Tusipotoshane, ajira ina nafuu na uhakika zaidi kuliko kujiajiri

Hawa waajiliwa wa serikali vichwa vimelala 3M hela ndogo
 
Kingine...ujasiriamali Ni kutoka jasho la damu haswa.....kikubwa ili upite kwenye great boom(kutoka level moja Hadi nyingine ya kibiashara) katika biashara Ni LAZIMA Kuna sehemu ufanye kitu Cha hatari au mchongo mkubwa ili utoke stage moja ya kibiashara Hadi nyingine....ndio maana huyu ana duka la nguo..na Yule ana duka la nguo na eneo ni moja...lakini unakuta mmoja anampita mwenzie fasta kama kipanga...
 
Wacha mtaji wa 3m,
Hata wa 10m hauwezi kukupa 2.5m kwa mwezi,
Buashara ni ngumu siku hizi yaani hakuna biashara ya peke yako
 
sizitaku mbichi hizi, leo watu wapo mapumzikoni na familia zao na mshahara unaingia
 
Mleta mada nitajie tajiri yeyote mkubwa nchini au duniani kote alietajirika kupitia mshahara
hao ni kundi la pili nimeshaweka wazi, tatizo kundi la kwanza wanajidanganya wapo kwenye hilo kundi
 
Umekuwa mtamu kuzidi tende.
 
Japo nimeajiriwa umeongea point
 
Je mishahara ya miezi yote aliyolipwa kabla ya kustaafu umeuhesabu?
 
kutetea
Kuponda mfumo wa kujiajiri na kutukuza mfumo wa ajira kwa kutumia mazingira ya sasa ni kuikosea sayansi ya Uchumi madhubuti. Mazingira ya sasa yamelazimisha mfumo wa mzunguko wa pesa kwa sehemu kubwa kuanzia kwenye ajira. Wakati huo huo kumekuwa na mbinyo mkubwa wa kuruhusu pesa kuingia kwa kiwango linganifu kwenye mfumo wa kujiajiri. Mfumo wa sasa umewaachia watunzaji binafsi wa fedha kuamua ni eneo lipi pesa zao ziende. Kwa kulenga faida pekee, imethibitika kwamba waajiriwa wana nafasi nzuri inayowapa uhakika wenye pesa kupata faida.

Serikali kupitia wizara husika ni kama imejiondoa kwenye suala la kujiajiri kwa sababu ya changamoto zinazokabili sekta hii, ikiwemo uwezekano wa kupata hasara na kushindwa kufanya marejesho. Kupongeza na kuushangilia mfumo wa ajira ni sawa na kupalilia mgogoro wa ajira na kuwafanya wengi wafikirie kuajiriwa wakati ajira ni wastani wa asilimia 20 tu za soko la ajira. Mifumo ya upatikanaji mitaji kwa wanaojiajiri inatakiwa kuboreshwa na kujenga mifumo imara inayowalazimisha wanufaikaji kutopoteza pesa. Mifumo migumu ya kuzuia pesa inachangia sana kuiona sekta ya kujiajiri kupata ugumu na kujaribu kushawishi umma kwamba ajira ni bora kuliko kujiajiri.

Ili kuboresha mfumo wa kujiajiri ambao ndio unaozaa kumiliki biashara, ni muhimu kusema wazi kwamba ajira ni mbadala wa utumwa. Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu sisi sote tunajua kwamba dhamana ya mfanyakazi ni uzalishaji wenye tija na kuleta faida. Tumeona wengi wakifukuzwa kwa maamuzi ya mwenye biashara kwa sababu mbalimbali zikiwemo uzalishaji kupungua. Kama ambavyo tumeona baada ya janga la Corona, karibu nchi nyingi duniani watu wamepoteza ajira na hakuna wa kuwatetea. Dhamana ya ajira ni wakati unazalisha na kile unachozalisha kinaleta faida, Ukiondoa sekta saidizi ambazo hata kama sekta ya kujiajiri ingekuwa nzuri zaidi ya ajira, bado wangehitajika waajiriwa kwenye sekta saidizi za umma zinazotoa huduma kwa wananchi kama majeshi, hospitali, sheria na kadhalika.

Mataifa yaliyoendelea kama Marekani, uchumi wao unategemea ajira binafsi ambazo ndizo muhimili mkubwa wa uchumi wa viwanda, na mashirika makubwa ambayo baadaye yanatengeneza ajira yenye tija. Nchi zetu hizi ikiwemo Tanzania, itakuwa ni dhambi kubwa sana kutetea ajira na kudumisha sekta ya kujiajiri. Kwa kufanya hivyo, ni kama tunakinzana na lengo la kufikia uchumi wa viwanda. Watanzania wasaidiwe kujiajiri kwa kuanzisha viwanda vidogo kwenye mashamba yao vya kuboresha mazao yao. Vijana wawe na uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo wakijiajiri katika kusindika mazao ya wakulima na wazalishaji wa msingi. Jamii ifike mahali ambapo kila anayeenda shule, anaenda ili kuongeza ujuzi wa kujiajiri na kuboresha mazingira anayoishi. Juhudi hizi zikipata usimamizi mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali wasiokuwa na fitina, unafiki na ubinafsi, tatizo la ajira litapungua sana na kupunguza migogoro ya ajira.
 
Je mishahara ya miezi yote aliyolipwa kabla ya kustaafu umeuhesabu?
Mishahara ya wafanyakazi wengi inaishia kwenye rat race.....hivi Yani....kuamka asubuhi-kurudi jioni-kukopa katikati ya mwezi-mwisho wa MWEZI kulipa-....kinachobakia kidogo unasave..kabla hujakaa sawa matatizo nayo Yana Jambo lao na wew..Yani yanapukutisha saving zako...mwisho wa siku unakua kwenye mbio za panya...mtu inabidi akubali umri umeenda..inabidi sasa asubirie kiinua mgongo chake...ajifunzie biashara uzeeni😃😄😄...ikifeli kidogo Basi Ni stress mpaka pressure..kulaleki
 
But kuna back-up ya mikopo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…