Tusipowakemea hawa wabunge wanaobeza elimu yetu na wasomi wetu, tutazalisha Taifa la hovyo kabisa

Tusipowakemea hawa wabunge wanaobeza elimu yetu na wasomi wetu, tutazalisha Taifa la hovyo kabisa

Nchi ikitengeneza incentives za watu kuwa creative na kufanya innovations na hapa ninaposema incentives ni kutengeneza mazingira mfano hizo colleges na universities kuzitengezea funds za kutosha na kuhakikisha zinakuwa ni Research departments zilizo bora , kuhalika wanunuzi na wawekezaji wa ideas za kivumbuzi kutoka kila kona ya dunia kuja Tanzania kuona kilichopo kwa graduates wake , kama kinachofanyika kule Marekani Silicon valley , Carlifonia , inakuwa kama nanenane flani ila hii inakuwa very specigic kwa maonyesho ya vumbuzi za kiteknolojia , bidhaa na huduma zake .
Watu waonyeshe umaridadi wao na talents walizo nazo na ideas na prototypes walizo nazo .

Hamna atakayeambiwa awe innovative , watu wenyewe watajikita kuresearch na kudevelop ideas mpya na kuzigeuza kuwa products au services .
Lakini hii ya mtu anapiga Mihayo ya njaa kali anawaza Tonge la ugali , unafikiri huo utulivu wa akili na hata resources za kuimplememt ideas zake anapata wapi ?
Nchi ambazo raia 90 percent ya raia wake wapo wanawaza kupata basic needs , unafikiri watadevelop nini kwa mwendo huu ?
Si ajabu leo hii hata maprofesa wengi wanaukimbia uprofesa hilo vyuoni na wanaenda kupambana kuingia kwenye siasa ili wawe machawa maana njaa ni kali huko kwenye vyuo , ambapo kiuhalisia zilipaswa kuwa academic and research institutes .
Lazima wawaze kuwa wachuuzi wa chupi za kichina na kuuza vitunguu gengeni .
Kama hamna incentives ni ndoto hicho kitu kutokea .
Na hii si Tanzania tu ,hii ni systemic issue katika Nchi za Kiafrika .
Nenda popote Africa , ni yale Yale .
With few exceptions labda Misri na south Afrika ndio wanajitahidi ,ila nao hawako levels ambazo tunaweza kuwaita innovative economy .
Bado hawapo hata karibu ya kufikia levels hizo .
Maana yake ni kuwa serikali inatakiwa iweke bajeti kwenye sector ya elimu mara tatu zaidi ya bajeti ya sector zote nchini sio kuongea maneno tu ya kisiasa bila pesa
 
Mie nimesoma historia ya zwangendaba na lubalunda empire na hakuna nilipo apply, hovyo tu,

nilimeza kile kitabu cha advanced marth na lile likitabu la physics tulikuwa tunaliita abbott, yaani mwalimu aliandika swali namtajia hadi ukurasa wa jibu lilipo ka mwinjilisti wa kisabato,

Sasa ile story ya manenge na mandawa ilikuwa ya nini? Na stori za juma roza.

Ile research paper niliyogundua uhusiano wa rushwa na umasikini sijawahi hata kupewa tuzo. Kuna kiongozi aliwahi sema hajui kwanini sisi ni masikini, nikafanya research hadi nikagundua kwanini sisi ni masikini hadi leo namimi ni masikini.

Bora hizi digirii ziwe kama hati ya nyumba tuweze kuchukulia mkopo au kuwekwa dhamana mahakani nikiwa na kesi,
 
Tatizo letu tunapewa elimu ya kimagharibu ambayo sio asili yetu, ndo maana inanufaishaifa mataifa, hayo tu sisi [QUOTE="Magobe T, post: 50318411, member: 9922"
Kama unapinga Ina maana unataka kusema kutosoma ndilo kunakoleta maendeleo. Maendeleo ni pamoja na uboreshaji wa njia za kupunguza umaskini, maradhi na ujinga, kuboresha uchumi, njia za mawasiliano, huduma za jamii na kuleta maisha bora. Sioni mchango wa kutosoma katika haya yote. Propaganda hizi za kupuuza usoni na wasomi zilipata mwanya katika utawala uliopita na naona kwa sababu washabiki wake ni wale wasiosoma (kwa maana ya kutoelimika), naona zinajipenyeza tena. Msomi anayepuuza usoni naye hajasoma in the real sense. Usomi ninaouongelea ni hali ya kuwa enlightened. Kama mtu hakusoma (hakumaliza shule, hakwenda shule au hakupata nafasi ya kusoma) na ikatokea akapata fedha na kupata maendeleo si kwa sababu ya kutosoma. Ni kwa sababu ya kutumia maarifa na vitu alivyovipata vinavyotokana na usomi. Akiumwa na kwenda hospitali atapata huduma zinazotok
 
Tatizo elimu yetu, iko kimagharibi sana, hatuna elimu ya kiuhalisia wa kiafrika? yani elimu ya asili, yetu africa? elimu inamtego wa kiutumwa kwa ajili mataifa ya ulaya magharibi, uchina walikuja na mfumo wao, wa elimu asilia, umepiga hatua kubwa sana, nchi za kiafrica ziko nyuma sana, kwa kuendekeza, elimu ya mfumo wa kikoloni.
 
Hoja zao ni kali sana kwa wasomi ku absorb, na hoja za msukuma zinaambatana na kejeli kwa ajili ya kuwa yeye ameshatoboa!!,
Lakini haiondoi ukweli kuwa wasomi wetu hawana clue kwenye kuondoka chamgamoto zinazotukabili.
Bandari tumefeli kuendesha, Gas ya Mtwara mikataba haieleweki, kwenye madini ndo hakueleweki kabisa.

Mtu msomi wa PhD anaweza akaamka akafuta matokeo ya Uchaguzi mkuu au akaamua kuufuta upinzani.

Kwa kweli katika kaelimu kadogo nilichonacho ila nakubaliana na hao wabunge wanaowabeza wasomi ndani ya Taifa hili.
 
So kifupi Mkuu unaona ni Bora bunge lijaze Darasa la Saba wote ambao ndio washiriki kwenye utunzi wa Sheria na kuendesha nchi? Nauliza sababu nawe waona wasomi hawana maana
Huhitaji kuwa na elimu ili usiuze bandari, mbona akina Wazee wetu walipambana kumpinga mkoloni kwa kupigania maslahi yao na hawakuwa wamesoma?

Si Bunge hilihili ndio linashindwa kumpinga Rais hata kama akifanya lolote baya? Si ndo Bunge hilihili linapitisha mambo ya hovyo ndani ya Taifa? Kwani hakuna wasomi?
 
Unachanganya siasa na elimu, kinachoturudisha nyuma ni siasa za tz sio elimu

Elimu ikiheshimiwa na tukaweka siasa uchwara na njaa pembeni maendeleo ni dk 0
Sio kuaminia tu watu waliopata elimu na kuwanyima haki ambao hawakubahatika kupata elimu, lakini kunawatu hawakupata elimu, ni wajuzi na wanamaarifa, ya kujenga misingi ya maisha bora ya kijamii, kuliko hata waliosoma, zaidi' kujinufaisha wao tu? haki iwe kwa wote atakayeonyesha upeo kwa mazingira fulani" aidha wasio na elimu na mwenye elimu.
 
Hii mada ingetolewa ufafanuzi na wasomi wenyewe. Naona comment za wasiosoma nyingi zinatolewa kwa chuki dhidi ya waliosoma.
Hii ndiyo inadhihirisha wazi kwamba hao wanaojiita wasomi hawana usomi hata wa kujenga hoja ya kutetea usomi wao.
 
Bado yupo pangoni huyo. Hakuna msomi hapa. instagramer unakwepa mjadala sheikh? [emoji3]
No nilibanana na majukumu ya weekend. Bado siungi mkono hizi hoja za kuwatetea wakina Msukuma and the likes, katika swala la kuwapinga na kuwakebehi wasomi.. Cha kupinga ni mfumo wa siasa zetu zaidi ambao haumpi nafasi Msomi Kutumia usomi wao kutatua changamoto za maendeleo.
 
Kwa Tanzania, unaweza kabisa kukuta huyo mbunge anayewasema wasomi, hao wasomi, na huyu member wa JF anayewatetea wasomi wote ni vilaza.

We si unaona mjadala mdogo tu nampeleka mdogomdogo kwa Socratic Method tujue mzizi wa fitna kakimbia tayari?

Sasa msomi ni mtu wa kukimbia maswali ya Socratic Method kwenye mazungumzo basic kama haya?
Nipo hewani. Bado hoja yangu ni Ile Ile sijaona ushawishi humu. Bado napinga tabia ya wakina Msukuma and the gang kuponda wasomi wetu. Walipaswa waponde mfumo wetu wa kisiasa ambao hauwapi nafasi wasomi kutatua changamoto za maendeleo.
 
Kama unapinga Ina maana unataka kusema kutosoma ndilo kunakoleta maendeleo. Maendeleo ni pamoja na uboreshaji wa njia za kupunguza umaskini, maradhi na ujinga, kuboresha uchumi, njia za mawasiliano, huduma za jamii na kuleta maisha bora. Sioni mchango wa kutosoma katika haya yote. Propaganda hizi za kupuuza usoni na wasomi zilipata mwanya katika utawala uliopita na naona kwa sababu washabiki wake ni wale wasiosoma (kwa maana ya kutoelimika), naona zinajipenyeza tena. Msomi anayepuuza usoni naye hajasoma in the real sense. Usomi ninaouongelea ni hali ya kuwa enlightened. Kama mtu hakusoma (hakumaliza shule, hakwenda shule au hakupata nafasi ya kusoma) na ikatokea akapata fedha na kupata maendeleo si kwa sababu ya kutosoma. Ni kwa sababu ya kutumia maarifa na vitu alivyovipata vinavyotokana na usomi. Akiumwa na kwenda hospitali atapata huduma zinazotokana na usomi. Akitumia usafiri ni huduma inayotokana na usomi. Akitafuta haki mahakamani anatumia huduma inayotokana na usomi. Akila chakula bora ni kutokana na influence ya usomi etc. Nionyeshe jambo lolote la maendeleo linalofanyika na linalotokana na kutosoma ili tupate justification kwamba kumbe hata bila usomi maendeleo yanapatikana.
Yes. This is the logic
 
Mimi nimesoma nimefika chuo -Ila wasomi wa Tanzania kwa kiwango kikubwa wapo nyuma Elimu haijawasaidia .

Fatilia vizuri wasomi wetu utagundua hilo jambo.

Wachache uno waona wapo smart ni wale ambao walitumia muda wao na gharama kujitafutia maarifa nje ya mtaala rasmi. Kama kusoma Sana vitabu n.k

MTU msomi hata kiingereza hajui, MTU msomi anatukana matusi , MTU msomi mwizi anaiba pesa za walipa kodi ,MTU msomi mzinzi. Anabeti ,mlevi

Hapa Tanzania hamna wasomi Kama wasomi
 
Huhitaji kuwa na elimu ili usiuze bandari, mbona akina Wazee wetu walipambana kumpinga mkoloni kwa kupigania maslahi yao na hawakuwa wamesoma?

Si Bunge hilihili ndio linashindwa kumpinga Rais hata kama akifanya lolote baya? Si ndo Bunge hilihili linapitisha mambo ya hovyo ndani ya Taifa? Kwani hakuna wasomi?
Kutokana na mfumo wa kisiasa wa nchi hii mambo mengi yanafanywa ay yanapaswa kufanya kwa utashi binafsi tu na sio elimu. Hata Bunge lingejaa vilaza wa lasaba bado wasingeweza kupinga maamuzi ya Rais.
 
Nipo hewani. Bado hoja yangu ni Ile Ile sijaona ushawishi humu. Bado napinga tabia ya wakina Msukuma and the gang kuponda wasomi wetu. Walipaswa waponde mfumo wetu wa kisiasa ambao hauwapi nafasi wasomi kutatua changamoto za maendeleo.
Nimekuuliza utajuaje huyu ni msomi na huyu si msomi, umekimbia bila kujibu.

Unapoangalia hili suala kama Msukuma kupinga wasomi wetu tayari ushakosa usomi.

Msomi anachambua hoja, msomi anajua abstract thinking.

Msomi haangalii habari kama ya Msukuma vs wasomi.

That is personalizing the matter. That is lacking abstract thinking and nuance.

Msomi anatakiwa juweza kufanya abstract and critical thinking beyond all tgese personal squabbles za watu ambao hawajaenda shule kama kina Msukuma na walioenda shule lakini si wasomi kama hao wengi mnaowaita wasomi wa Tanzania.

Inawezekana kabisa Msukuma akawa wrong ku criticize culture ya usomi lakini akawa right ku criticize wasomi wa Tanzania wasio na results kwenye matatizo nengi tu. Watu wanaosoma kupata Ph.D ya kuongeza mshahara bila kuwa na matunda si wasomi, hao ni office seekers tu. Msukuma akiwasrma hawa yuko right, ingawa kuwalundika wasomi wote kundi moja au kuulaumu utamaduni wote wa usomi ni makosa pia.

So this is not a simple matter if whether Msukuma is right or wasomi wako right. That is a lazy false dichotomy.
 
Mimi nimesoma nimefika chuo -Ila wasomi wa Tanzania kwa kiwango kikubwa wapo nyuma Elimu haijawasaidia .

Fatilia vizuri wasomi wetu utagundua hilo jambo.

Wachache uno waona wapo smart ni wale ambao walitumia muda wao na gharama kujitafutia maarifa nje ya mtaala rasmi. Kama kusoma Sana vitabu n.k

MTU msomi hata kiingereza hajui, MTU msomi anatukana matusi , MTU msomi mwizi anaiba pesa za walipa kodi ,MTU msomi mzinzi. Anabeti ,mlevi

Hapa Tanzania hamna wasomi Kama wasomi
You're partly right! Nakumbuka enzi za serikali ya Kikwete kulikuwa na mijadala kwenye TV au redioni na nilikuwa naifuatilia kwa karibu sana. Kuna pia This Week in Perspective, kipindi ambacho lilikuwa kikirushwa na TBC na akina Prof K Mumbo, Ayubu Rioba na wengine wengi walikuwa wachangiaji wazuri sana. Wote hawa walibadilika wakati wa Magufuli na tangu wakati huo wakaanza kuwa na msimamo tofauti wa uchangiaji. Kipindi cha This Week in Perspective nadhani kilisitishwa. Kuanzia hapo wasomi wetu wakaanza kuzika usomi wao. Critical thinking yao ikapotea kabisa! Na sidhani kama tutarudi kupata critical/intelligent thinkers. Of course, mmoja mmoja wapo, lakini wanavyoshambuliwa na 'mbumbu mzungu wa reli' ni ajabu kabisa!
 
Nimekuuliza utajuaje huyu ni msomi na huyu si msomi, umekimbia bila kujibu.

Unapoangalia hili suala kama Msukuma kupinga wasomi wetu tayari ushakosa usomi.

Msomi anachambua hoja, msomi anajua abstract thinking.

Msomi haangalii habari kama ya Msukuma vs wasomi.

That is personalizing the matter. That is lacking abstract thinking and nuance.

Msomi anatakiwa juweza kufanya abstract and critical thinking beyond all tgese personal squabbles za watu ambao hawajaenda shule kama kina Msukuma na walioenda shule lakini si wasomi kama hao wengi mnaowaita wasomi wa Tanzania.

Inawezekana kabisa Msukuma akawa wrong ku criticize culture ya usomi lakini akawa right ku criticize wasomi wa Tanzania wasio na results kwenye matatizo nengi tu. Watu wanaosoma kupata Ph.D ya kuongeza mshahara bila kuwa na matunda si wasomi, hao ni office seekers tu. Msukuma akiwasrma hawa yuko right, ingawa kuwalundika wasomi wote kundi moja au kuulaumu utamaduni wote wa usomi ni makosa pia.

So this is not a simple matter if whether Msukuma is right or wasomi wako right. That is a lazy false dichotomy.
Sikubaliani na maswali yako.. Ila nakubaliana na hoja zako katika paragraph mbili za mwisho. Upo sawa.

Lakini tukumbuke usomi wa nchi hii unaathiriwa Kwa kiwango kikubwa na mfumo wa uendeshaji nchi kisiasa. Na ndio maana wasomi wengi wanataka kua Wanasiasa... Sio tu kimaslahi, lakini pia kupitia siasa ndio mtu anaweza kusikilizwa zaidi na kua na ushawishi binafsi.

Na Hilo ndio jambo limesababisha Hawa kina Musukuma and the likes wachukulie poa wasomi. Ishu sio wasomi wameshindwa ku'deliver.. no way na doesn't make sense, ishu ni laymen waliopata fedha bila kusoma kuamini inawezekana kufanikiwa bila elimu. Na on top of that wakiona maprofesa wawili watatu wameongea utumbo kama wao Bungeni na kupigiwa makofi basi wanaamini wao wapo sawa pia.. stupid!
 
You are still in a false dichotomy like you did not understand what I wrote.

This is more complex than just wasomi vs laymen.

Na wewe tatizo lako unaandika lazily "sikubaliani na maswali yako..." bila hata kueleza hukubaliani na nini.

Hutaki nuance. Unawezaje kujadili usomi bila kutaka nuance? Nakuuliza unajuaje huyu msomi na huyu si msomi, unakimbia swali. Are you even qualified to talk about this subject?

Huyo Msukuma na wenzake kwa kiasi kikubwa ni wajinga, wana imani kwamba kupata hela ni ujanja zaidi ya usomi. Wanaamini wana "street smarts" na "natural intelligence", wakati ukiwasikiliza mostly wana hoja za kijinga.

Kufikiri kwamba kuwa na hela na political position ndiyo ujanja zaidi ya usomi ni ujinga kwa sababu si lazima msomi awe na hela na political position. Kuna wasomi wanataka kutatua matatizo zaidi ya kupata hela na clout. Wako poa na maisha ya kawaida tu.

Lakini pia, hao wanaoitwa wasomi wengi si wasomi, wengi wamepita shule kimagumashi tu. Wengi wamesoma ili kupata status na kazi. Huo si usomi, hiyo inaitwa "status anxiety".

Kwa hivyo na huko kwa hao wanaoitwa wasomi kuna wajinga wengi pia. Na hapo Msukuma na wenzake wanaweza kuwa na ukweli fulani kusema hawa wasomi gani mbona hatuoni matokeo ya usomi wao?
 
Tatizo letu tunapewa elimu ya kimagharibu ambayo sio asili yetu, ndo maana inanufaishaifa mataifa, hayo tu sisi [QUOTE="Magobe T, post: 50318411, member: 9922"
Kama unapinga Ina maana unataka kusema kutosoma ndilo kunakoleta maendeleo. Maendeleo ni pamoja na uboreshaji wa njia za kupunguza umaskini, maradhi na ujinga, kuboresha uchumi, njia za mawasiliano, huduma za jamii na kuleta maisha bora. Sioni mchango wa kutosoma katika haya yote. Propaganda hizi za kupuuza usoni na wasomi zilipata mwanya katika utawala uliopita na naona kwa sababu washabiki wake ni wale wasiosoma (kwa maana ya kutoelimika), naona zinajipenyeza tena. Msomi anayepuuza usoni naye hajasoma in the real sense. Usomi ninaouongelea ni hali ya kuwa enlightened. Kama mtu hakusoma (hakumaliza shule, hakwenda shule au hakupata nafasi ya kusoma) na ikatokea akapata fedha na kupata maendeleo si kwa sababu ya kutosoma. Ni kwa sababu ya kutumia maarifa na vitu alivyovipata vinavyotokana na usomi. Akiumwa na kwenda hospitali atapata huduma zinazotok
What do you mean unaposema kwamba elimu ya kiafrika ?

Unaelewa hata unachoandika wewe ?
Au ndio ninyi kufuata Mkumbo na kuandika vitu bila thinking na analysis ?

Unataka kuniambia mfano contents au modules za engineer ambaye amesoma Tanzania miaka minne ni tofauti na modules au contents za Engineer ambaye amesoma MIT ,au Edinburgh ?

Unafikiri ni nini kinachosababisha huyu graduate WA MIT au Edinburgh university anayerudi huku Tanzania wawe level moja na Engineer aliyesoma local college za humu ?
Na unafikiri ni kwanini Engineer ambaye anabaki UK au USA baada ya kugradruate five years after that anakuja na kupata patent ya kazi ya ubunifu au uvumbuzi na kuwa millionaire tofauti na huku ?
Ambapo five years after graduation engineer anakuwa mchuuzi wa chupi za kichina kariakoo au nyanya Buguruni ? Au chawa ?
Au hao akina Andrew Chenge na watu kibao si wote wamesoma hizo top colleges duniani huko na wamerudi hapa Bongo ? ,mbona hatuoni tofauti yao na hawa wasomi locals WA humu ?

Ukijibu hili swali nitajua naongea na mtu wa namna gani

Don't give me that bullshit ,kwamba mfumo wa elimu mfumo wa elimu .
Mnaandika msichokijua , contents ni zile zile za higher learning .
Tofauti inaletwa na mazingira mtu alimo na miundombinu wezeshi ya mtu kusucceed .
Wewe kwa akili yako yule Elon Musk angekuwa vile kama baada ya kugradruate University of Pretoria angeendelea kubaki South Afrika badala ya kutimkia Canada ?
 
Sio kuaminia tu watu waliopata elimu na kuwanyima haki ambao hawakubahatika kupata elimu, lakini kunawatu hawakupata elimu, ni wajuzi na wanamaarifa, ya kujenga misingi ya maisha bora ya kijamii, kuliko hata waliosoma, zaidi' kujinufaisha wao tu? haki iwe kwa wote atakayeonyesha upeo kwa mazingira fulani" aidha wasio na elimu na mwenye elimu.

Unaelewa hata unachoandika wewe ?
Au ndio ninyi kufuata Mkumbo na kuandika vitu bila thinking na analysis ?

Unataka kuniambia mfano contents au modules za engineer ambaye amesoma Tanzania miaka minne ni tofauti na modules au contents za masomo za Engineer ambaye amesoma MIT ,au Edinburgh ?

Unafikiri ni nini kinachosababisha huyu graduate WA MIT au Edinburgh university au chuo China , Australia ,Canada , Germany ,Japan nk anayerudi huku Tanzania wawe level moja na Engineer aliyesoma local college za humu ?
Na unafikiri ni kwanini Engineer ambaye anabaki USA baada ya kugradruate five years after that anakuja na kupata patent ya kazi ya ubunifu au uvumbuzi na kuwa millionaire tofauti na huku ?
Ambapo five years after graduation engineer anakuwa mchuuzi wa chupi za kichina kariakoo au nyanya Buguruni ? Au chawa ?
Au hao akina Andrew Chenge na watu kibao si wote wamesoma hizo top colleges duniani huko na wamerudi hapa Bongo ? ,mbona hatuoni tofauti yao na hawa wasomi locals WA humu ?

Ukijibu hili swali nitajua naongea na mtu wa namna gani

Don't give me that bullshit ,kwamba mfumo wa elimu mfumo wa elimu .
Mnaandika msichokijua , contents ni zile zile za higher learning .
Contents za masomo ni zile zile , contents za masomo kuhusu SCADA , motor ,au human physiology au CSS ,java programming ni zile zile vyuo dunia nzima ,hivi vitu ni universal .
Tofauti ya results za hawa university na middle college graduates inaletwa na mazingira mtu alimo na miundombinu wezeshi ya mtu kusucceed katika ambitions zake .
Wewe kwa akili yako yule Elon Musk angekuwa vile alivyo leo kama baada ya kugradruate University of Pretoria angeendelea kubaki South Afrika badala ya kutimkia Canada na baadaye Marekani ?
 
Back
Top Bottom