Tusipowakemea hawa wabunge wanaobeza elimu yetu na wasomi wetu, tutazalisha Taifa la hovyo kabisa

kwa halii hiiii bado mtasemwa sanaaaa
 
So kifupi Mkuu unaona ni Bora bunge lijaze Darasa la Saba wote ambao ndio washiriki kwenye utunzi wa Sheria na kuendesha nchi? Nauliza sababu nawe waona wasomi hawana maana
Kuna kusoma na kuna kuwa na akili ni vitu tofauti
Sheria ni utaratibu wa maisha watu wanaojiwekea
Achana na darasa la saba wasisome kabisa wanaweza kujiwekea utaratibu wa namna watakavyoendesha mambo yao na taratibu zinakafuatwa na kila kitu kikaenda sawa kabisa
Elimu ni muhimu lakini wasomi katika nchi yetu hawajatupatia kile ambacho tunastahili kukipata kutoka kwao
Kuna wakati maamuzi ya kiserikali yanafanywa hovyo kiasi kwamba unajiuliza hawa watu wana akili kweli!
Au akili gani ilitumika kufanya maamuzi kama haya unashindwa kuelewa huo usomi uko wapi


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hii nchi inawajinga wengi walioenda shule. Hao wajinga wanamchango mkubwa sana kutufikisha hapa tulipo.
Wenye akili fupi wanawalaumu vijana waliohitimu vyuo miaka hii; kuweka kumbukumbu sawa wengi wa wahitimu wa sasa ni matokeo ya mlipuko wa shule za kata na MEM bila ya uwekezaji wa kutosha miaka ya 2000 - 2008 hapo.
Watunga sera walilipua kwenye Elimu - fuatilia mchango DEO Filikunjombe (RIP) bungebni kuhusu shule za kata; matokeo mabovu ya kidato cha Nne 2012, n.k na sasa Elimu inalilipua taifa.
 
Hao akina Msukuma ni wa kupuuzwa,wanaongea Ujinga na kudharau Wasomi wakati huohuo watoto wao wanasoma shule za kimataifa!!!
 
Ni kweli tunamapungufu kama taifa na tunahitaji kuamka kutoka usingizini na kujikita katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia na tutoke kwenye zile sayansi za kula kwa urefu wa kamba😔
 
Baafhi walikubali ku compromise elimu yao kwa ajili ya faida za kisiasa.
Kama nimri
Very lame excuses!! Napster music community ilitengenezwa na dogo akiwa kwenye college dormitory.
Wenzetu wanapata matokeo ya elimu kwenye ujuzi waliojifunza, sisi huku matokeo ni hadi irudi tena kutoa back. Up.
 
Taifa limefika hapa tulipo kwasababu ya tunaowapa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi,(unyumbu), a.k.a kujizima data
 
Sema wasomi wengi mlio kwenye utumishi wa umma ni wazembe, wezi na wavivu.

Matarajio ya wananchi juu yenu yalikuwa makubwa, lakini mnachokifanya haki akisi usomi wenu. Kwakweli ninyi ndio mnaofanya, wasomi tuonekane hatuna tija katika taifa hili.

Hamtimizi majukumu yenu, ndio maana mnadharauriwa na darasa la saba.
 
Hata tusipowakemea elimu yetu ni ya ovyo sana mkuu
 
Hapa umetumia akili za kijiwe,yaani unasoma mpaka ya u Professor kwa kutumia ya kiingereza then bado lugha hiyo hiyo inakupiga chenga
Rais Ruto wa Kenya sio tu kasoma Sana Tena nchi za ulaya na america Bali nchini mwake kiingereza ni lugha ya kawaida, lakini bado juzi alikiri mbele ya umati kwamba kinamsumbua kuelewa anapokutana ma mfasaha wa lugha hiyo... Take note!!
 
Nadhani wewe ni mmoja wapo wawasomi wasikuwa na faida . kwanza tuanze na wewe uliye soma umeisadia nn jamii yako kupitia elimu yako ya juu?

sisi wafugaji na wakulima hawa wasomi wametutia hasara sana kwenye miradi yetu ya kilimo na mfugo
mtu katoka sua degree yake mlete shambani sasa hata kwenye kuku muulize kuku wangu anaumwa anaumwa nini
ni lazima azeme kwenye simu tena bila woga ana google kule mashambani ndo usiseme hakuna cha maana wanachofanya

imefikia hatua sasa ni heri uende kwa mkulima mzoefu akakupe abc kuliko hawa wasomi wasiokuwa na msaada wowote kwenye jamii.

mimi naungana na kishimba kwa 100% wasomi ndo mmetifika hapa tulipo sana sana mnasoma ili mjue namna nzuri ya kutuibia tu.

pale SUA kuna wasomi kibao lkn kinachofanyika hata hakieleweki lkn ni chuo kikubwa hasa
mbegu zote nzuri iwe breed ya ng,ombe wa maziwa tunatoa kenya mbuzi kenya ama uganda. ukija mbegu zinzo fanya vyema hasa za matunda kenya imetuacha mbali mno sio kwamba wasomi wanao semwa hatuna la hasha tuna maprofesa kibao yamkini hata ukijitolea umchimbie bwawa la samaki na kila kitu ukaleta kama hata ajiri mfugaji asiye soma basi tegemea maajabu makuu
 
Very lame excuses!! Napster music community ilitengenezwa na dogo akiwa kwenye college dormitory.
Wenzetu wanapata matokeo ya elimu kwenye ujuzi waliojifunza, sisi huku matokeo ni hadi irudi tena kutoa back. Up.
Hili sasa ni tatizo la mfumo sio la wasomi mmoja mmoja. Badala ya kuwafanyia bullying wasomi kama anavyofanya Msukuma bungeni tupige kelele mfumo ufanyiwe mageuzi otherwise mfumo utatuzalishia wasomi hawa hawa tu tulionao.
 
T

 
Msomi anapokutana na asie msomi,basi msomi anatakiwa kumijibu asie msomi kwa njia ya kisomi ili kudhihirisha uwezo wa usomi wake,lakini msomi anapofyata mkia mbele ya asie msomi,basi huyo msomi kuna mahali hapako sawa.
Msomi asie na uwezo wa kuleta mabadiliko, basi huyo ni mjinga kama wajinga wengine,ingali bado ujinga utabaki kuwa sifa na usomi utbaki kuwa uwezo wa kutumia maarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…