Tusipowakemea hawa wabunge wanaobeza elimu yetu na wasomi wetu, tutazalisha Taifa la hovyo kabisa

Tusipowakemea hawa wabunge wanaobeza elimu yetu na wasomi wetu, tutazalisha Taifa la hovyo kabisa

Hao akina Msukuma ni wa kupuuzwa,wanaongea Ujinga na kudharau Wasomi wakati huohuo watoto wao wanasoma shule za kimataifa!!!
Spot on!! Ilitakiwa upate clue kwa nini akina msukuma wanasomeaha watoto wao international schools.!!
Maana yake elimu yetu ina under perform, watu wanakariri kufaulu na sio kuelewa. Graduates kama kina mwinjaku wanapojinasibu hadharani kuwa ni machawa we huogopi?
I too, wouldn't take my son down that road, ni either asisome kama mie baba ake au nimsomeshe kwenye elimu ambayo itampa matokeo chanya, sio hii yetu kumfanya mtumwa.
 
Fatilia vyema hoja za Hawa jamaa.... Utagundua wanawaponda wasomi na usomi kwa ujumla kwa kua wao wametoboa kwa njia zao bila kusoma.... Fikiria nje ya box
Hili taifa changamoto sana, hawa wabunge wanaoponda elimu kweli wengi wamefanikiwa kiuchumi, ukimwambia aweke wazi aliwezaje, itakuwa ngumu sana kukuelezea. Wengi njia waliopitia ni kwa waganga, kuzulumu wenzao, bahati ya kuokota utajiri (hawa wa machinboni) nk. Kuna mwingine darasa la nne nakumbuka kampeni za mwaka 2015, alikuwa akijinadi kuwa yeye ni bingwa wa uchumi, kwamba kwake shilingi inazaa shilingi! 2020 akapata ubunge kupiti CCM, tumesubiri atupe hizo mbinu za shilingi kuzaa shilingi wapi, miaka 4 inakata sasa.
 
Habari wanabodi...

Nimekua mfatiliaji kidogo wa mijadala ya Bungeni hasa michango inayotolewa na wabunge mashuhuri wawili watatu hivi kuhusu Taifa na maendeleo yake Kiuchumi kisiasa na kiteknolojia.

Lengo la kuandika huu uzi sio kuwataja hao wabunge au kuwadhalilisha bali ni kuwakosoa ili kujenga Taifa bora Zaidi.

Mara zote katika michango yao, wabunge hawa wawili wamekua wakipinga sana ajenda ya usomi na wasomi wenyewe. Kwa haraka haraka wanaamini kabisa wasomi wetu ambao wapo katika sekta mbalimbali hakuna wanalolifanya kwa Kutumia elimu yao. Yaani kimsingi wanaamini mambo yataenda tu kienyeji bila elimu. Kifupi hawaamini kama elimu Ina msaada wowote katika kukuza chumi za nchi na ustawi wa wananchi wake.

Hawa watu ukiwafatilia kiundani ni watu waliofanikiwa kiuchumi kwa njia ambazo wao wanaamini hazikuhitaji elimu, sababu wao wameishia la saba. Hivyo wanaamini mtu yoyote sio lazima asome ili afanikiwe, kisa tu wao hawajasoma na wametoboa.

Tusipowadhibiti au kupinga hizi kauli zao za kibaguzi dhidi ya wasomi wetu, yamkini watoto au wajukuu zetu huko mbeleni wakipata hizi Hansard hawataona umuhimu wa kusoma, wataamini kama huyu "Joshua" alitoboa(ga) bila kusoma basi kumbe kuna short cut ya Maisha inawezekana.

TUWAKEMEE MARA MOJA.

Nawasilisha.

Mimi napinga kabisa kwamba usomi ndo unaleta maendeleo, kusoma kote huko sisi watanzania na bado nchi inazidi kuwa maskini tu, mimi najua tupate watu wa kuwajibika na kuleta maarifa, tupate watu wa kujua na kupambana, na mazingira kwenye jamii na kuondoa changamoto zinazowakabili, wananchi. Kwa mfano marekan ilianza kujengwa na watu wakaida kabisa wasio na elimu, na ndo waliiweka kwenye msingi ndo leo!
Kama unapinga Ina maana unataka kusema kutosoma ndilo kunakoleta maendeleo. Maendeleo ni pamoja na uboreshaji wa njia za kupunguza umaskini, maradhi na ujinga, kuboresha uchumi, njia za mawasiliano, huduma za jamii na kuleta maisha bora. Sioni mchango wa kutosoma katika haya yote. Propaganda hizi za kupuuza usoni na wasomi zilipata mwanya katika utawala uliopita na naona kwa sababu washabiki wake ni wale wasiosoma (kwa maana ya kutoelimika), naona zinajipenyeza tena. Msomi anayepuuza usoni naye hajasoma in the real sense. Usomi ninaouongelea ni hali ya kuwa enlightened. Kama mtu hakusoma (hakumaliza shule, hakwenda shule au hakupata nafasi ya kusoma) na ikatokea akapata fedha na kupata maendeleo si kwa sababu ya kutosoma. Ni kwa sababu ya kutumia maarifa na vitu alivyovipata vinavyotokana na usomi. Akiumwa na kwenda hospitali atapata huduma zinazotokana na usomi. Akitumia usafiri ni huduma inayotokana na usomi. Akitafuta haki mahakamani anatumia huduma inayotokana na usomi. Akila chakula bora ni kutokana na influence ya usomi etc. Nionyeshe jambo lolote la maendeleo linalofanyika na linalotokana na kutosoma ili tupate justification kwamba kumbe hata bila usomi maendeleo yanapatikana.
 
Mimi sina elimu ila ninazo akili nyingi kuweza kutambua wapumbavu wenye majina ya wasomi.....kuna mpuuzi kama wewe alibishana na mimi hapa kuhusu elimu nilimuumbua ....kulikuwa na hoja ya tz kuwa na MA IT nilimwambia hakuna IT yoyote tanzania ni ushuzi wa bata tu ...yeye akabisha nikamwambia ni kwanini tz hakuna ma IT ...jibu ni kwamba hata hao walimu wao vyuoni awawezi kufanya chochote cha maana kama ma IT sasa unategemea nini kwa wanafunzi wao.
Tena huko kwenye wataalamu wa IT ndio hovyo kabisa, ni moja ya eneo ambalo linajieleza vizuri jinsi elimu yetu ilivyo butu, watu hawana clue kabisa.
 
Sasa hao wasomi wameshindwa kujenga hoja za kujitetea hadi wananchi waone umuhimu wa Elimu?

Hadi wewe unawasemea inamaana wao wanakubaliana na hizo hoja na madai ya hao wabunge.
 
Nyerere aliendesha nchi kwa mafanikio makubwa sana bila kuwa na wasomi wa kutosha kwanini tumerudi nyuma baada ya kuwa na hao unaoita wasomi wa kutosha?
Viwanda vilikufa
Mashirika yalikufa na mambo mengine ya hovyo
Kwasababu huna akili za kutosha na huo usomi haujakusaidia chochote utasema tumepiga hatua kubwa lakini kiuhalisia kama kweli usomi ungekuwa umeplay part yake tungekuwa mbele mara mia kuliko pale tulipo sasa
Lakini kwasababu huna unachokijua pamoja na usomi wako wote hapa tulipo wewe uliye msomi unaona ni sawa sawa kabisa
Wenye akili wanaona nyie wasomi wa vyeti mnapamba, unapambana nini sasa
Tuambie mlifaulu kwenye jambo gani zaidi ya makaratasi tu
Umeme hovyo
maji hovyo
Barabara hovyo
Elimu hovyo
Hospitali hovyo
Uongozi hovyo
Taja mambo yanayokupambanueni kwamba nyie ni wasomi

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Wakati wa Nyerere tulikuwa na suasa ya ujamaa na kujutegemea, bidhaa Kama. Majembe na zana za kilimo nyingi tulizalusha wenyewe lakini wakati tuna wasomi wengi wanaweza kujenga maduka ili tuwe wachuuzi sads hivi majembe yanatika china,, chepeo,,, shika yaani badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma
Kafulila anajusifu kwa kulipa waziri wa fedha Hana mikakati wowote.
 
Nyerere aliendesha nchi kwa mafanikio makubwa sana bila kuwa na wasomi wa kutosha kwanini tumerudi nyuma baada ya kuwa na hao unaoita wasomi wa kutosha?
Viwanda vilikufa
Mashirika yalikufa na mambo mengine ya hovyo
Kwasababu huna akili za kutosha na huo usomi haujakusaidia chochote utasema tumepiga hatua kubwa lakini kiuhalisia kama kweli usomi ungekuwa umeplay part yake tungekuwa mbele mara mia kuliko pale tulipo sasa
Lakini kwasababu huna unachokijua pamoja na usomi wako wote hapa tulipo wewe uliye msomi unaona ni sawa sawa kabisa
Wenye akili wanaona siyo sawa nyie wasomi wa vyeti mnapambana, unapambana nini sasa
Tuambie mlifaulu kwenye jambo gani zaidi ya makaratasi tu
Umeme hovyo
maji hovyo
Barabara hovyo
Elimu hovyo
Hospitali hovyo
Uongozi hovyo
Taja mambo yanayokupambanueni kwamba nyie ni wasomi ili mueleweke hakuna hata kimoja badala yake watanzania tunadharaulika na hii nchi kidunia ni shamba la bibi tu kwa watu waliosoma huko kwenye nchi zao wanakuja hapa kuvuna

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Nyerere aliweza kwa sababu yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa mfumo, akisema tunakwenda kulia wote tunaenda kwakukimbia. Sasa hivi viongozi wengi ni "watoto wetu" nani anaweza kuwakemea, hebu nioneshe mtu mmoja ambaye anaweza kumkemea waziri na huyo waziri akatikisika, jibu ni hakuna, mwisho wa siku hawa mawaziri watakwambia "uhamie Burundi au mumuue" serious kabisa waziri anapata guts za kuongea kauli za hovyo namna hiyo! Nani wa kuwakemea?
 
Nyerere aliendesha nchi kwa mafanikio makubwa sana bila kuwa na wasomi wa kutosha kwanini tumerudi nyuma baada ya kuwa na hao unaoita wasomi wa kutosha?
Viwanda vilikufa
Mashirika yalikufa na mambo mengine ya hovyo
Kwasababu huna akili za kutosha na huo usomi haujakusaidia chochote utasema tumepiga hatua kubwa lakini kiuhalisia kama kweli usomi ungekuwa umeplay part yake tungekuwa mbele mara mia kuliko pale tulipo sasa
Lakini kwasababu huna unachokijua pamoja na usomi wako wote hapa tulipo wewe uliye msomi unaona ni sawa sawa kabisa
Wenye akili wanaona siyo sawa nyie wasomi wa vyeti mnapambana, unapambana nini sasa
Tuambie mlifaulu kwenye jambo gani zaidi ya makaratasi tu
Umeme hovyo
maji hovyo
Barabara hovyo
Elimu hovyo
Hospitali hovyo
Uongozi hovyo

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Ni Bora tanesco inabaki na la saba, Mamlaka za Maji zibaki na la saba, tanroads ibaki na la saba, hospitals zibaki na la saba, Mamlaka ya hewa ibaki na la saba. Idara au kampuni za mawasiliano zibaki na la saba. Vyombo vya ulinzi vibaki na la saba labda ndiyo tutayaona mabadiliko. Ingawa mi naamini mabadiliko makubwa katika nchi yanategemea uongozi. Nchi ikishakuwa na uongozi Bora kwingine kitanyooka tu
 
Sio vyema kubeza elimu yetu hata kidogo kwa tabia za wasomi wachache, Tukianza kuangalia tangu nchi hii imepata Uhuru maendeleo yote yamesimamiwa na nao wasomi wetu mfano.
Elimu
Afya
Miundo mbinu
Majeshi
Kilimo
Mawasiliano
Maji
Umeme
Nk.Tulipotoka na tulipo kwa juhudi za wasomi leo hii tukiondoa wasomi au tukafuta elimu Tukaruhusu washika Tunguli(wanganga) waendeshe nchi ninatumai tutakumbuka elimu yetu na wasomi wetu.
Vita ya wenye elimu vs wasio na elimu haijawai kuisha, ni Sawa na Vita ya wananchi vs watumishi wa Umma haina tofauti na Vita ya matajiri vs masikini ukweli
Ukweli usemwe ila ukweli unaoambatana na chuki ni kuaminisha vizaz vijavyo elimu haina umuhimu.
Nanukuu mh. Msukuma Aliwahi kusema sekita Fulani inapiga fine kubwa wananchi wanaongiza mifugo porini na hyo sekita wasipo Angalia watakufa wameinama. Alishangiliwa kwa kutetea wananchi kwa kuwachonganisha watumishi, ila ukweli sheria zote hutungwa na bunge na kuletea wasomi watafsiri why aongee vile ili hali ukweli anaujua kama sio chuki
Hoja za kishimba na Msukuma ni za kuchungwa Sana na ikiwesekana sipika asiwape Airtime kwa masilahi mapana ya nchi.
Imagine unaamka Hakuna mwalimu, nesi, PolisI, eng, kwa kifupi Hakuna chochote nchi itakuwaje.
Marehemu Lowasa aliwahi kusema ELIMU ELIMU ELIMU.
 
Sasa hao wasomi wameshindwa kujenga hoja za kujitetea hadi wananchi waone umuhimu wa Elimu?

Hadi wewe unawasemea inamaana wao wanakubaliana na hizo hoja na madai ya hao wabunge.
Haaaaaaahhhh wanaujua ukweli nikama watu wa dini tu wakiwa makanisani na misikitini wanajifanya wajuaji ila hoja ikija hapa JF kuhusu dini kamwe awajitokezi wanaogopa kuumbuka ...na wakijitokeza wanaficha vyeo vyao vya makanisani na misikitini mfano mitume manabii au wanena kwa roho mtakatifu uwezi kuwakuta hapa jf wakijibu maswali na kujitambulisha hivyo sababu ni kwamba wanajua kuwa hapa JF watakutana na watu tofauti na wale misukule yao makanisani na misikitini.
 
Sasa hao wasomi wameshindwa kujenga hoja za kujitetea hadi wananchi waone umuhimu wa Elimu?

Hadi wewe unawasemea inamaana wao wanakubaliana na hizo hoja na madai ya hao wabunge.
Swadaktaaaa
 
Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kuyachukulia kuwa hayapo. Ni mpumbavu tu anayedhani kuwa Professor LIPUMBA alivyositaafu na baadae kurudi ofisini kwa mitutu eti ame elimika kwa elimu bora na mpumbavu huyohuyo akambeza professor KABUDI aliyesema aliokotwa pale JALALANI UDSM eti akiamini kwamba KABUDI ame elimika kutokana na elimu bora aliyoipata.
Habari wanabodi...

Nimekua mfatiliaji kidogo wa mijadala ya Bungeni hasa michango inayotolewa na wabunge mashuhuri wawili watatu hivi kuhusu Taifa na maendeleo yake Kiuchumi kisiasa na kiteknolojia.

Lengo la kuandika huu uzi sio kuwataja hao wabunge au kuwadhalilisha bali ni kuwakosoa ili kujenga Taifa bora Zaidi.

Mara zote katika michango yao, wabunge hawa wawili wamekua wakipinga sana ajenda ya usomi na wasomi wenyewe. Kwa haraka haraka wanaamini kabisa wasomi wetu ambao wapo katika sekta mbalimbali hakuna wanalolifanya kwa Kutumia elimu yao. Yaani kimsingi wanaamini mambo yataenda tu kienyeji bila elimu. Kifupi hawaamini kama elimu Ina msaada wowote katika kukuza chumi za nchi na ustawi wa wananchi wake.

Hawa watu ukiwafatilia kiundani ni watu waliofanikiwa kiuchumi kwa njia ambazo wao wanaamini hazikuhitaji elimu, sababu wao wameishia la saba. Hivyo wanaamini mtu yoyote sio lazima asome ili afanikiwe, kisa tu wao hawajasoma na wametoboa.

Tusipowadhibiti au kupinga hizi kauli zao za kibaguzi dhidi ya wasomi wetu, yamkini watoto au wajukuu zetu huko mbeleni wakipata hizi Hansard hawataona umuhimu wa kusoma, wataamini kama huyu "Joshua" alitoboa(ga) bila kusoma basi kumbe kuna short cut ya Maisha inawezekana.

TUWAKEMEE MARA MOJA.

Nawasilisha.
 
Kwani sheria zilizoweka sifa za mtu kugombea nafasi ya Ubunge ambazo ni pamoja na kujua KUSOMA na KUANDIKA KWA KISWAHILI ziliwekwa na WATAALAMU au hao unawaita DARASA LA 7?
So kifupi Mkuu unaona ni Bora bunge lijaze Darasa la Saba wote ambao ndio washiriki kwenye utunzi wa Sheria na kuendesha nchi? Nauliza sababu nawe waona wasomi hawana maana
 
Yuko mbunge mmoja nampenda sana kwa kujua kujenga hoja japo elimu yake sio kubwa lakini ni dr
Anachoniuzi ni kimoja tu ana inferiority complex ya hali ya juu mno muda mwingi anaongelea yeye ni darasa la saba hii inakera sana.
Kama ana ponda usomi mbona watoto wake wanasoma nchi za nje

Hili tatizo la inferiority complex limejikita sana kanda flani nchi hii

Marekani kuna mabilionea sana lakini sio watu walio na elimu ndogo ndogo kama huku kwetu hadi kutoa makafara na kuua watu ndio watajirike huu ni ukenge sana.
Unaweza kuwa tajiri huna elimu lakini ukawa unaishi maisha ya kijima aheri asiye na utajiri kabisa.
Nitoe mfano una ng,ombe 10,000 how come uwe bado unalalia ngozi ya ngombe na huli nyama hadi afe au utokee msiba.

Hapa ndio inapokuja tofauti ya Tajiri aliyekwenda shule na tajiri ambaye hajakwenda shule kabisa.Akipata kanafasi kadogo anasumbua sana watu.

Aliyeweka sheria mbunge awe na sifa tatu KKK Kuongea,Kusoma na Kuandika aliweka wakati wa uhuru watu walikuwa hawajaelimika sana hii sheria irekebishwe.

Enzi hizi sio enzi za kina bibi Titi Mohamed kwenda ziara China anamuambia mzungu we are eating the country yaana tunakula nchi hadi Nyerere kumpiga kibao alivyorudia baada ya kutia aibu ugenini maana mzungu alishangaa how can you eat the country.
 
Tanzania njaa nyingi sana yaani mtu akiwa na pesa wengine wote ni wapumbavu na hii inaletwa na kuwepo kwa gap kubwa lililopo baina ya wenye nacho na wasio nacho

Lakini level ikiwa sawa na watu wakaacha kulingishiana vigari vya afu 3 ushamba utatutoka wa kuiba rasilimali za nchi na kudharau taaluma
Kabisa
 
Habari wanabodi...

Nimekua mfatiliaji kidogo wa mijadala ya Bungeni hasa michango inayotolewa na wabunge mashuhuri wawili watatu hivi kuhusu Taifa na maendeleo yake Kiuchumi kisiasa na kiteknolojia.

Lengo la kuandika huu uzi sio kuwataja hao wabunge au kuwadhalilisha bali ni kuwakosoa ili kujenga Taifa bora Zaidi.

Mara zote katika michango yao, wabunge hawa wawili wamekua wakipinga sana ajenda ya usomi na wasomi wenyewe. Kwa haraka haraka wanaamini kabisa wasomi wetu ambao wapo katika sekta mbalimbali hakuna wanalolifanya kwa Kutumia elimu yao. Yaani kimsingi wanaamini mambo yataenda tu kienyeji bila elimu. Kifupi hawaamini kama elimu Ina msaada wowote katika kukuza chumi za nchi na ustawi wa wananchi wake.

Hawa watu ukiwafatilia kiundani ni watu waliofanikiwa kiuchumi kwa njia ambazo wao wanaamini hazikuhitaji elimu, sababu wao wameishia la saba. Hivyo wanaamini mtu yoyote sio lazima asome ili afanikiwe, kisa tu wao hawajasoma na wametoboa.

Tusipowadhibiti au kupinga hizi kauli zao za kibaguzi dhidi ya wasomi wetu, yamkini watoto au wajukuu zetu huko mbeleni wakipata hizi Hansard hawataona umuhimu wa kusoma, wataamini kama huyu "Joshua" alitoboa(ga) bila kusoma basi kumbe kuna short cut ya Maisha inawezekana.

TUWAKEMEE MARA MOJA.

Nawasilisha.
Elim yetu inadharaulika coz hailipi kama siasa ilipavyo!

Professor anajiona yupo jalalani pale udsm Bora akalale Bungeni apige hela!

Thamani ya elim yetu ilipe na utafiti uongezewe fedha ili kuikuza elim yetu!
 
Unaona sasa!!! Ndio maana wasomi wetu mnadharaulika, sababu yapoor reasoning!
Next time Nikikwambia siendi Kusi haimaanishi kuwa naenda Kaskazi.!!
Ngumbaro ku dharau wasomi wetu inatokana na wasomi wetu ku under perform, haimaanishi kwa amba elimu haina umuhimu.
Nimetoka mfano hapo wa mtoto wa collage aliyezindua world's first peer to peer music sharing program( napster) akiwa dormitory, Msomi wetu anamaliza chuonna degree halafu wala hajui ataifanya nini kutokana na elimu yake zaidi ya utumwa wa ajira.
Hujui unaloongea wewe , nionyeshe ni nchi gani au taifa gani ambalo lina mfumo wa elimu au Mtaala unaomfundisha mtu kuwa enterpreneur .
Mtu kuwa mjasiriamali au mbunifu ni suala la mfumo wa nchi husika jinsi unavyotoa incentives na means za watu kuwa wabunifu na wajasiriamali .
Kuna mfano mtu katoa huko juu
Leo hii unagraduate WA doctors of medicine , Engineering nk , unafikiri huyu mtu atadevelop service au product ipi kwa sector yake bila kuwa na startup capital kubwa ya kueleweka na miundombinu ya kufanikisha hilo ?
Au unafikiri hao madogo wanaodevelop hizo software programs mpaka zinaingia sokoni na kuanza kugenerate income ni out of nowhere kama fairy tales unazoandika humu ,kwamba dogo kadevelop software Tu ya kushare mziki peer to peer kwenye dormitory halafu paap software ikawa consumed na millions of people na kuanza kuingiza pesa .

Unajua lolote kuhusu venture capital na miundombinu ya kusuport kazi za uvumbuzi na ubunifu mfano pale silicon valley , Marekani ?
Unajua capital and resources injection inayofanyika kule mpaka hizo software kuingizwa sokoni ?
Au unafikiri kazi za ubunifu na uvumbuzi ni kama biashara ya kuuza viazi Buguruni ?

Acha ujinga
 
Hili taifa changamoto sana, hawa wabunge wanaoponda elimu kweli wengi wamefanikiwa kiuchumi, ukimwambia aweke wazi aliwezaje, itakuwa ngumu sana kukuelezea. Wengi njia waliopitia ni kwa waganga, kuzulumu wenzao, bahati ya kuokota utajiri (hawa wa machinboni) nk. Kuna mwingine darasa la nne nakumbuka kampeni za mwaka 2015, alikuwa akijinadi kuwa yeye ni bingwa wa uchumi, kwamba kwake shilingi inazaa shilingi! 2020 akapata ubunge kupiti CCM, tumesubiri atupe hizo mbinu za shilingi kuzaa shilingi wapi, miaka 4 inakata sasa.
Ukanjanja mwingi nchi hii , hamna clear path inayoforce watu kutengeneza wealth Kwa kutumia akili , taaluma na elimu .
Huyu mpumbavu anayesema elimu haina maana , kama anajiamini na anachoongea aende na hivyo leo hii tumpeleke developed nation yoyote halafu aanze from scratch tuone kama anaweza toboa .
Angalia wealthy individuals top 20 pale Marekani kama utakuta kuna mbumbumbu mule
 
Hili taifa changamoto sana, hawa wabunge wanaoponda elimu kweli wengi wamefanikiwa kiuchumi, ukimwambia aweke wazi aliwezaje, itakuwa ngumu sana kukuelezea. Wengi njia waliopitia ni kwa waganga, kuzulumu wenzao, bahati ya kuokota utajiri (hawa wa machinboni) nk. Kuna mwingine darasa la nne nakumbuka kampeni za mwaka 2015, alikuwa akijinadi kuwa yeye ni bingwa wa uchumi, kwamba kwake shilingi inazaa shilingi! 2020 akapata ubunge kupiti CCM, tumesubiri atupe hizo mbinu za shilingi kuzaa shilingi wapi, miaka 4 inakata sasa.
Mtu kama Warren Buffet ,Bill Gates , Bezos ,Musk nk ,wamezungukwa na teams za brilliant scholars Kwa fani mbalimbali katika miradi yao ,na hao ndio watendaji wa hiyo miradi .
Hao ndio washauri ,wasimamizi na wealth creators kwenye hizo kampuni na miradi na kuwafanya hao mabwana kuwa mabilionea na kuendelea kuwa mabilionea .

Leo hii unaweza ukamchukua kilaza pro max kama King Msukuma ,au Lusinde au Kishimba kuwa manager WA au CEO WA space X , Nvidia JP Morgan au mradi wowote wa bilionea na akauendesha na kusustain wealth generation kupitia huo mradi ?

Watu wapumbavu hawajiulizi hili swali ,wamekalia kuponda elimu tu .
 
Mtu kama Warren Buffet ,Bill Gates , Bezos ,Musk nk ,wamezungukwa na teams za brilliant scholars Kwa fani mbalimbali katika miradi yao ,na hao ndio watendaji wa hiyo miradi .
Hao ndio washauri ,wasimamizi na wealth creators kwenye hizo kampuni na miradi na kuwafanya hao mabwana kuwa mabilionea na kuendelea kuwa mabilionea .

Leo hii unaweza ukamchukua kilaza pro max kama King Msukuma ,au Lusinde au Kishimba kuwa manager WA au CEO WA space X au mradi wowote wa bilionea na akauendesha na kusustain wealth generation kupitia huo mradi ?

Watu wapumbavu hawajiulizi hili swali ,wamekalia kuponda elimu tu .
Njaa tu zinatusumbua na wengine uelewa mdogo unatakiwa ukiwa na elimu uwe superman ugundue vitu kwa miujiza, uwe na hela bila ajira tena bila kujali faculty uliosomea kila kitu watakiwa uwe unakielewa mfano umesomea ualimu lakini mambo za sheria, biashara, technology, elimu ya anga, engineer n.k vyote uwe unavielewa na uwe na pesa kuwazidi wasiosoma tofauti na hapo elimu haina maana
 
Back
Top Bottom