Tusipotoshe, ukweli ni kwamba Samia Suluhu ni Rais wa Kikatiba na si Rais wa kuchaguliwa

Tusipotoshe, ukweli ni kwamba Samia Suluhu ni Rais wa Kikatiba na si Rais wa kuchaguliwa

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
651
Reaction score
2,246
Ni ujinga kunilazimisha eti Samia ni Rais wa kupigiwa kura!

Samia alikuwa msaidizi wa Hayati Magufuli ambaye ndiye aliyepigiwa kura za Watanzania kuwa Rais.

Lakini baada ya kifo cha Magufuli kikatiba makamu wake ndiye aliyepaswa kuwa mkuu wa Nchi. IELEWEKE,NI KWA MUJIBU WA KATIBA na si kwa MUJIBU WA WAPIGA KURA.

Kwa muktadha huo si sahihi kusema Samia ni Rais aliyepigiwa kura bali ni Rais ALIYEPO MADARAKANI KWA MUJIBU WA KATIBA na huo ndiyo ukweli.
 
Samia ni Rais wa JMT, mengine ni vibwagizo tu.

Mlipokuwa mnachagua RAIS mlikuwa mnachagua TICKET ya wawili ambao walikuwa MAGUFULI na SAMIA na ndiyo maana waligawana mikoa kwenda kuomba kura!

Samia alichaguliwa kwasababu alikuwa mmoja wa waomba ridhaa wa nafasi ile!! Ni kwa misingi hiyo Katiba inamtambua kuwa ni RAIS halali wa JMT.
 
Ni ujinga kunilazimisha eti Samia ni Rais wa kupigiwa kura!

Samia alikuwa msaidizi wa Hayati Magufuli ambaye ndiye aliyepigiwa kura za Watanzania kuwa Rais...
Nini maana ya running mate? Wakati unapiga kura si kulikuwa na watu wawili pale kwenye eneo la CCM ikiwa na maana kwamba unawapigia kura wote na ukijua kichwani kwamba likitokea la kutokea msaidizi atainuliwa?
 
Ni ujinga kunilazimisha eti Samia ni Rais wa kupigiwa kura!

Samia alikuwa msaidizi wa Hayati Magufuli ambaye ndiye aliyepigiwa kura za Watanzania kuwa Rais.

Lakini baada ya kifo cha Magufuli kikatiba makamu wake ndiye aliyepaswa kuwa mkuu wa Nchi. IELEWEKE,NI KWA MUJIBU WA KATIBA na si kwa MUJIBU WA WAPIGA KURA.

Kwa muktadha huo si sahihi kusema Samia ni Rais aliyepigiwa kura bali ni Rais ALIYEPO MADARAKANI KWA MUJIBU WA KATIBA na huo ndiyo ukweli.
Kwahiyo?!!! Tuungane na wewe kutomtambua au? Na vipi hilo linaleta faraja kidogo kutokana na upigaji mwingi wa mama?!!!
 
Back
Top Bottom