Siku zote mapambano ya ukombozi huanza usiku wa manane. Na ndiyo maana madikteta yote yakiona mambo yanawaendea vibaya, hatua ya kwanza huwa ni kuwazuia watu kutembea usiku.
Uhuru wa Tanganyika ulitangazwa usiku wa tarehe 8 kuamkia tarehe 9 December 1961. Mapinduzi ya Zanzibar yalikamilika usiku wa kuamkia tarehe 12. Ushindi wa Kristo dhidi ya mauti ya mwili ulipatikana usiku wa kuamkia siku ya kwanza ya juma. Hii inadhihirisha kuwa usiku umebarikiwa na kufanywa ni muda sahihi wa mapambano ya kuutafuta ushindi.
Watanzania wanaishi katika laana kubwa usiyoweza kuelezeka, watu wanatekwa na kuuawa kama vile uhai wao hauna thamani. Leo hii uhai wa mbwa aishiye Ulaya una thamani kuliko uhai wa mtanzania. Nchi ya Tanzania imefanywa kuwa mali ya kikundi cha wahuni, na wengine wote ni kama wageni wasio na thamani. Chaguzi zimekuwa maagizo ya kuonesha watanzania wasivyo na akili. Mahakama zimekuwa vyombo vya kikundi cha wahuni kuwaonea wananchi. Rasilimali za nchi zimefanywa kuwa za kikundi cha watu ambacho kinaweza kumgawia yeyote wanayemtaka, na anayehoji anatekwa na kuuawa. Kikundi cha wahuni wachache kinaamua nani awe kiongozi wa nchi, na nani asiwe.
Sasa ni wakati wa kuamka na kuwaambia hawa wahuni kuwa Tanganyika ni ya Watanganyika wote, wananchi ndiyo wenye mamlaka ya kuamua nani awe kiongozi wao, rasilimali za nchi ni mali ya umma, na zipo kwaajili ya kuunufaisha umma wa Watanganyika kwanza kabla ya mwingine yeyote.
Wananchi waliofanywa hawana akili, ni wakati wa kuwaonesha wahuni kuwa wao wahuni kwa kuuabudu uhuni, ndiyo hawana akili.
Tuufanye usiku wa tarehe 28, kuwa usiku mtakatifu. Tuwaambie wahuni kwa vitendo kuwa hatuhitaji vituo vya kuhalalishia ushetani wao, wala ofisi za wahuni, kwa sababu hatutaki nchi ya wahuni. Yeyote anayeungana na wahuni dhidi ya wananchi, naye ni mhuni, adhibitiwe kama watakavyodhibitiwa wahuni.
Wakati wa mapambano haya, umoja na upendo wa kweli miongoni mwa wote wenye dhamira njema kwa Taifa letu, ni jambo muhimu sana. Hapa siyo suala la vyama bali ni uzalendo dhidi ya wahuni.
Mungu Akiwa Upande wetu, nani atazuia ukombozi wetu! Hakika hayupo. Tunafanyiwa ushetani wa ajabu ma wahuni kwa kuwa tumekuwa wavivu wa kupeleka ujumbe muhimu kwao kuwa hili ni Taifa letu sote. kila jambo lina wakati wake, na huu ndiyo wakati sahihi.