cc: jokate, nikiwapili
Jiulize kwanini hata wazazi wengi wanaofanya biashara wanapeleka watoto kusoma na kuwaambia wasome ili wapate ajira?? kwanini wasiwaambie wasome ili wafanye biashara ?? hapa sizungumzii wafanya biashara wakubwa kama kina bakhresa, nazungumzia wafanya biashara kwa mfano wenye maduka ambayo faida kwa siku unakuta ni chini ya elf 20, hapo anampigania mwanae aje kupata ajira ili aweze kupata mshahara wake wa milion au zaidi na asiteseke kuuza duka kila siku .
Biashara ni nzuri ikiwa na mikakati ya kuipanua, Mfano kwa watu kama wakinga tunajionea kwa macho yetu ni next level, , pale mtu unaona live bila chenga jinsi biashara ilivyo tamu kuzidi ajira , Lakini kama huna mikakati ya kupanua biashara yako, hapo ni sawa na kukamua chungwa kavu yani unalikamua sana lakini juisi ni ndogo sana (the squeeze aint worth the juice)
Natoa mfano kwa Marekani, Siku hizi wanaijeria ndio kundi linaoongoza kwa kuelimika kwa watu weusi, kwa sasa wanaajiriwa sana kwenye makampuni, serikalini, vyeo vizito, n.k Wale wamarekani weusi ambao walikuwa wanaona ajira ni utumwa ndio leo hii wanapiga kelele sana kwamba wanaibiwa ajira na hii yote ni sababu wanavyoona wanaijeria wanapiga mishahara safi, wana madaraka kwenye system, n.k.
Tatizo wengi wanapofikiria kujiajiri mawazo yao yanaenda moja kwa moja kwa wafanya biashara matajiri na kujiwekea bench ark hapo.
Kiukweli kujiajiri hapa Tanzania hakuna nafuu endapo utakuwa unapata kipato chini ya au kinacholingana na mtu alieajiriwa.
Tunaanza na swala la mahudhurio, Mtu alieajiriwa, anaweza akawa haendi kazi jumamosi na jumapili, hizo ni siku 104 kwa mwaka, tukiongezea na likizo ya mwezi hapo ni siku 134, tukiongezea na zile public holidays hapo ni siku kama 150. Kwa upande wa Mtu aliejiajieri hapo inakuwa taabu, wengi hasa wenye maduka hufungua kila siku, ama kwa mbali watapumzika jumapili tu, hakunapublic holidays wala kujipa likizo, N bampa to bampa.
Ajira ni kipato cha uhakika na kadri miaka inavyoenda kuna mishahara kupanda, promotions, n.k mtu anaweza kuingia kwenye ajira akiwa na 25, hapo atapata kipato chake cha uhakika mpaka akiwa na 60 nila misuko suko, Kimbembe kinakuja kwa aliejiajiri hapo, Yaani akiibiwa mzigo, akipata kesi, akifungwa, n.k hapo kupata mtaji upya inakuwa ni shughuli na inaweza kubadili maisha yake kabisa.
Kazni ni kuzea kazi tu, kazi nyingi hazina ugumu, ndio maana hata waliofoji vyeti wanapiga kazi fresh tu, Njoo kwene biashara sasa uone kam unaweza kufoji
Kiufupi Biashara ni nzuri lakini kama kipato ni chini kuliko alieajiriwa au kipo sawa, yule mwenye biashara atahangaika sana.
ntaendelea.....