Tusipotoshane, ajira ina nafuu na uhakika zaidi kuliko kujiajiri

Acha masihara kaka,6M ni hela ya kawaida sana kwenye biz,usiikuze kiasi hicho man,fungua macho utafute fursa utaziona zinazoweza kulipa kiasi hicho
6 M sio pesa ya kawaida mkuu, ni ndogo kwa kuongelea hapa jf ambako wengi wanaandikaga wanakaa masaki

Watu kibao waningia dukani saa 12 wanatoka saa nne faida ni elf 30.

Hao wazee wa 6m wanagesabika na wengi wao walikuwa na mitaji aidha kutoka kwenye mishahara, wazazi, n.k.

Hata robert Kayosaki alipata mtaji wake kutoka kwenye mshahara, Kina biil gates na Mark zuck wazazi wao walikuwa wananuka pesa
 
Mimi naongelea biashara kaka siyo duka,
Kuna mtu hapo juu kasema inawezekana hata maana ya biashara wengi wetu hatujui,na wewe panua akili na ujielimishe zaidi,biashara siyo duka pekee
 
Kwani hujui JF wanaongea humu kesho hao hao zikibuma wnakuja na id za kuomba ajira eti 6mil ni ndogo wanaumwa huyu nikki wa pili asingeenda kweny ajira
 
Watu wana utani kweli
 
Mimi naongelea biashara kaka siyo duka,
Kuna mtu hapo juu kasema inawezekana hata maana ya biashara wengi wetu hatujui,na wewe panua akili na ujielimishe zaidi,biashara siyo duka pekee
Biashara tu ya kuingiza 3 m as a profit baada ya kutoa gharama zote sio kitoto wapo kariakoo kibao miaka kibao wanaishia kuvaa nguo tu kali ila maendeleo bado sana miaka minne mtu hana nyumba biashara ngumu sio kitoto unajinyima time zaidi kuna jmaa wanafuatilia mizigo yao bandari mpaka usiku hawalali roho juu

Hatuongelei nduma ila real business inahitaji muda sana na biashara za mtaji mdogo kukua ni changamoto sana fanya business kitu hujui 90% ya motivational speakers haswa wa bongo sio wafanya biashara ila ni wakariri wa quotes na kusoma vitabu ishu inawapa uwakika kuishi ni zile sitting allowance per head wanaokuja kuhudhuria makongamano yao
 
Watu wana utani kweli
Watu wa humu ndani hujawazoea kwani 🤣🤣🤣🤣ndani ya ajira watu wanapata fursa kibao especially position za juu jiulize hao wakina mbowe si wafanya business wakubwa wanashika parefu ila wanataka ubunge na urais ili mambo yawe mazuri zaidi
 
Hizi story ukiwaambia watu waliopo Vodacom,Tigo,TCC,mgodini,Bandari,nmb,nssf,wataona una kichaa!!kama kuwa mtumwa ndio unapata overtime zaidi ya milioni mbili kwa wiki!basi huo utumwa mzuri.
Sasa hizo sehemu ulizotaja Kama umewekwa kimkakati sawa lakini Kama inategemea boss ataamkaje bado plan B ni muhimu sana.

Sent from my itel A16 using JamiiForums mobile app
 
Umeandika vizuri sana mkuu. Asante sana!
 
Biashara zimewanufaisha wengi ila kama unawaangalia watu walio jiajiri kwenye maduka ya rejareja mtaani hapo hata mm huwa nahisi zile biashara zina shida fulani ni wachache sana wanao toboa kimaisha wengi unaweza ukaanza shule ya msingi unamuona had unamaliza hali bado ni ileile maendeleo ya dukan kwake labda alete kabati jipya la kupangia bidhaa na kubadili muonekano wa duka tu.

Ila ukiingia town ukakutana na jamaa wenye maduka ya bidhaa za jumla au nguo , furniture & spare parts wale huwa wanamaendeleo siyo mchezo mchezo ndani ya miaka mi5 anapiga gape kubwa sana la maendeleo uwekezaji wake kwenye biashara unakua n mkubwa hata wahudumu pale dukani wanakua wengi sana.

Biashara ni nzuri sana hasa ukiiona fursa na ukawa na mtaji shida n kuwa sisi watt wa maskin mtaji hatuna ndo maana macho yetu tunaangalia upande wa kuajiriwa ili angalau tuweze kubadilisha maisha kutoka kwenye hali mbaya had kwenye hafadhali kidogo, na muda mwngne kuifanya ajira kama sehem ya kutafutia mtaji, Sasa mm sina mtaji alafu uniambie nijiajiri hapo lazma itakua n ngumu kukuelewa.
 
Wabongo wengi ni Self employed, hawa wanauza maduka wenyewe, wanafanya shughuli zote wenyewe, hapo mtu anageuka tayari kuwa mtumwa,

Hii ni tofauti na Business owner, hawa wanaajiri wengine kuwafanyia kazi, kama ni boda boda atatafta kijana, kama ni duka atatafuta wauzaji, n.k hawa ndio matajiri tunaowaona sasa,

Wengi hawajui kutofautisha hivyo vitu viwili
 
Nadhani kila mtu afanye anachoona ni sawa, wengine tumejiajiri huwezi kuniambia hayo unayosema nikakuelewa na nip private sector mwaka wa kumi na ushee, we endelea na ulichoona kinakufaa kila mtu na uwezo wake wa akili kwenye haya maisha.
 
Watu ambao ni wavivu , hupendelea mno kuajiriwa kuliko kujiari
 
Dah aisee mkopeshe mtaji
 
Hapo ukijitahidi sana utaanza kuwa machinga tu kubangaiza maisha!

Otherwise mtu anaona bora aajiriwe alipwe laki 7 kuliko kuteseka juani kuitafuta elfu 10 kila siku!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…