Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Amani iwe nanyi

Kama kichwa cha uzi kinavyosema, Kama Mtanzania ninayeipenda nchi yangu, ninayejali maendeleo ya Watanzania wote vizazi na vizazi, leo nasema kwa Sauti moja, Kama tunajali maendeleo ya Tanzania yetu, Ni lazima wamasai waondoke Ngorongoro ili lile eneo liendelee kuwa na wanyama wengi na kuvutia watalii ambao ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa Taifa letu

Kwa nini nasema haya?

1. Ngorongoro ni moja ya sehemu chache hapa Tanzania ambazo mtalii ana uhakika wa kuona wanyama walio kwenye hatari ya kupotea Duniani yaani Tembo, Faru, Simba, Nyati na Chui.

Nimefika ngorongoro kusema ukweli hadi Tour guides wanakwambia hivi karibuni imekuwa ngumu sana kuwaona baadhi ya hawa wanyama na sio tu hawa bali hata wanyama wengine ambao huko mwanzoni walikuwa ni wengi na wanaonekana kirahisi na kuvutia watalii wengi na kuongeza mapato mf pundamilia, pofu na wengineo. Hii ni kwa sababu wanadamu wameongezeka sana Ngorongoro na asili ya wanyama pori ni kuwa hawapendi kuchangamana na binadamu na shughuli za kibinadamu zikizidi huwa wanahama.

2. Kuna taarifa za uhakika kuwa Wanyama wanaohama Tanzania wanahamia upande wa pili yaani Kenya hivyo Kenya anafaidika kwa kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu Ngorongoro ambazo zinahamishia wanyama wetu Kenya. Hii ni hatari sana kwa uchumi wa Tanzania kwa sababu siku si nyingi, Watalii hawataona umuhimu wa kuja Ngorongoro na hivyo kwenda Kenya na kufanya nchi yetu kukosa Mapato.

3. Kuna taarifa za uhakika pia kuwa Wamasai waishio Ngorongoro hawana hata makabuli. Hivyo ikitokea mmasai amefariki anaachwa aliwe na fisi na mbweha. kibinadamu hii si sawa.

Napenda kumaliza kwa kusema imefika wakati sasa kwa maslahi mapana ya Tanzania, Wamasai wahamishwe Ngorongoro. Eneo hili ni nyeti na Tanzania nzima tunalitegemea kimapato. Likiangamia, Tanzania imeangamia. Ni wakati sasa Fedha zinazotengwa kuwalisha wamasai takribani bilioni 3-4 kwa mwaka zielekezwe sasa kuwajengea makazi ya kudumu wamasai hawa eneo jingine na kuwapatia teknolojia ya kufuga wanyama wachache tena kibiashara na kuachana na Maisha yale ya kijima

Naomba kuwasilisha!
Kwann iwe sasa? Masai wapo miaka na miaka why now? Hizo effects za uwepo wao ulizoainisha hapa nadhan mpaka sasa ngorongoro ingekua imebaki na ng' ombe za Masai pekee!!
 
Mleta mada umeshiba maharage.....watalii africa siyo endelevu.....hao wanao kuja kuja humu wanakuja kuangalia mali zao za kale walixoacha babu yao mkoloni.....sasa wanataka kuchimba kwa kisingizio cha kuondoa masai.
Sawa wanyama wataenda kenya mwafrica mwenzako.jirani yako mbantu mweusi tii akila hizo hela za utalii unaumia nini?...mahali ambapo ukienda mnafanana rangi na mjisura huo!!!
Unafurahia muarabu akibeba twiga kunako midege kupeleka uarabuni??? Unafurahia km juha ila mweusi akikaa asiyekula una muona nuksi Km hujarogwa sijui....
 
Huna akili wewe! Hela anazolipa mtalii akiingia Kenya zitanunua madawa kwa ajiri yako na bibi yako mliopo hapa Tanzania?
 
Yaani ujute milele kwa masai kukaa ngorongoro kwenye makazi yao, badala ya kujuta milele kwa kufanya dhambi ambazo zinaweza kukupeleka jehanamu!?

Kwa hiyo unamaanisha tunaweza jikuta tumeingia jehanamu kwa masai kuendelea kukaa ngorongoro? au sijapata logic yako unaposema tutajuta milele.........
Umeishia darasa la ngapi?
 
Machinga wamehama mjini ya wapi labda?

Mbona wanatembeza biashara zao kama kawaida bwashee.

Halafu nani kakudanganya Tanzania kuna wasomi?

Au hizo PhD za Jaffo na Biteku?

Tanzania watu wanahudhuria tu shule kama unabisha angalia Kibatala anavyowageuza kama chapati.

Uwe na siku njema na uwapendao meku!
Wanatembeza hawajaweka vibanda. Ilibaki kidogo wangejenga vibanda katikati ya barabara. Kuna issues zinataka majibu baada ya kufikiria. Sio majibu rahisi yenye kutaka umaarufu wa kisiasa.
Tanzania ina wasomi...ila sio wenye hizo Phd. Na ile nyingine ambayo nayo sijui kama ilikuwa Phd
 
Wamachinga hawajawahi kujenga vibanda bwashee!
 
Kuna jambo haliko sawa ktk hili suala,na kuna siku litakuwa wazi
Simple and Clear- Kenya anataka kuua Ngorongoro kwa kufund watu watetee wamasai waendelee kuwepo Ngorongoro ili baadae Ngorongoro ife , ifuatie Serengeti na watalii wote waende Masai Mara ambapo Wanyama wote watakuwa wamehamia huko
 
Mbona watu wanaongezeka kila mahali? Je wote watahamishiwa wapi?
Isije kuwa Norongoro imeshauzwa halafu sis tunapiga chapuo tu!
 
Simple and Clear- Kenya anataka kuua Ngorongoro kwa kufund watu watetee wamasai waendelee kuwepo Ngorongoro ili baadae Ngorongoro ife , ifuatie Serengeti na watalii wote waende Masai Mara ambapo Wanyama wote watakuwa wamehamia huko
Pamoja na hayo Tz pia Kuna watu wanamaslahi fulani SI bure
 
Amani iwe nanyi

Kama kichwa cha uzi kinavyosema, Kama Mtanzania ninayeipenda nchi yangu, ninayejali maendeleo ya Watanzania wote vizazi na vizazi, leo nasema kwa Sauti moja, Kama tunajali maendeleo ya Tanzania yetu, Ni lazima wamasai waondoke Ngorongoro ili lile eneo liendelee kuwa na wanyama wengi na kuvutia watalii ambao ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa Taifa letu

Kwa nini nasema haya?

1. Ngorongoro ni moja ya sehemu chache hapa Tanzania ambazo mtalii ana uhakika wa kuona wanyama walio kwenye hatari ya kupotea Duniani yaani Tembo, Faru, Simba, Nyati na Chui.

Nimefika ngorongoro kusema ukweli hadi Tour guides wanakwambia hivi karibuni imekuwa ngumu sana kuwaona baadhi ya hawa wanyama na sio tu hawa bali hata wanyama wengine ambao huko mwanzoni walikuwa ni wengi na wanaonekana kirahisi na kuvutia watalii wengi na kuongeza mapato mf pundamilia, pofu na wengineo. Hii ni kwa sababu wanadamu wameongezeka sana Ngorongoro na asili ya wanyama pori ni kuwa hawapendi kuchangamana na binadamu na shughuli za kibinadamu zikizidi huwa wanahama.

2. Kuna taarifa za uhakika kuwa Wanyama wanaohama Tanzania wanahamia upande wa pili yaani Kenya hivyo Kenya anafaidika kwa kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu Ngorongoro ambazo zinahamishia wanyama wetu Kenya. Hii ni hatari sana kwa uchumi wa Tanzania kwa sababu siku si nyingi, Watalii hawataona umuhimu wa kuja Ngorongoro na hivyo kwenda Kenya na kufanya nchi yetu kukosa Mapato.

3. Kuna taarifa za uhakika pia kuwa Wamasai waishio Ngorongoro hawana hata makabuli. Hivyo ikitokea mmasai amefariki anaachwa aliwe na fisi na mbweha. kibinadamu hii si sawa.

Napenda kumaliza kwa kusema imefika wakati sasa kwa maslahi mapana ya Tanzania, Wamasai wahamishwe Ngorongoro. Eneo hili ni nyeti na Tanzania nzima tunalitegemea kimapato. Likiangamia, Tanzania imeangamia. Ni wakati sasa Fedha zinazotengwa kuwalisha wamasai takribani bilioni 3-4 kwa mwaka zielekezwe sasa kuwajengea makazi ya kudumu wamasai hawa eneo jingine na kuwapatia teknolojia ya kufuga wanyama wachache tena kibiashara na kuachana na Maisha yale ya kijima

Naomba kuwasilisha!
Ukiniambia Wazanzibari wote wahamishwe Zanzibar ili kisiwa chote kiwe eneo la utalii, nitakubaliana na hoja yako.
 
kama kisiwa cha Zanzibar kingekuwa na wanyama ambao wangekuwa wanatoweka kulingana na kuongezeka kwa shughuli za binadamu basi tungesema binadamu wahamishwe

Ukiniambia Wazanzibari wote wahamishwe Zanzibar ili kisiwa chote kiwe eneo la utalii, nitakubaliana na hoja yako.
 
Mwenye maslahi ni Kenya anayetaka Ngorongoro ife ili watalii wasije Tanzania wahamie Kenya ambako wanyama wanakimbilia kutokana na kuongezeka kwa shughuli za binadamu Ngorongoro. Ngorongoro ikifa mapato yote ya utalii yanahamia Kenya
Pamoja na hayo Tz pia Kuna watu wanamaslahi fulani SI bure
 
Kwanini hamtaki kukaa meza ya majadiliano? Hamna hoja za maana zaidi ya kutekeleza mnayoambiwa na masponsor wenu.
Ingekuwa mnakuja na ushahidi kwamba Wamaasai wanaua wanyama au wanakata miti au wanalima kinyume na makubaliano. Sasa hamna lolote nduo maana mmeona muwadhalilishe kupitia media za Wapumbavu.
Wamaasai hawali nyamapori hovyo hovyo, ni aibu pia kuwinda. Kuwinda kwa mmasai tunaona ni laana.
Bahati mbaya hutaki kulisha chakula ubongo wako kujua kabila gani liliwahi kuamishwa toka hifadhini kupelekwa eneo lingine.

Ila kwa sababu tecknolojia imekuwa kwa kasi kwenye umri wenu ndiposa mnaona maasai wanaonewa although kuna Watanzania wengine huko nyuma waliwahi kuamishwa na HAKUKUWEPO kelele kama hizi.

Hata hao unaopigia kelele hawakuwepo pale bali walihamishiwa pale, don't ask you're self but give brain work!.
 
Amani iwe nanyi

Kama kichwa cha uzi kinavyosema, Kama Mtanzania ninayeipenda nchi yangu, ninayejali maendeleo ya Watanzania wote vizazi na vizazi, leo nasema kwa Sauti moja, Kama tunajali maendeleo ya Tanzania yetu, Ni lazima wamasai waondoke Ngorongoro ili lile eneo liendelee kuwa na wanyama wengi na kuvutia watalii ambao ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa Taifa letu

Kwa nini nasema haya?

1. Ngorongoro ni moja ya sehemu chache hapa Tanzania ambazo mtalii ana uhakika wa kuona wanyama walio kwenye hatari ya kupotea Duniani yaani Tembo, Faru, Simba, Nyati na Chui.

Nimefika ngorongoro kusema ukweli hadi Tour guides wanakwambia hivi karibuni imekuwa ngumu sana kuwaona baadhi ya hawa wanyama na sio tu hawa bali hata wanyama wengine ambao huko mwanzoni walikuwa ni wengi na wanaonekana kirahisi na kuvutia watalii wengi na kuongeza mapato mf pundamilia, pofu na wengineo. Hii ni kwa sababu wanadamu wameongezeka sana Ngorongoro na asili ya wanyama pori ni kuwa hawapendi kuchangamana na binadamu na shughuli za kibinadamu zikizidi huwa wanahama.

2. Kuna taarifa za uhakika kuwa Wanyama wanaohama Tanzania wanahamia upande wa pili yaani Kenya hivyo Kenya anafaidika kwa kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu Ngorongoro ambazo zinahamishia wanyama wetu Kenya. Hii ni hatari sana kwa uchumi wa Tanzania kwa sababu siku si nyingi, Watalii hawataona umuhimu wa kuja Ngorongoro na hivyo kwenda Kenya na kufanya nchi yetu kukosa Mapato.

3. Kuna taarifa za uhakika pia kuwa Wamasai waishio Ngorongoro hawana hata makabuli. Hivyo ikitokea mmasai amefariki anaachwa aliwe na fisi na mbweha. kibinadamu hii si sawa.

Napenda kumaliza kwa kusema imefika wakati sasa kwa maslahi mapana ya Tanzania, Wamasai wahamishwe Ngorongoro. Eneo hili ni nyeti na Tanzania nzima tunalitegemea kimapato. Likiangamia, Tanzania imeangamia. Ni wakati sasa Fedha zinazotengwa kuwalisha wamasai takribani bilioni 3-4 kwa mwaka zielekezwe sasa kuwajengea makazi ya kudumu wamasai hawa eneo jingine na kuwapatia teknolojia ya kufuga wanyama wachache tena kibiashara na kuachana na Maisha yale ya kijima

Naomba kuwasilisha!

Wenzako wengine wanasema wamasai waondoke sababu wanaliwa na simba, we unasema simba wanakimbia,nadhani mnge jiorganizes kwanza ili muwe na kauli moja.
 
Back
Top Bottom