Tusipowakemea hawa wabunge wanaobeza elimu yetu na wasomi wetu, tutazalisha Taifa la hovyo kabisa

Yale majinga ya kisukuma yalishindwa shule sasa yanaumwa ugonjwa unaitwa "inferiority complex". Shida waliowachagua, pili kuruhusu std VII kugombea. Wanatukana elimu wakati watoto wao wanasoma shule za gharama kubwa, ila nna wasiwasi km hao watoto wenyewe watakuwa na akili
 
So kifupi Mkuu unaona ni Bora bunge lijaze Darasa la Saba wote ambao ndio washiriki kwenye utunzi wa Sheria na kuendesha nchi? Nauliza sababu nawe waona wasomi hawana maana
Tujaribu tuone, maana hao wachache waneonekana wana nafuu kuliko wasomi wengi. Au unaonaje mwanetu 😂
 
UKWELI LAZIMA USEMWE.
Kwa wele tuliokuwa wafuatiliaji wa shindano la kujibu maswali la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki lililokuwa likidhaminiwa na kampuni ya TOYOTA, tulishuhudia Udsm ilivyokuwa ikishika mkia kila mara.
Je, umesahau alichokisema Jenerali Ulimwengu kuhusu chuo kikuu cha Dar es Salaam, kwa kifupi ni SEKONDARI ILIYO JIONGEZA.
Ninakushauri mwezi wa saba katembelee banda la chuo kikuu cha Dar es Salaam kwenye uwanja wa maonesho wa Dar es Salaam barabara ya Kilwa, utapata jibu sahihi.
 
Nguvu ya Elimu ina Umuhimu Pale Elimu inapotumika,kama Una degree na unafanya mambo kama layman,nani ataona Umuhimu wa Elimu??Una masters ya SUA huna ajira unalalamika njaa??

Professor PhD holder unakua Ass kisser kwa Wana Ccm ku chase Teuzi,hiyo Ina sound vipi??

Hawa tunao waita "wasomi" ndio ilitakiwa wafanye mapinduzi katika nyanja zote,Kiuchumi,siasa,jamii,

Sasa hivi Kuna hoja ya muundo wa Muungano,mfate doctor Udsm akupe maoni yake na ushauri Nini kifanyike,Lazima amshukuru Mama.. pathetic,

NB: Wote hawakutaki Jalalani
 
Hao akina Msukuma ni wa kupuuzwa,wanaongea Ujinga na kudharau Wasomi wakati huohuo watoto wao wanasoma shule za kimataifa!!!
Sasa shida ndio ipo hapo hawapuuzwi.... Kila watakaloongea ndio linakua headline katika media zetu.... Yaani nchi yetu imekua ya kupenda kusambaza taarifu za hovyo zaidi kuliko Bora za kujenga. Wenye mawazo jengefu hawapati airtime Ila mawazo hovyo ndio airtime zaidi.
 
Mkuu wewe ukiumwa hua unahudhuria hospitali kupata matibabu au unajitibu mwenyewe?

Kuhusu Kuagiza Baadhi ya bidhaa/vitu nje Ambavyo ndani vipi sio ishu ya wasomi ni ishu ya mfumo na mfumo huo inaanzia Bungeni kwenye kutengeneza sera... Huwezi Kuta mtu kama Tundu Lissu (sio siasa) akawa Bungeni akasapoti "Sheria" ya (let say) SAMAKI anatoka ziwa Victoria anapelekwa Kenya wanamtoa ngozi au mifupa then arudishwe kuja kuuzwa Tena hapa... Noway.... Hayo yanafanywa na hao tunaowalalamikia kutuharibia mfumo wa nchi kwa kuiponda elimu...
 
No yote uliyosema sio lengo. Lengo ni kwamba wapunguze kudharau au kuishusha elimu yetu. Na kuaminika kwamba kwa kua wasomi Wachache hawafikii Matarajio yao/yetu basi elimu ionekane Haina maana.
 
Kwanza kabisa, ili tuwe pamoja, elimu ni nini?
Elimu Ina tafsiri Pana kutokana na Mahala wataka tumia.

Darasani: Elimu ni maarifa anayopata mtu au Maelekezo rasmi ambayo hakua nayo au Kuzaliwa nayo ili kumsaidia kubadili mfumo wa fikra zake katika kuchochea ubunifu. Na hupatikana darasani.

Mtaani: Elimu ni utambuzi wa Fursa mbalimbali ambazo hukua nazo ili kuzitumia kupambana na maisha. Na hupatikana Mtaani.

Dini: Elimu ni kumjua Mungu na mambo yake. Na hupatikana dinini au kidogo darasani.

NB: Hizi ni tafsiri zangu binafsi hazina uhusiano na tafsiri rasmi. Lakini pili mjadala huu ujikite kwenye elimu ya kwanza (darasani) ambayo inaenda kwa hatua.
 
Faza, unaisema hii elimu ya kuambiwa binadamu wa kwanza alitokana na sokwe akaenda akibadilika kutokana na mazingira ili hali mpaka leo kuna masokwe kibao yako porini?

Elimu hii isofata uhalisia miaka nenda rudi? Hivi unamfundisha mtoto kuhusu vita ya pili na kwanza ya dunia, inamsaidia nini?
 
Nakunaliana na hoja yako, haiwezekani wasomi wote wakadeliver sawa.... Watakaofeli, basi ni kuwaadress hao hawa particularly.... Lakini Hawa jamaa wanaponda wasomi kiujumla.... Hiyo ndio hoja yangu... Na angalia nilivyomalizia mwishoni
Wasomi wengi wamekuwa machawa hawana msaada ni wasaka vyeo wacha wapondwe
 
No yote uliyosema sio lengo. Lengo ni kwamba wapunguze kudharau au kuishusha elimu yetu. Na kuaminika kwamba kwa kua wasomi Wachache hawafikii Matarajio yao/yetu basi elimu ionekane Haina maana.
hakuna dharau kwenye Ukweli gentleman 🐒

unatakiwa uwaprove wrong kwa kwa vitendo na kwa kuibua alternatives plans kwakutumia maarifa ulopata kutokana na hayo madigrii yako kutatatua changamoto mbalimbali binafsi na kwenye jamii, ambazo hawa darasa la saba wanaziibua na kuwabeza waliosoma kwamba they have failed 🐒

lakini pia msomi kubishana na asie msomi ni changamoto, au msomi kumlalamikia asie msomi ni changamoto zaidi.

ni dhahiri kuna kutokujiamini na hofu tena ni ile fear of unknown, miongoni mwa wasomi dhidi ya wasio wasomi 🐒
 
Vipi na wasomi tulio nje ya ajira ndugu mlalamikaji Mtanzania 🤔
 
Rais Ruto wa Kenya sio tu kasoma Sana Tena nchi za ulaya na america Bali nchini mwake kiingereza ni lugha ya kawaida, lakini bado juzi alikiri mbele ya umati kwamba kinamsumbua kuelewa anapokutana ma mfasaha wa lugha hiyo... Take note!!
Yuko sahihi,lakini huwezi mfananisha na Jiwe ambaye hakuweza kunyoosha hata sentensi moja ya kiingereza. Wewe pia waweza sema kuwa kiswahili hukijui vizuri lakini siyo huwezi kuwa sawa na mtu kutoka Burundi
 
WEWE UTAKUWA NI MMOJA WAO WA WASOMI WAPUMBAVU .....NI UKWELI USIO PINGIKA KUWA TZ INAWASOMI FEKI TUPU KUANZIA WALIMU MPAKA WANAFUNZI ...KUANZIA PRIMARY MPAKA VYUONI ...TENA WASOMI WENYEWE SIYO FEKI TU HATA AKILI HAWANA
 
Acha ukweli usemwe wasomi wabovu ni zao la mfumo wa elimu mbovu, turekebishe mfumo wetu wa elimu kwanza.Leo hii tunaowaita wasomi ndio majizi makubwa, ndio wavivu hata kufikiria tu hawawezi matokeo yake hufanya maamuzi ya ovyo kabisa hata wasioenda shule hawawezi kufanya huo ujinga.Usomi ndio kufanya huo upuuzi?
 
NKNS...

#Mambo imechemka!

Usomi mashudu ni shida kweli--si uongo wala utani.

Mambo ya kumezeshwa, kumeza na kujimezesha mashudu ya maarifa yaliyochenjuliwa na 'wahuni'.

Hmmm



 
Vipi na wasomi tulio nje ya ajira ndugu mlalamikaji Mtanzania 🤔
Tafuta kazi ndugu msomaji.. si unaona mwenzio hapo juu katoka povu unadhani mi ndo babaake niliyemzaa 😂😂
 
Yuko sahihi,lakini huwezi mfananisha na Jiwe ambaye hakuweza kunyoosha hata sentensi moja ya kiingereza. Wewe pia waweza sema kuwa kiswahili hukijui vizuri lakini siyo huwezi kuwa sawa na mtu kutoka Burundi
Jiwe alikua mkemia si mlugha
 
WEWE UTAKUWA NI MMOJA WAO WA WASOMI WAPUMBAVU .....NI UKWELI USIO PINGIKA KUWA TZ INAWASOMI FEKI TUPU KUANZIA WALIMU MPAKA WANAFUNZI ...KUANZIA PRIMARY MPAKA VYUONI ...TENA WASOMI WENYEWE SIYO FEKI TU HATA AKILI HAWANA
Mkuu Kuna mawili, either tafuta hela au tafuta ajira, maana hizi hasira hakika ni za stress!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…