Tusirudie tena Makosa Kwenye mchakato wa Katiba Mpya

M
Waziri wa katiba na sheria ameshatangaza rasmi kwamba mchakato wa katiba mpya utaanza mwezi wa Saba mwanzoni. Nilikuwa na ushauri kwamba makosa yaliyopelekea mchakato wa katiba mpya mwaka 2014 kukwama yasijirudie.

Nimeanisha makosa Kama yafuatayo:

1. Tume ya katiba ndio ipewe mamlaka ya kisheria ya kuandika rasimu ya katiba itakayojadiliwa na kupitishwa na Bunge la Katiba. Tusirudie kosa la kuliachia bunge la Katiba kuandika rasimu yake na kuitupa kapuni ile ya Tume ya Katiba.

2. Kabla ya kuanza mchakato wa katiba mpya, ningeshauri tuanze na kura ya maoni ili wananchi waamue ni mfumo gani wa muungano wanaoutaka. Je wanataka mfumo wa Unitary, Federal au confederation. Wananchi wengi wakikubali mfumo mmojawapo, basi rasimu ya Tume ya Katiba itengenezwe kwa kufuata muundo ulioamuriwa Kwenye kura ya maoni.

3. Rais asioneshe upande wake Kwenye rasimu ya katiba. Ili kosa alilifanya Mh Rais Mstaafu Kikwete. Aliposimama Kwenye bunge la Katiba na kuonesha kwamba yeye anataka katiba ya aina gani, hivyo kupelekea wajumbe wa chama chake kufuata maelekezo yake. Mwisho wa siku katiba mpya haikupatikana. Rais ajitenge kuwapelekesha wanachama wa chama chake wafuate maoni yake baadala yake awaachie Uhuru wa kujadili.

4. Tuangalie mahitaji ya Sasa na sio misismamo ya chama. Tunapoenda kuandika katiba mpya tushughulike zaidi ya matatizo yanayotukumba Leo na namna ya kuyaondoa na sio kuangalia vyama vinataka Nini. Ufisadi, maadili, Uhuru katika uchaguzi, mfumo wa kiuchumi, mamlaka ya bunge, haki jinai, sera ya kimataifa, vyombo vya ulinzi, Uhuru wa mahakama, mamlaka ya Rais, ajira, mfuko wa mapato ya gesi na mafuta, mikopo ya wanafunzi iwe Ruzuku sio mkopo, vyama vya siasa, Tume huru, shirika la Taifa la habari etc.

5. Spika au Mwenyekiti wa bunge la Katiba asitokane na chama Cha siasa. Ateuliwe jaji wa mahakama ya Rufaa ambaye atasimamia bila upendeleo bunge la katiba. Tukiweka watu wa vyama sampuli ya Tulia Akson tutapata bunge la hovyo na litakalo toa rasimu ya hovyo na ya kichama.

NB:Tukirudia makosa hatutapata katiba mpya kamwe, na Kama hatupo tayari kuandika katiba mpya ni Bora kuacha kuliko kufanya maigizo.
Mchakato ni mchakato nafikiri utamalizika mwezi mmoja kabla Samia kumaliza miaka yake 10!
 
What's is the point ya bunge la katiba 'kujadili' ikiwa hawawezi kufanya maboresho yoyote kwenye hiyo rasimu?

Hilo la muungano ndio hata msithubutu, mtakuwa wajinga wakubwa kama hamkujifunza kwenye ile rasimu iliyokwama.

Hakuna taifa la kipumbavu duniani linalo hatarisha uhai wake kwa kura za maoni! Hilo la muundo wa muungano achaneni nalo.
Zanzibar iulizwe aina ya Muungano wanoutaka ,Na
Tanganyika iulizwe aina ya Muungano wanaoutaka.
Kisha tuoanishe maoni yapande mbili katika Tume husika ili tupate Mchujo wa maoni ya Muundo wa Mungano.
Ikiwa Basi naiwe basi,Maana Zanzibar inahitaji More Sovereghnity ili iweze kuendesha Maisha ya Watu wake.
 
Kwa upande wangu, nitakubaliana na uundwaji wa katiba mpya IWAPO kutakuwa na katazo katika sheria kuwa mtu yeyote atakayehusika na uandaaji, utungaji na upitishwaji wa katiba mpya asigombee nafasi yoyote kwa muda wa miaka 20 including RAIS. Au asiajiriwe serikalini kwa muda wa miaka 20. Hapo tutapata katiba mpya. Zaidi ya hapo, watu watakuwa wanajitafutia ULAJI tu. Umenipata
Kwa sharti hili WAZEE waliostaafu na wenye hekima pekeyao ndio watakaoshiriki kututengenezea Katiba kitu amnbacho kitakuwa na uhalisia na uadilifu. NADHANI WANASHERIA NA MAJAJI NI LAZIMA WAWE NDIO WASIMAMIZI WAKUU WAKIWEMO VIONGOZI WA DINI WENYE ELIMU ZAO, SIO AKINA JONGO WANAOLIA BUNGENI KUMLILIA NYERERE
 
Zanzibar iulizwe aina ya Muungano wanoutaka ,Na
Tanganyika iulizwe aina ya Muungano wanaoutaka.
Kisha tuoanishe maoni yapande mbili katika Tume husika ili tupate Mchujo wa maoni ya Muundo wa Mungano.
Ikiwa Basi naiwe basi,Maana Zanzibar inahitaji More Sovereghnity ili iweze kuendesha Maisha ya Watu wake.
Mmh, hilo litakuwa gumu, hata watu wa Catalonia wanataka uhuru, lakini huwezi kuusikia umoja wa Ulaya wanawaapia Spain wawaulize wakatalonia.

Uhai wa nchi huwa unalindwa kwa nguvu zote. Serikali moja ndio suluhisho.
 
Lakini na majaji pamoja na hao viongozi wa dini wasiwe na uwezekano wa kugombea nyazifa za kisiasa. Mfano Gwajima etc
 
Mmh, hilo litakuwa gumu, hata watu wa Catalonia wanataka uhuru, lakini huwezi kuusikia umoja wa Ulaya wanawaapia Spain wawaulize wakatalonia.

Uhai wa nchi huwa unalindwa kwa nguvu zote. Serikali moja ndio suluhisho.
Zanzibar haidai Uhuru kutoka Tanganyka, Zanzibar Tayari ilikuwa Nchi Huru na ni mwanachama wa UN ,
Hata kesho tukiamua Kwenda UN na kusema Tunakalia Kiti chetu hakuna wa kutuzuwia, Muungano ulkuwa ni wa Hiari tuu.
Ndo maana Tanganyika Wanabembeleza sana ili Tanzania Ibakie kama Ilivyo.
Kimsingi Zanzibar Inaona Inaakndamizwa ndani ya Unganiko hili, na ikibidi ,kama hakuna jinsi tunatagaza Kujitowa.
Hili lko wazi.
Maeneleo ya Zanzibar yamekwama kwa kikwazo cha Muungano.
Tunataka Kuchimba Mafuta na Gesi , Muungano umetuwekea Mguu,
Bahari yetu kuu hatuna Mmlaka ya kuitumia,
Hatuna Mmlaka ya kuita Makampuni ya Nje kuja kuwekeza Zanzibar bila ya kibali cha Muungano ambao umeshikiliwa na Tanganyika.
Tumechoka Mno.
Hat Mzee wa Uchumi wa Buluu amegonga Mwamba.
 
Iwepo pia kamati au watu makini watakaopita wateuliwa wa makundi hayo wasijekuwa wameteuliwa kisiasa.

Kwa mfano, mfumo uliopo, ukienda kutafuta wawakilishi wa walimu Tz, utakuta mkono wa CCM,

Ukienda Kwa MACHINGA, CCM wamepenyeza viongozi wao huko, sekta ya usafirishaji CCM wameweka viongozi Kwa maslah Yao, ktk michezo ndo usiseme, ukienda Majeshi utawakuta, ukija ktk viongozi wa dini, wengi wamo kwenye payrol, waandishi wa habari ndo usiseme,nk nk nk.

In short, ukienda ktk makundi hayo na kupeak viongozi, utajikuta unakokota mapandikizi ya KIJANI bila kujua.

Ingeundwa Tume hiyo ambayo ingeenda ktk kundi moja moja na kuendesha uchaguzi na kuchambua Kwa weledi kupata watakaosimamia maslah ya nchi bila kuingiliwa na mashinikizo ya vyama vya siasa.

Shida ni CCM kutaka kuhodhi mchakato wa Katiba. Wataharibu Kama walivyofanya mchakato uliopita.
 
Rasimu ya Warioba ilipendekeza ziwe 3 na ilionyesha njia Bora sana ya kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali.

Anyway tukijadiliana Kwa kina tutaelewana tu, idadi ya sirikali Si issue, tunataka Kodi za raia ziwarudie,

Kodi zirudi kusaidia kuwalipa posho wasio na ajira angalau waweze kujikimu, wasirudi kutegemea wazazi kama watoto.

Kodi zetu zisaidie wazee wote walipwe pension bila kujali waliajiriwa au hawakuajiriwa sirikalini maana wote walilitumikia Taifa sekta rasmi na isiyo rasmi.

Kodi zetu zisaidie matibabu yawe Bure Kwa wananchi wote. Bima Kwa wote iwezekane sababu tunalipa Kodi.

Mapendekezo mazuri mkuu, shida Viongozi wetu hawana macho ya mbele.
 
Rasimu ya Katiba ya Warioba na Ya Sitta zijadiliwe kwa pamoja na kuongeza au kupunguza mambo muhimu na bila kuathiri uwepo wa muungano hapo mtafaulu. Mengine ni mepesi ukiondoa suala la muungano tu,ukarabati wake usilenge kuleta mabadliko ya kimuundo,bora ucheze na mifumo yake.

Rasimu ya Warioba na Sitta ni mbili tofauti haziwezi kujadiliwa kwa pamoja. Moja ni Federal na nyingine sui generis.
 
Zanzibar haidai Uhuru kutoka Tanganyka, Zanzibar Tayari ilikuwa Nchi Huru na ni mwanachama wa UN ,
Hata kesho tukiamua Kwenda UN na kusema Tunakalia Kiti chetu hakuna wa kutuzuwia, Muungano ulkuwa ni wa Hiari tuu.
Ndo maana Tanganyika Wanabembeleza sana ili Tanzania Ibakie kama Ilivyo.
Kimsingi Zanzibar Inaona Inaakndamizwa ndani ya Unganiko hili, na ikibidi ,kama hakuna jinsi tunatagaza Kujitowa.
Hili lko wazi.
Maeneleo ya Zanzibar yamekwama kwa kikwazo cha Muungano.
Tunataka Kuchimba Mafuta na Gesi , Muungano umetuwekea Mguu,
Bahari yetu kuu hatuna Mmlaka ya kuitumia,
Hatuna Mmlaka ya kuita Makampuni ya Nje kuja kuwekeza Zanzibar bila ya kibali cha Muungano ambao umeshikiliwa na Tanganyika.
Tumechoka Mno.
Hat Mzee wa Uchumi wa Buluu amegonga Mwamba.
Na hili watu wengi wanalipuuza. Kwamba Zanzibar ilikuwa nchi huru yenye kiti umoja wa mataifa. Ndio maana nikashauri Kama tinataka katiba Bora tuanze na kura za maoni kuhusu muundo wa muungano.
 
M

Mchakato ni mchakato nafikiri utamalizika mwezi mmoja kabla Samia kumaliza miaka yake 10!
Haina tatizo iwapo makosa ya jk hayatajirudia. Tunataka katiba Bora sio mchakato wa kinafiki.
 
Zanzibar iulizwe aina ya Muungano wanoutaka ,Na
Tanganyika iulizwe aina ya Muungano wanaoutaka.
Kisha tuoanishe maoni yapande mbili katika Tume husika ili tupate Mchujo wa maoni ya Muundo wa Mungano.
Ikiwa Basi naiwe basi,Maana Zanzibar inahitaji More Sovereghnity ili iweze kuendesha Maisha ya Watu wake.
Hilo ndio suluhisho. Tusije tukaishia Kama muungank wa Yugoslavia. Tukubaliane Kama taifa muundo Bora wa muungano, tukishakubaliana Basi twende Kwenye kutengeneza katiba yenye mwelekeo wa muundo wa muungano.
 
Kwa sharti hili WAZEE waliostaafu na wenye hekima pekeyao ndio watakaoshiriki kututengenezea Katiba kitu amnbacho kitakuwa na uhalisia na uadilifu. NADHANI WANASHERIA NA MAJAJI NI LAZIMA WAWE NDIO WASIMAMIZI WAKUU WAKIWEMO VIONGOZI WA DINI WENYE ELIMU ZAO, SIO AKINA JONGO WANAOLIA BUNGENI KUMLILIA NYERERE

Kweli kabisa
 
Waziri wa katiba na sheria ameshatangaza rasmi kwamba mchakato wa katiba mpya utaanza mwezi wa Saba mwanzoni. Nilikuwa na ushauri kwamba makosa yaliyopelekea mchakato wa katiba mpya mwaka 2014 kukwama yasijirudie.

Nimeanisha makosa Kama yafuatayo:

1. Tume ya katiba ndio ipewe mamlaka ya kisheria ya kuandika rasimu ya katiba itakayojadiliwa na kupitishwa na Bunge la Katiba. Tusirudie kosa la kuliachia bunge la Katiba kuandika rasimu yake na kuitupa kapuni ile ya Tume ya Katiba.

2. Kabla ya kuanza mchakato wa katiba mpya, ningeshauri tuanze na kura ya maoni ili wananchi waamue ni mfumo gani wa muungano wanaoutaka. Je wanataka mfumo wa Unitary, Federal au confederation. Wananchi wengi wakikubali mfumo mmojawapo, basi rasimu ya Tume ya Katiba itengenezwe kwa kufuata muundo ulioamuriwa Kwenye kura ya maoni.

3. Rais asioneshe upande wake Kwenye rasimu ya katiba. Ili kosa alilifanya Mh Rais Mstaafu Kikwete. Aliposimama Kwenye bunge la Katiba na kuonesha kwamba yeye anataka katiba ya aina gani, hivyo kupelekea wajumbe wa chama chake kufuata maelekezo yake. Mwisho wa siku katiba mpya haikupatikana. Rais ajitenge kuwapelekesha wanachama wa chama chake wafuate maoni yake baadala yake awaachie Uhuru wa kujadili.

4. Tuangalie mahitaji ya Sasa na sio misismamo ya chama. Tunapoenda kuandika katiba mpya tushughulike zaidi ya matatizo yanayotukumba Leo na namna ya kuyaondoa na sio kuangalia vyama vinataka Nini. Ufisadi, maadili, Uhuru katika uchaguzi, mfumo wa kiuchumi, mamlaka ya bunge, haki jinai, sera ya kimataifa, vyombo vya ulinzi, Uhuru wa mahakama, mamlaka ya Rais, ajira, mfuko wa mapato ya gesi na mafuta, mikopo ya wanafunzi iwe Ruzuku sio mkopo, vyama vya siasa, Tume huru, shirika la Taifa la habari etc.

5. Spika au Mwenyekiti wa bunge la Katiba asitokane na chama Cha siasa. Ateuliwe jaji wa mahakama ya Rufaa ambaye atasimamia bila upendeleo bunge la katiba. Tukiweka watu wa vyama sampuli ya Tulia Akson tutapata bunge la hovyo na litakalo toa rasimu ya hovyo na ya kichama.

NB:Tukirudia makosa hatutapata katiba mpya kamwe, na Kama hatupo tayari kuandika katiba mpya ni Bora kuacha kuliko kufanya maigizo.
Umeongea pointi tupu. Hongera
 
Hizo pesa za kugharamia mchakato mpya wa kukusanya maoni na kuandaa Rasimu nani anatoa ?......ile ya Warioba ina tatizo gani mpaka itoswe ?.....
Haina tatizo ila baada ya magufuli hata wanaccm wanaamini Rasimu ya Warioba haitoshi. Maana tusije pata magufuli mwingine.
 
Aaah!..jamaa alikuwa na madhaifu yake kama binadamu wengine, kuendelea kumfanya reference ya ubaya kila sehemu sio sawa.......

kumbuka bado wanaweza kuja wengine msiowajua mnaweza kusema afadhali yeye tena.
 
Back
Top Bottom