Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Walichokifanya kina ​

Kwanza ahsante kuchukua muda wako kuandika uchambuzi ule. Nadhani imetoka kwa subject matter expert, na ambae alikuwemo kwenye mifumo. Hicho kitu tunakihitaji sana na kipo sana uzunguni, wachambuzi wengi kwenye press ni watumishi waliotoka kwenye mfumo, wanakosoa vitu ambavyo wanavyovijua, huku kwetu watumishi wakishamaliza kazi wamemaliza, na wakiongea ni usaliti. Sasa hivi Humphrey Polepole keshapewa fatwa mpaka ukija utawala mwingine kama ukiwa wa tofauti ndo ufute fatwa ya Humphfrey Polepole.

Unasema sheria mpya ya Usalama ya 2023 ilipitishwa sasa kumi na moja jioni. Ilitakiwa ipitishwe saa ngapi ?
 
Haki juzi nimeshangaa dem wang anaulizia link ya polepole nilishangaa sana
 
Haya WAKUU, mimi NIWATAKIENI KILA LA KHERI

===================================================
​
Hatuna la zaidi ya kusema :

Tunakushukuru.

Wabheja

Hongeah

Songera

Haikambe

Avahache

Wakora waitu

Ndaga fijo

Thank you

Merci

Gratias

Gracias

Danke

Grazie

Ευχαριστώ

ありがとう

谢谢

감사합니다

شكراً

Спасибо
 
Tuunde mkoa mmoja tuuite Tanganyika ili kuhifadh jina la asili la nchi yetu:
Au wilaya
Au kata
Au kijiji
Au hata mtaa:
 
Bandiko zuri ila kihalisia linawabeba watawala.
Salungi, Mange, Polepole unadai wanamakosa huko nyuma kwamaana hiyo hawana haki ya kukosoa chochote unadhani upo sahihi?
Mbona hao unaodhani hawana makosa huko nyuma wapo kimya kipindi hiki ambapo katiba na utawala bora vikizidi kufinyangwa? Bila hao kina salungi, Mage na Polepole nk. Unadhani hali ingekuwaje?
Umedai tatizo la watanzania hatufuati kanuni na uwajibikaji. Ni nani mwenye mamlaka yakuwafanya watanzania wafuate kanuni na kuwa wawajibikaji? Au haya mambo yanatoka mbinguni?
 
MALCOM LUMUMBA Lord Denning ahsante kwa mjadala mzuri. Baada ya muda nimeingia na kusoma kitu.
Hata kama sikubaliani na baadhi ya hoja zenu, nakubaliana na ujenzi wenu wa hoja na kina cha mjadala

Nimefurahi , nililolieleza takribani miaka 10 hapa JF linaongelewa kwa ukubwa, yaani tatizo la Taasisi na mifumo yake.

Katika hili namlaumu Mwl. Nyerere kwa kuamini kwamba uzalendo na maadili waliokuwa nayo yangeheshimiwa na kuwa utamaduni. Mwalimu akatujengea mifumo na Taasisi zinazotegemea uadilifu badala ya kanuni, taratibu na sheria. Mwl alidhani Vijana wake na Wajukuu watakuwa kama yeye na wenzake. Mwl akatuachia;

1. Katiba ya Nchi isiyoweza kujitetea kwasababu haina mifumo inayoitetea kama Mahakama
2. Taasisi zinazotegemea Mtu au Watu badala ya Taasisi zinazojiendesha kwa sheria , kanuni na taratibu zake.

Niliwahi kutoa mfano wa Nchi ya India iliyokaa miezi 3 bila Waziri Mkuu kwasababu hakuna aliekuwa na majority.
UK (Uingereza) ilikaa wiki 3 bila Waziri Mkuu, hakuna aliyeweza kuunda serikali.

India na UK hazikutetereka mifumo ya Ulinzi, Usalama, Uchumi na siasa ilikuwa chini ya Taasisi, nchi haitegemei mtu.

Magufuli altusaidia kujua panapovuja. JK alianza kuvuruga Taasisi kimya kimya, pigo la mwisho lilikuwa la Magufuli.

Hizo Task force , kudhalilisha Mahakama,kuingiza vyombo vya ulinzi na usalama katika siasa, kuzifanya Taasisi ni mali ilianzia kwa JK kisha Magufuli. Tangu hapo Taasisi hazijasimama tena.

Hata Taasisi kama Jeshi hazijachwa salama , Mzee Warioba alithibitisha.

Tatizo letu si Taasisi moja moja ni jumla ya Taasisi zetu. Tunapaswa kuwa na mfumo unatengeneza Taasisi (Institutions) zinazojitegemea na zinazosimama kwa masilahi ya Nchi na si mtu wala Watu.

Taasisi haziwezi kufanikiwa isipokuwa kwa kufanya mageuzi yafuatayo
1. Kutengeneza sheria zinazolinda Taasisi- KATIBA
2. Kuwapa Wananchi nguvu ya kumiliki Taasisi (BUNGE)
3. Kulinda Wananchi na sheria za Nchi- MAHAKAMA

Haya yakifanikiwa mengine yatafuata mtawalia

JokaKuu
 
Kwa maneno mengine Gwajima yuko sahihi lakini kwa kusema hivyo kanisa lake limefungwa
 
Basi Polepole yuko mbele ya wakati mkuu.

Unganisha sauti yake na yako na zetu ili tuijenge Tanzania mpya.
 
Asante sana, Mkuu, kwa kunielewa na kutoa mapendekezo muhimu ya kutafuta muafaka. Hoja zako hapa ni za msingi sana. Hii model uliyopendekeza Ina mashiko kama local government za Sasa haziwajibiki ipasavyo kwa wananchi.
Nitarudi kama nitagundua hii model uliyopendekeza inaweza kuwa na tatizo huko mbele, ili kwa pamoja tujadili namna ya kutatua tatizo hilo.
 
Huyu malcom anajifanya jasusi uchwara mwenye nia njema ya "kuikomboa" Tanganyika lakini nimegundua ana malengo fiche ambayo yako mbali sana na kuikomboa Tanganyika.

Hili ni boksi. Garasa.
 
Pointi kubwa kwa sasa ni namba 2 hapo juu.

Hata kwa katiba hii, wananchi wangejitambua hakika mambo yangekuwa tofauti.

Katiba ya JMT: Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote.

Hilo unalielewaje mkuu?
 
Malcom wewe ni msomi mzuri ila una matatizo mawili...

Unafiki...

Kutumika...
Sana. Analeta mastori yake ya kijinga ya kutulaghai kumbe ana malengo tofauti kabisa.

Huyu utakuta ndio mtumishi mwandamizi wa wahuni.

Perechepereche mingi kujifanya anataka kutukomboa kumbe anatema sumu kimkakati.

Anaandika ukweli nusu nusu, anachanganya na uongo kidogo, anashambulia watu muhimu, anawavuruga, anajifanya ana uchungu, anapandikiza wasiwasi, mashaka, na kuyagawanya makundi ya wafuasi wa wanaharakati.

We utaikomboa Tanganyika wapi bwana, hebu atupishe huko.

Kuikomboa Tanganyika mchezo! Kwa maneno na janja janja!? Ah Thubutu!

ilienda ikashuka, mwalimu nyerere, Tanu, mzena, sambusa, maharage chapati na chachandu!!!
 
Umewahi kutumikia jeshi kama Commissioned Officer ???

Bila kuwa Commissioned Officer hata nikikupa mifano lukuki huwezi kuelewa.
​
Huyo ni close minded , amefungwa na uchawa hivyo ni ngumu kuelewana yeye anachojua ni kupiga mapambio ya SAMIA na CCM , hana kingine anachokifahamu utqjichosha bure hata kumjibu
 
Unasema sheria mpya ya Usalama ya 2023 ilipitishwa sasa kumi na moja jioni. Ilitakiwa ipitishwe saa ngapi ?
Saa tatu asubuhi mkuu.

Maana yake ipate muda wa kutosha kabisa kujadiliwa faida na hasara zake, bila kusahau sababu za msingi za kuwepo kwake licha ya kumulikwa huko zamani.
 
Lissu sioni akiungana na Polepole kwa sababu wanaamini katika vitu tofauti. CCM imara = Nchi imara Vs Bila CCM = nchi imara.
Hapo wote wako sahihi kabisa mkuu.

HP anadai kama CCM haiko tayari kubadilika, basi inapaswa kusambaratika kabisa.

Hukumsikia?

Mabadiliko anayozungumzia kimsingi hayana tofauti na haya tunayotaka sasa.

Juzi alisema kila kipisi na kila punje ya jambo lolote baya vitunzwe na viongozi husika ili vije kutumika kuwawajibisha wabadhirifu siku ya siku - bila kujali vyeo vyao.

Unaelewa maana yake?

Hiyo haina tofauti na kudai katiba mpya!

Unadhani kwa nn Polepole anawakubali sana wazee kama Warioba?

Kwa sababu ya rasimu ya katiba mpya ya Warioba.

Hivi umegundua hata tukipata katiba mpya, uwepo wa vyama ni halali?

Kuna ubaya gani HP akitetea nchi (katiba mpya) huku akipigania mabadiliko muhimu ndani ya chama chake?

By the way, anavyoisema CCM ni kwamba yenyewe pia imetekwa kama tu nchi ilivyotekwa.

Kama nimemwelewa, nchi ikinasuka kwa hao jamaa basi na chama nacho kitakuwa kimekombolewa kwenye makucha yao.

Kitakuwa kwenye haki sawa na vyama vingine katika harakati za kushika dola katika Tanzania mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…