo Polepole
Ukiiba mali za umma ukibadilika unaachiliwa tu uendelee na maisha kama kawaida??
 
Kwa mara ya kwanza nilitaka kumwelewa kidogo MALCOM LUMUMBA na mada yake hii...

But as the discussion goes on, namuona anaanza kujichanganya na kumuona kuwa huyu ni ndani ya serikali hii hii, anaitetea kwa kuuma kidogo na kupuliza...

Mimi nahisi MALCOM LUMUMBA yeye ndiye hakumwelewa TL na pengine hajawahi kumwelewa kabisa...

Ukimsikiliza kwa makini Tundu Lissu utamwelewa haraka kuwa hakuwa na tatizo na Hayati Rais Magufuli ku - deal na mikataba ya rasrimali madini. Tofauti ya TL na JPM ilikuwa ni njia (methods) aliyokuwa anatumia Magufuli...

Na TL alikuwa very clear kuwa, kama kweli tuko serious kunataka kurekebisha mambo haya, kwanza tupitie na kurekebisha sheria zetu kwanza ikiwemo sheria mama (Katiba) na kisha tuziangalie kwa makini sheria za uwekezaji wa kimataifa. Ndipo hapo suala la MIGA na mahakama za kimataifa likaingia. Kwamba tuuangalie upya uanachama wetu ktk baadhi ya mikataba na makubaliano ya kimataifa...

Kama kawaida serikali ya CCM wakati huo chini ya Rais John P. Magufuli ni kiburi na huwa hawataki kusikiliza mawazo toka nje ya wao wenyewe. Lakini kwa ushauri wa TL, Rais Magufuli aliufanyia kazi kidogo kwa mlango wa nyuma na ndio zikaja sheria zile za ulinzi wa rasrimali asili zetu za mwaka 2017/2018 nafikiri...

Tukubali tusikubali, Tundu Lissu kwenye hili, wakati ule hakuwahi kutetea wanamtandao au wawekezaji wa sekta ya madini matapeli....

Na historia ya huyu jamaa (TL) inaonesha wazi kabisa kuwa, tangu miaka ya 1997 wakati kampuni hizi za kigeni za uchimbaji madini yanaingizwa nchini chini ya utawala wa Rais Ben Mkapa na waziri wake wa nishati na madini (by then Jakaya Kikwete), amekuwa akipinga na kukosoa mikataba iliyoingiwa na serikali na namna wanavyoanzisha shughuli zao wakiwaumiza wananchi wa maeneo yao ya asili...

Na kwa sbb hii, ndio maana mpaka leo Tundu Lissu ni adui namba moja wa serikali zote za CCM ingalau toka awamu ya Rais Hayati Ben Mkapa...

Kwa hiyo, kuhusu TL ktk eneo la sekta ya madini na nia yake, mimi naupinga katakata mtazamo wa MALCOM LUMUMBA kuhusu Tundu Lissu...

Ofcoz, Tundu Lissu naye ni mwanadamu na ana udhaifu wake. Lakini kwenye hili, sioni makosa yake. He was damn right. Kama sio egostic behaviour ya serikali ya CCM chini ya Hayati Rais Magufuli, TUNDU LISSU angeweza kuwa included kwenye timu ya wataalam wa kuishauri serikali namna ya kwenda mbele kwenye eneo hili na angekuwa msaada mkubwa...

Lakini bahati mbaya sana, Hayati Rais Magufuli alimwona ni adui na badala akatamani amuue tu.🤔🤔🤔

That was so sad..☹☹
 
Ukiiba mali za umma ukibadilika unaachiliwa tu uendelee na maisha kama kawaida??
Kuna wakati unaweza kusamehe vitu kwa lengo la kupata amani ya kudumu.
Mfano tume ya reconciliation ya SA wakati wa raisi Mandela. Ile ya akina Askofu Tutu.
 
Umesema sahihi kabisa. Nchi hii ingekuwa na watu wenye akili na wanaojitambua vizuri. Lissu ndo angekuwa Think Tank Mkuu kwenye masuala ya Kisheria nchini na ingewezekana angeanza kutumika mapema leo hii nchi hii ingekuwa kama Norway kwa kunufaika na rasilimali zake.

Ni bahati mbaya CCM na washenzi wao kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama wanaendeleza rushwa na kujinufaisha binafsi. Ndo mana hii nchi imefeli karibu kwenye kila kitu.
 
Kiufupi ni rahisi wanamtandao kumtumia Lissu kuliko polepole niulize kwa nini Lissu ni mtu kulipuka pamoja na kua mtu smart but ana mapungufu kama binadamu wengine
 
Kinachosikitisha ni kwamba watu ambao wako tayari kupambania mabadiriko wapo mtandaoni na in fact ni chini ya 10% ya watanzania.
 
Kwa mara ya kwanza nilitaka kumwelewa kidogo MALCOM LUMUMBA na mada yake hii...
Nimemwelewa !hoja anayoisimamia nimeieleza takribani miaka 10 iliyopita, kwamba, lazima tuunde Taasisi zinazojisimamia kwa mujibu wa sheria na si ''one man show'' kama ilivyo sasa hivi.

Taasisi zina matatizo. Ilitegemewa Mahakama kama Taasisi yenye nguvu kisheria na Mhimili wa dola ingekuwa 'independent'' na kimbilio la Wananchi. Je ndivyo ilivyo? Mahakama imekuwa tawi tu la Chama

Taasisi ya TBC ni mali ya Umma , je inatenda haki kama uanzishwaji wake ulivyoandikwa?
Tazama tukio la leo la TCRC kuifungia JF na hoja husika. Mbona picha zinazodaiwa zime 'post' na mhusika,
JF imetenda kosa gani!

Polisi wanasema Uchaguzi ni halali kwa mujibu wa Katiba inayosema ''ufanyike October'' ( Oct haijatajwa Kikatiba).
No reforms no election ni uhalifu. Polisi wamekuwa Mahakama ! Wanasimamia sheria na kutoa hukumu hapo hapo.

NRNE si suala la tafsiri ya Polisi, ni suala la Mahakama baada kufikishiwa malalamiko na mlalamikaji.
Mlalamikaji si ya Kamanda J4 ! Maelezo ya NRNE si hali Mh J4 anayotoa kwa mujibu wa sheria gani!

Unapokuwa na Bunge mfukoni, Mahakama mkononi, media kibindoni hapo unategemea nini!
Mimi nahisi MALCOM LUMUMBA yeye ndiye hakumwelewa TL na pengine hajawahi kumwelewa kabisa...
Maelezo yako kuhusu TAL yameeleweka vizuri. TAL ni mwanasheria si mwanasiasa, inahitaji fikra sana kumwelewa.
Ni ukweli usijulikana. TAL hakumpinga Magufuli binafsi au upoteaji wa rasilimali . Hoja yake ni utaratibu unaotumika.

Kwa mfano, TAL alipinga Magufuli kuitoa Tanzania katika Mahakama za Kimataif akisema tatizo si Mahakama bali sababu zinazopelekea sisi kupelekwa Mahakama hizo. Tunaingia mikataba ya hovyo halafu wawekezaji wakitushtaki tunaona Mahakama za Kimataifa ni mbaya, eti solution ni kesi kuamuliwa Nchini, none sense!

Mfano wa Pili, TAL akiongelea Muungano utamuona ni mkorofi, lakini ukimsikiliza hoja zake utaona matundu mengi ya Muungano! TAL anasema Muungano haupo! akimaanisha upo kwasababu ya Imani tu kisheria kuna matatizo mengi. Tuna Amir Jeshi Mkuu wawili, wa JMT inayohusu Zanzibar na wa SMZ , hii inawezekanaje?

TAL akimaliza kuongea kunatakiwa watu kama akina Lema na Heche watafune hoja zake kwa viwango vya kawaida.

JokaKuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…