Sio kuaminia tu watu waliopata elimu na kuwanyima haki ambao hawakubahatika kupata elimu, lakini kunawatu hawakupata elimu, ni wajuzi na wanamaarifa, ya kujenga misingi ya maisha bora ya kijamii, kuliko hata waliosoma, zaidi' kujinufaisha wao tu? haki iwe kwa wote atakayeonyesha upeo kwa mazingira fulani" aidha wasio na elimu na mwenye elimu.
Unaelewa hata unachoandika wewe ?
Au ndio ninyi kufuata Mkumbo na kuandika vitu bila thinking na analysis ?
Unataka kuniambia mfano contents au modules za engineer ambaye amesoma Tanzania miaka minne ni tofauti na modules au contents za masomo za Engineer ambaye amesoma MIT ,au Edinburgh ?
Unafikiri ni nini kinachosababisha huyu graduate WA MIT au Edinburgh university au chuo China , Australia ,Canada , Germany ,Japan nk anayerudi huku Tanzania wawe level moja na Engineer aliyesoma local college za humu ?
Na unafikiri ni kwanini Engineer ambaye anabaki USA baada ya kugradruate five years after that anakuja na kupata patent ya kazi ya ubunifu au uvumbuzi na kuwa millionaire tofauti na huku ?
Ambapo five years after graduation engineer anakuwa mchuuzi wa chupi za kichina kariakoo au nyanya Buguruni ? Au chawa ?
Au hao akina Andrew Chenge na watu kibao si wote wamesoma hizo top colleges duniani huko na wamerudi hapa Bongo ? ,mbona hatuoni tofauti yao na hawa wasomi locals WA humu ?
Ukijibu hili swali nitajua naongea na mtu wa namna gani
Don't give me that bullshit ,kwamba mfumo wa elimu mfumo wa elimu .
Mnaandika msichokijua , contents ni zile zile za higher learning .
Contents za masomo ni zile zile , contents za masomo kuhusu SCADA , motor ,au human physiology au CSS ,java programming ni zile zile vyuo dunia nzima ,hivi vitu ni universal .
Tofauti ya results za hawa university na middle college graduates inaletwa na mazingira mtu alimo na miundombinu wezeshi ya mtu kusucceed katika ambitions zake .
Wewe kwa akili yako yule Elon Musk angekuwa vile alivyo leo kama baada ya kugradruate University of Pretoria angeendelea kubaki South Afrika badala ya kutimkia Canada na baadaye Marekani ?