Tusirudie tena Makosa Kwenye mchakato wa Katiba Mpya

Asante mkuu.
 
Hapana mkuu. Ndio maana nikashauri kama hawana nia ya kuleta katiba mpya, waache kuliko kufanya maigizo.
Hapo ndipo mnakosea. Unadhani ni nani mwenye NIA hapa Tanzania ya kukuletea wewe katika sahani katiba mpya ambayo inapunguza madaraka ya Rais, inamnyanyua mwananchi na kupunguza mamlaka ya viongozi. Katiba itakayoweka usawa wa kimapato kati ya wakubwa na wadogo. Katiba itakayofanya kiongozi wa sasa ambaye alipata uongozi kwa hila; apatikani kwa matakwa ya wapiga kura. ETC

Kwa upande wangu, nitakubaliana na uundwaji wa katiba mpya IWAPO kutakuwa na katazo katika sheria kuwa mtu yeyote atakayehusika na uandaaji, utungaji na upitishwaji wa katiba mpya asigombee nafasi yoyote kwa muda wa miaka 20 including RAIS. Au asiajiriwe serikalini kwa muda wa miaka 20. Hapo tutapata katiba mpya. Zaidi ya hapo, watu watakuwa wanajitafutia ULAJI tu. Umenipata
 
Umeleta jambo zuri lakini utekelezaji wake ni mgumu. Ukisema kila aliyeshiriki kutengeneza katiba mpya asiajiriwe Wala kuteuliwa serikalini kwa miaka ishirini hiyo sheria itakuwa batili, maana itabagua baadhi ya watu. Hivyo, itapingwa mahakamani na hata bungeni haitapitishwa.

Ingawa unanipinga, ila msimamo wangu upo palepale kwamba Kama tunataka kutengeneza katiba mpya tutulie tutengeneze katiba mpya, Kama tunabahatisha tuache huo mchakato , tuendelee na ripoti za CAG na kujenga SGR.
 
Hakuna kitu kiliniboa wakati ule pale JK aliuliza Wabunge, nyie hamtaki kuwa mawaziri? Wote wakasema tunataka. Unajua rasimu ya Wariyoba ilitaka Wabunge wasiwe Mawaziri (kitu ambacho ni cha maana katika nchi). Siamini tulivyo tunaweza kutoa katiba mpya ya maana. Ngoja nifunge domo langu
 

Kweli mkuu, JK alikosea kuwauliza wabunge lile swali. Nakubaliana na wewe kwa jinsi mambo yanavyoenda nadhani Viongozi wetu hawawezi kutuletea katiba mpya iliyo Bora. Ndio maana nikashauri kama wanataka kuendeleza ujinga wao ni Bora waache Mara moja tufanye mengine, kuliko kuzungushwa kwa Jambo ambalo halina uhalisia.

Kenya walipata shida Kama hiyo ikabidi Mwenyekiti wa Tume ya Katiba wamtoe Hong Kong alikuwa anaitwa profesa Yash Pal Ghai. Nadhani waliona asimamie yeye aliyeko nje mchakato kuliko wenyeji wa Kenya.
 
Hapo unaanza kujielewa! Kwetu hatuwezi maana tunataka kushibisha matumbo yetu. Unajua kwanini ile ya Wariyoba ilikuwa nzuri, kwa vile Wariyoba hakuwa na vest interest. Alitenda kihaki lakini uliona alivyonyanyaswa.
 
Mzee wetu WARIOBA arudishwe ktk Tume Ili amalizie KAZI aliyoianza.

Rasimu alosimamia Judge WARIOBA kabla haijaitwa KATIBA pendekezwa irudi mezani,

Wananchi tupewe fursa ya kuongeza na kuiboresha Rasimu hiyo.

Baada ya hapo, tujadiliane mfumo upi mzuri wa kuwapata wajumbe wa kuingia Bunge la Katiba ambao watatoka Kila kundi bila mashinikizo Kutoka vyama vya siasa.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo, TANZANIA.

Amen
 
Dr Slaa: Katiba ya Wananchi itaandikwa na Wananchi Wenyewe
Kama lini na wapi?

Wananchi tushiriki na kutoa maoni yetu, wanasheria waandike.

Jambo hili ni muhimu mno kwa mustakabali wa nchi yetu sasa na baadaye. Sio la kisiasa au kishabiki.
 
ushindi mkubwa sana sana kwa CHADEMA hongera sana sana
 
Hapo unaanza kujielewa! Kwetu hatuwezi maana tunataka kushibisha matumbo yetu. Unajua kwanini ile ya Wariyoba ilikuwa nzuri, kwa vile Wariyoba hakuwa na vest interest. Alitenda kihaki lakini uliona alivyonyanyaswa.

Tatizo tunaendekeza uchama Sana baadala ya utaifa. Nadhani itakuwa ngumu kupata katiba mpya.
 

Kweli kabisa. Lazima tupate njia Bora ya kuwateua wajumbe wa Bunge la Katiba mpya. Mimi ningependekeza kila kundi litoe wajumbe wenye idadi sawa.
 
Ile rasimu ya Warioba ndio itajadiliwa upya na bunge la katiba au ile ya kina Sitta (Rip) itajadiliwa upya na kupigiwa kura ?

JokaKuu zitto junior Bams
 
Kweli kabisa. Lazima tupate njia Bora ya kuwateua wajumbe wa Bunge la Katiba mpya. Mimi ningependekeza kila kundi litoe wajumbe wenye idadi sawa.
Iwepo pia kamati au watu makini watakaopita wateuliwa wa makundi hayo wasijekuwa wameteuliwa kisiasa.

Kwa mfano, mfumo uliopo, ukienda kutafuta wawakilishi wa walimu Tz, utakuta mkono wa CCM,

Ukienda Kwa MACHINGA, CCM wamepenyeza viongozi wao huko, sekta ya usafirishaji CCM wameweka viongozi Kwa maslah Yao, ktk michezo ndo usiseme, ukienda Majeshi utawakuta, ukija ktk viongozi wa dini, wengi wamo kwenye payrol, waandishi wa habari ndo usiseme,nk nk nk.

In short, ukienda ktk makundi hayo na kupeak viongozi, utajikuta unakokota mapandikizi ya KIJANI bila kujua.

Ingeundwa Tume hiyo ambayo ingeenda ktk kundi moja moja na kuendesha uchaguzi na kuchambua Kwa weledi kupata watakaosimamia maslah ya nchi bila kuingiliwa na mashinikizo ya vyama vya siasa.
 
Rasimu ya Katiba ya Warioba na Ya Sitta zijadiliwe kwa pamoja na kuongeza au kupunguza mambo muhimu na bila kuathiri uwepo wa muungano hapo mtafaulu. Mengine ni mepesi ukiondoa suala la muungano tu,ukarabati wake usilenge kuleta mabadliko ya kimuundo,bora ucheze na mifumo yake.
 
Rasimu ya Katiba ya Warioba na Ya Sitta zijadiliwe kwa pamoja na kuongeza au kupunguza mambo muhimu na bila kuathiri uwepo wa muungano hapo mtafaulu. Mengine ni mepesi ukiondoa suala la muundo wa muungano tu,ukarabati wake usilenge kuleta mabadliko ya kimuundo,bora ucheze na mfumo na sera zinazoendana na uimarishaji wake. Mbinu nyingine ni kukubaliana na machache yasiyo radical baadaye makubwa yatakuja kulingana na mabadiliko ya kijamii kuliko kungangania radicalism ukakosa vyote km wakati ule.
 
Rasimu ya Warioba ilipendekeza ziwe 3 na ilionyesha njia Bora sana ya kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali.

Anyway tukijadiliana Kwa kina tutaelewana tu, idadi ya sirikali Si issue, tunataka Kodi za raia ziwarudie,

Kodi zirudi kusaidia kuwalipa posho wasio na ajira angalau waweze kujikimu, wasirudi kutegemea wazazi kama watoto.

Kodi zetu zisaidie wazee wote walipwe pension bila kujali waliajiriwa au hawakuajiriwa sirikalini maana wote walilitumikia Taifa sekta rasmi na isiyo rasmi.

Kodi zetu zisaidie matibabu yawe Bure Kwa wananchi wote. Bima Kwa wote iwezekane sababu tunalipa Kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…