Tusipotoshane, ajira ina nafuu na uhakika zaidi kuliko kujiajiri

Kujiajiri vs Kuajiriwa
Wale ma ceo wanaopokea mil 60 kwa mwenzi plus allowances za kutosha sijui wanasemaje ktk hili
 
Ajira kitu ingine, imagine huyo mkuu wa wilaya aliwai kuimba ''nakataa kuwa mtumwa najituma'' leo hii anatumwa kama kawaida tu, duh!
 
Umeandika vema sana.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Huu mjadala wa kujiajiri na kuajiriwa ni muhimu kujadiliwa kwa upana wake, maana Kuna sintofahamu nyingi hapo ambazo hupelekea baadhi ya watumishi wa serikali kuacha kazi na mwishowe kuanza kuishi kwa kutapatapa.
 
Huu mjadala wa kujiajiri na kuajiriwa ni muhimu kujadiliwa kwa upana wake, maana Kuna sintofahamu nyingi hapo ambazo hupelekea baadhi ya watumishi wa serikali kuacha kazi na mwishowe kuanza kuishi kwa kutapatapa.
Ni naona ajira ufanye huku unaokusanywa kama hauna mtaji kabisa na uwe na uwezo wa saving na malengo ya mda mfupi na mrefu .hii ni poa sana at least uanze business ukiwa bado inakupatia la mshahara ilisimama poa unaacha kazi mazima
 
Huu mjadala wa kujiajiri na kuajiriwa ni muhimu kujadiliwa kwa upana wake, maana Kuna sintofahamu nyingi hapo ambazo hupelekea baadhi ya watumishi wa serikali kuacha kazi na mwishowe kuanza kuishi kwa kutapatapa.
Usiache ajira ili kufanya biashara

Acha ajira, biashara ikianza kukulipa vizuri na kwa uhakika kuliko ajira yako.

Tatizo watu wengi hawana financial education, nashangaa sana mtu anamaliza mpaka chuo hajawahi kusoma vitabu muhimu kama rich dad poor dad au rich man in babylon, hivi vitabu ni muhimu sana kuvisoma kama unaweza kusoma.

Mtu anaacha ajira kisa kawasikiliza motivation speakers waliokariri quotes, motivational speaker anahubiri uache ajira sasa wewe jichanganye humo bila kuongezea akili yako, ndio utajua hujui.
 
Unasema?! Hivi nyie watu mnaishi wapi? Tokeni ndani ya maboksi hayo. Mshahara wa 6m kila mwezi ni hela ya kubeza biashara? Be serious man! Nilitaka nipite kimya ila uzalendo umenishinda.
Yani laki 2 per day eti ndio anatishika. Lol sina biashara lakin najua hio hela ni ndogo sana kwa wenye maduka makubwa ya jumla
 
We built this city,On these blocks we hustle,Turn bricks to whips, A-City the capital of crime!
 
Kila upande una faida na hasara pia,

1 (a) aliyeajiriwa anaweza kuwa na mikopo mingi ambayo hajaifanyia cha maana zaidi ya starehe
(b) aliyejiajiri atahakikisha mkopo unafanya kazi ya jinsi alivyopanga

2 (a) aliyeajiriwa kipato chake kina uwezo wa kumtosheleza endapo ana nidhamu ya fedha
(b) aliyejiajiri kipato chake inabidi awe na bajeti kali ili kumuwezesha kutekeleza majukumu mengine nje ya mahitaji ya kila siku

NB: Ajira hazipo ndio maana kujiajiri kunaonekana kunafaa, mtu akiwa na kianzio tu anaingia kupambana badala ya kusubiri ajira ambazo zina mamilion ya wahitaji wanaosubiri kuajiriwa
 
Kuna tofauti kubwa kati ya mfanyabiashara na mjasiriamali, mfanyabiashara anaweza kuacha biashara akatamani kuajiriwa; lakini mjasiriamali hana mtazamo wa kuajiriwa kamwe, yuko tayari hata zaidi ya miaka 10 apate hasara, lakini atimize kile anachokiamini. Wajasiriamali huwa ni 'greatest thinkers'. Mafanikio mnayoyaona hapa duniani ni kwa sababu ya wajasiriamali. Kwa mtazamo wako wewe, huna 'element' za ujasiriamali. Pia, ujasiriamali 'is not for every one'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…