Tusishobokee Kingereza, ni moja katika lugha mbovu duniani

Kiingereza ndio Engine ya biashara duniani kama USD tu..unaweza kuiponda hiyo lugha ukiwa unalima zako matikiti msata ila ukiwa mtu wa safari na kazi zako zinahitaji utoe maelezo huko unakokwenda utaelewa umuhimu wa Lugha ya Malkia..
 
Kwahiyo madam huko ulipoenda mlikuwa mnaongea kiswahili?? Kwann hukuona umuhimu wa kingireza hapo.
Kiingireza ni muhimu katika dunia ya Leo mana kiswahili hakivuki mipaka
 
Shida ni siku nchi inapata mtu wa hisia kama wewe kuongoza lazima Kila kitu kitaharibika
 
atakuwa na kasoro ya matamshi (phoenetic) au webgine huita "accent",kwa sabau Kingereza hakina uasili.

Lugha kubwa duniani zote zina lafudhi za kubadilika iwe Kifaransa, kiarabu, kispanyola, kiingereza, kiSwahili n.k

Lugha zote kubwa duniani ni muhimu sana ikiwemo Kiingereza.

Waliosoma enzi za Tanganyika, na baadaye Tanzania ya 1970s, 1980s wasitake kuwaambia vizazi vya sasa kuwa Kiingereza kibezwe na kuachwa.

Rwanda ilikuwa inaongea French hadi miaka ya 1990s lakini wamestuka na kukitilia mkazo kiingereza pia kwa kuelewa umuhimu wake katika dunia kijiji (globalisation)

Huku pia lugha yao mama kama kinyarwanda inatiliwa mkazo, bila kusahau pia kutokana na historia ya kiSwahili eneo la Afrika ya Mashariki na Maziwa Kuu lugha ya kiswahili inatumika .

Tanzania tuachane na dhana ya kupuuza umuhimu wa kujifunza na kufundishwa lugha za kigeni kama Kiingereza na pia kwa nyongeza kiarabu, kifaransa n.k ili kuweza kwenda na dunia hii ya kisasa.
 
Siyo kweli.

Kingereza hakina asili.

Kiarabu hakibadiliki lafdhi yake, usichanganye lafdhi za watu na lafdhi ya lugha. Kiarabu kinavyoandikwa ndivyo kinavyotamkwa, popote utapo kuwepo.

Kiarabu tunafundishwa madrasa Tanzania ndicho kile kile anachofundishwa madrasa Mchina kwao China. Na hata tukienda kusali China au iwe umatumbini, Kiarabu kinabaki kuwa ni kile kile na lafdhi ile ile.

Kiswahili pia, kinabaki na lafdhi ile ile labda waje waliosomea ujimga kubadili mahari wakaiita mahali na mahali wakapaita mahari.

Kigereza ni tofauti kabisa, hakitamkwi kinavyoandikwa. Mfano inaandikwa "women" inatamkwa "wimen". Inaandikwa "laugh" inatamkwa "laf".

Upo hapo ulipo?
 
Wamarekani wenyewe unakuta wanajua Eng Spanish etc
Mbongo kakumbatia kiswahili tuu
Bongo jina kubwa lkn hamna kitu - Prof J
 
Wamarekani wenyewe unakuta wanajua Eng Spanish etc
Mbongo kakumbatia kiswahili tuu
Bongo jina kubwa lkn hamna kitu - Prof J
Wapo Wamarekani wenye asili ya Uhispania wengi tu.

Tanzania tunatakiwa tukumbatie Kiswahili, tusijidhalilishe na lugha ya kijinga, Kingereza. Inatudunisha kimawazo.
 
wewe unakijua, unataka wengine wasikijue
acha roho mbaya kama ya mtume
 
Sizitaki mbichi hizi....Sungura akajisemea!
 
Wapo Wamarekani wenye asili ya soain wengi tu.

Tanzania tunatakiwa tukumbatie Kiswahili, tusijidhalilishe na lugha ya kijinga, Kingereza. Inatudunisha kimawazo.
Labda kwa ambae anataka kuishia tandale
 
Siyo kweli.
Modern Standard Arabic (MSA) is a modernized form of Classical Arabic, the language of prayer and recitation throughout the Islamic world. Standard Arabic is the language of literature and education in most Arabic countries. Educated people throughout North Africa and the Arabian Peninsula have good to excellent command of Standard Arabic besides their native Arabic dialect. It is estimated that some 165,000,000 people throughout the Islamic world have some knowledge of Standard Arabic. Standard Arabic is not acquired as a mother tongue, but rather it is learned as a second language at school and through exposure to formal broadcast programs (such as the daily news), religious practice, and print media. The media in which Standard Arabic is not as frequently used as the spoken Arabic dialects are in song, film, and the theater.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…