Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Amani iwe nanyi

Kama kichwa cha uzi kinavyosema, Kama Mtanzania ninayeipenda nchi yangu, ninayejali maendeleo ya Watanzania wote vizazi na vizazi, leo nasema kwa Sauti moja, Kama tunajali maendeleo ya Tanzania yetu, Ni lazima wamasai waondoke Ngorongoro ili lile eneo liendelee kuwa na wanyama wengi na kuvutia watalii ambao ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa Taifa letu

Kwa nini nasema haya?

1. Ngorongoro ni moja ya sehemu chache hapa Tanzania ambazo mtalii ana uhakika wa kuona wanyama walio kwenye hatari ya kupotea Duniani yaani Tembo, Faru, Simba, Nyati na Chui.

Nimefika ngorongoro kusema ukweli hadi Tour guides wanakwambia hivi karibuni imekuwa ngumu sana kuwaona baadhi ya hawa wanyama na sio tu hawa bali hata wanyama wengine ambao huko mwanzoni walikuwa ni wengi na wanaonekana kirahisi na kuvutia watalii wengi na kuongeza mapato mf pundamilia, pofu na wengineo. Hii ni kwa sababu wanadamu wameongezeka sana Ngorongoro na asili ya wanyama pori ni kuwa hawapendi kuchangamana na binadamu na shughuli za kibinadamu zikizidi huwa wanahama.

2. Kuna taarifa za uhakika kuwa Wanyama wanaohama Tanzania wanahamia upande wa pili yaani Kenya hivyo Kenya anafaidika kwa kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu Ngorongoro ambazo zinahamishia wanyama wetu Kenya. Hii ni hatari sana kwa uchumi wa Tanzania kwa sababu siku si nyingi, Watalii hawataona umuhimu wa kuja Ngorongoro na hivyo kwenda Kenya na kufanya nchi yetu kukosa Mapato.

3. Kuna taarifa za uhakika pia kuwa Wamasai waishio Ngorongoro hawana hata makabuli. Hivyo ikitokea mmasai amefariki anaachwa aliwe na fisi na mbweha. kibinadamu hii si sawa.

Napenda kumaliza kwa kusema imefika wakati sasa kwa maslahi mapana ya Tanzania, Wamasai wahamishwe Ngorongoro. Eneo hili ni nyeti na Tanzania nzima tunalitegemea kimapato. Likiangamia, Tanzania imeangamia. Ni wakati sasa Fedha zinazotengwa kuwalisha wamasai takribani bilioni 3-4 kwa mwaka zielekezwe sasa kuwajengea makazi ya kudumu wamasai hawa eneo jingine na kuwapatia teknolojia ya kufuga wanyama wachache tena kibiashara na kuachana na Maisha yale ya kijima

Naomba kuwasilisha!
Mnapenda kufanya sasa kwa sababu mmeshamuona Mhe. Samia Suluhu Hassan kama uchochoro kupitisha ajenda zenu zilizofeli katika tawala zilizopita.
 
ajenda ipi ilifeli awamu iliyopita wakati huu mchakato umeanza awamu ya tano?
 
Wamasai ni watu wapuuzi sana yaani fikiria unatelekeza maiti ya baba yako porini iliwe na fisi
Hili jambo ni vita vya nchi mbili kiuchumi. Kenya anawatumia wamasai hawa kuharibu ekolojia ya wanyama upande wa Tanzania ili wanyama wahamie Kenya na Watalii wasije tena Tanzania. Wanyama wakiondoka Tanzania basi ndo kifo cha sekta ya Utalii Tanzania ambayo kwa miaka mingi ndo imekuwa ikichangia zaidi kwenye pato la Taifa
 
Hata tukisema tuzuie wahamiaji,hatuwezi zuia watu kuzaliana hasa kwenye jamii zetu za kiafrika.
Futa Ngorongoro kama eneo maalum. Acha watu waishi. Kwanini wanyama wanapewa kipaumbele kuliko binadamu? Mna ajenda zenu za kuondoa baffer iliyowekwa na wamaasai pale. Mnataka kumaliza wanyama wetu.
 
Utakuwa umechanganyikiwa wewe! Serikali imalize wanyama Ngorongoro? Watu tunazungumzia wanyama kulindwa ili utalii uwepo wewe unazungumzia wanyama kumalizwa! utakuwa umewehuka wewe
 
Umewahi kusikia Tibetan Sky Burials?

Hawa ndugu zao wakifa huwa wanakatakata maiti na kuwapa Tai (vultures)
Tena wanakata na kuwagia ndege kama wewe unavyompa mbwa nyama

Kila watu na njia zao za kuwaaga wapendwa wao
Waacheni hata waweke juu ya miti
 
Nimefika ngorongoro kusema ukweli hadi Tour guides wanakwambia hivi karibuni imekuwa ngumu sana kuwaona baadhi ya hawa wanyama na sio tu hawa bali hata wanyama wengine ambao huko mwanzoni walikuwa ni wengi na wanaonekana kirahisi na kuvutia watalii wengi na kuongeza mapato mf pundamilia, pofu na wengineo. Hii ni kwa sababu wanadamu wameongezeka sana Ngorongoro na asili ya wanyama pori ni kuwa hawapendi kuchangamana na binadamu na shughuli za kibinadamu zikizidi huwa wanahama.
Hilo tu! Si mtengeneze zoo, hao wanyama wanaopotea ili watalii wawaone kwa urahisi? Yaaani ebu nishawishi kwa hoja nyingine. Mimi hii haijanikaa. Aah kumbe umeorodhesha hoja nyingine, ngoja niendelee kuzisoma.
 
3. Kuna taarifa za uhakika pia kuwa Wamasai waishio Ngorongoro hawana hata makabuli. Hivyo ikitokea mmasai amefariki anaachwa aliwe na fisi na mbweha. kibinadamu hii si sawa.
Wafundisheni namna ya kuwastiri wenzao wanaofariki.
 
Amani iwe nanyi

Kama kichwa cha uzi kinavyosema, Kama Mtanzania ninayeipenda nchi yangu, ninayejali maendeleo ya Watanzania wote vizazi na vizazi, leo nasema kwa Sauti moja, Kama tunajali maendeleo ya Tanzania yetu, Ni lazima wamasai waondoke Ngorongoro ili lile eneo liendelee kuwa na wanyama wengi na kuvutia watalii ambao ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa Taifa letu

Kwa nini nasema haya?

1. Ngorongoro ni moja ya sehemu chache hapa Tanzania ambazo mtalii ana uhakika wa kuona wanyama walio kwenye hatari ya kupotea Duniani yaani Tembo, Faru, Simba, Nyati na Chui.

Nimefika ngorongoro kusema ukweli hadi Tour guides wanakwambia hivi karibuni imekuwa ngumu sana kuwaona baadhi ya hawa wanyama na sio tu hawa bali hata wanyama wengine ambao huko mwanzoni walikuwa ni wengi na wanaonekana kirahisi na kuvutia watalii wengi na kuongeza mapato mf pundamilia, pofu na wengineo. Hii ni kwa sababu wanadamu wameongezeka sana Ngorongoro na asili ya wanyama pori ni kuwa hawapendi kuchangamana na binadamu na shughuli za kibinadamu zikizidi huwa wanahama.

2. Kuna taarifa za uhakika kuwa Wanyama wanaohama Tanzania wanahamia upande wa pili yaani Kenya hivyo Kenya anafaidika kwa kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu Ngorongoro ambazo zinahamishia wanyama wetu Kenya. Hii ni hatari sana kwa uchumi wa Tanzania kwa sababu siku si nyingi, Watalii hawataona umuhimu wa kuja Ngorongoro na hivyo kwenda Kenya na kufanya nchi yetu kukosa Mapato.

3. Kuna taarifa za uhakika pia kuwa Wamasai waishio Ngorongoro hawana hata makabuli. Hivyo ikitokea mmasai amefariki anaachwa aliwe na fisi na mbweha. kibinadamu hii si sawa.

Napenda kumaliza kwa kusema imefika wakati sasa kwa maslahi mapana ya Tanzania, Wamasai wahamishwe Ngorongoro. Eneo hili ni nyeti na Tanzania nzima tunalitegemea kimapato. Likiangamia, Tanzania imeangamia. Ni wakati sasa Fedha zinazotengwa kuwalisha wamasai takribani bilioni 3-4 kwa mwaka zielekezwe sasa kuwajengea makazi ya kudumu wamasai hawa eneo jingine na kuwapatia teknolojia ya kufuga wanyama wachache tena kibiashara na kuachana na Maisha yale ya kijima

Naomba kuwasilisha!
Mpuuuzi ww
 
Back
Top Bottom