Tusishupaze shingo tukaruhusu raia wetu wapewe ukimbizi Mataifa ya nje kwa sababu za kiusalama na siasa

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Tanzania ni nchi inayoamini katika Demokrasia. Demokrasia ni mfumo unaoambatana na Uhuru wa kusema, Uhuru huo wa kusema umewekewa mipaka na sheria pamoja na katiba na hakuna mtu mwingine mwenye mamlaka ya kumhukumu aliyesema kwamba ametenda kosa bali nafasi ya kuhukumu imeachwa mahakama.

Upande wa pili Demokrasia inaambatana na Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa. Katika kuchagua na kuchaguliwa pamewekwa neno haki, maana yake uchaguliwe kwa haki na pale ambapo ujachaguliwa kwa haki basi unayo haki ya kuhoji maamuzi yaliyotolewa kinyume cha sheria. Kuhoji huko nako kumeachiwa mahakama na si mtu mwingine.

Kitu cha tatu chini ya Demokrasia ni utawala wa sheria, maana yake kila Jambo linalofanywa na viongozi pamoja na wananchi lazima lizingatie sheria zilizowekwa. Lazima Jambo ilo lisimamiwe kwa uwazi na sheria zinazosimamiwa zijulikane kwa anayehukumiwa kwazo.

Pamoja na msingi huo, lipo tatizo kubwa linalotukumba na ambalo litaligharimu taifa lisiposema. Taifa limeanza kubadili Uhuru wa kusema, kusikilizwa, kuchaguliwa na kuchagua pamoja na misingi yote ya kidemokrasia na sasa limeingia katika misingi ambayo naweza iweka katika makundi matatu.

1. Ndani ya Tanzania unao Uhuru wakusema lakini hauna Uhuru baada ya kusema.
- Anayetafsiri ulichosema ni Cha kweli au si Cha kweli, Ni kosa au si kosa nk si mahakama Tena bali Ni wale waliokuzunguka wakiwemo waajiriwa wa wananchi. Hii siyo afya kwa Taifa, si afya kwa utawala Bora na si afya kwa Demokrasia yetu. Idadi ya watu walio ndani baada ya kusema inaongezeka kwa kasi sana jambo ambalo linawafanya watu waone hawana Uhuru ndani hivyo Bora wakaishi ukimbizini. Tukemeee.

2. Upo Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa lakini hakuna Uhuru wa kujua nafasi ya kura yako kwenye kuchagua na kuchaguliwa.
- Kama Uhuru huu ukipokwa upo uwezekano wa kuwa na viongozi wasiotokana na wananchi, upo uwezekano wakuwa na viongozi wasiofaa, upo uwezekano ukawa na viongozi ambao awawezi kushirikiana na wananchi kupanga na kuamua juu ya vipao mbele vyao. Tuamue Sasa kuukataa Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa au kupoteza kabisa. Lakini madhara ya kukosekana kwa Uhuru huu nikutengeneza mpasuko wa kisiasa na walioshindwa wanaweza amua kwenda kuusaka ukimbizi nje ya nchi na endapo wataupata Basi litakua doa kubwa sana kwa Taifa.

3. Upo Uhuru wa kuhojiwa lakini hakuna Uhuru wa kuhojiwa.
- Binadamu kwa utashi tu ni mdadisi, akinyimwa haki ya kuhoji atatamani aondoke kwenye jamii anayoishi akatafute maisha sehemu atakayopewa nafasi yakupumua angalau kwa kuhoji kidogo. Kuhoji ni chakula kikuu cha ubongo, Uhuru huu ukipokwa uzaliwa Taifa mfu.
 
“Dictatorships are like weeds, they grow almost everywhere, they don’t need a lot of conditions to survive. Democracy is like a rare flower that demands lots of preconditions in order to succeed” - Prof Yuval Harari
 
Mafi
Kila mtu ana hofu na huzuni, hata walio upande wake wote hawaelewi hatima yao na wengi tumetiwa kamba shingoni tukisubiri ivutwe tunyongwe hiyo ndiyo sehemu ya kuminywa kwa uhuru wa mtu mmoja mmoja kuongea.
Mafisadi mko kazini, mitano bado mtaongea saana.
Ila ipo siku pumzi ya uongo itaisha mtatulia tu.
 
Tanzania ni nchi inayoamini katika Demokrasia. Demokrasia ni mfumo unaoambatana na Uhuru wa kusema, Uhuru huo wa kusema umewekewa mipaka na sheria pamoja na katiba na hakuna mtu mwingine mwenye mamlaka ya kumhukumu aliyesema kwamba ametenda kosa bali nafasi ya kuhukumu imeachwa mahakama.

Upande wa pili Demokrasia inaambatana na Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa. Katika kuchagua na kuchaguliwa pamewekwa neno haki, maana yake uchaguliwe kwa haki na pale ambapo ujachaguliwa kwa haki basi unayo haki ya kuhoji maamuzi yaliyotolewa kinyume cha sheria. Kuhoji huko nako kumeachiwa mahakama na si mtu mwingine.

Kitu cha tatu chini ya Demokrasia ni utawala wa sheria, maana yake kila Jambo linalofanywa na viongozi pamoja na wananchi lazima lizingatie sheria zilizowekwa. Lazima Jambo ilo lisimamiwe kwa uwazi na sheria zinazosimamiwa zijulikane kwa anayehukumiwa kwazo.

Pamoja na msingi huo, lipo tatizo kubwa linalotukumba na ambalo litaligharimu taifa lisiposema. Taifa limeanza kubadili Uhuru wa kusema, kusikilizwa, kuchaguliwa na kuchagua pamoja na misingi yote ya kidemokrasia na sasa limeingia katika misingi ambayo naweza iweka katika makundi matatu.

1. Ndani ya Tanzania unao Uhuru wakusema lakini hauna Uhuru baada ya kusema.
- Anayetafsiri ulichosema ni Cha kweli au si Cha kweli, Ni kosa au si kosa nk si mahakama Tena bali Ni wale waliokuzunguka wakiwemo waajiriwa wa wananchi. Hii siyo afya kwa Taifa, si afya kwa utawala Bora na si afya kwa Demokrasia yetu. Idadi ya watu walio ndani baada ya kusema inaongezeka kwa kasi sana jambo ambalo linawafanya watu waone hawana Uhuru ndani hivyo Bora wakaishi ukimbizini. Tukemeee.

2. Upo Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa lakini hakuna Uhuru wa kujua nafasi ya kura yako kwenye kuchagua na kuchaguliwa.
- Kama Uhuru huu ukipokwa upo uwezekano wa kuwa na viongozi wasiotokana na wananchi, upo uwezekano wakuwa na viongozi wasiofaa, upo uwezekano ukawa na viongozi ambao awawezi kushirikiana na wananchi kupanga na kuamua juu ya vipao mbele vyao. Tuamue Sasa kuukataa Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa au kupoteza kabisa. Lakini madhara ya kukosekana kwa Uhuru huu nikutengeneza mpasuko wa kisiasa na walioshindwa wanaweza amua kwenda kuusaka ukimbizi nje ya nchi na endapo wataupata Basi litakua doa kubwa sana kwa Taifa.

3. Upo Uhuru wa kuhojiwa lakini hakuna Uhuru wa kuhojiwa.
- Binadamu kwa utashi tu ni mdadisi, akinyimwa haki ya kuhoji atatamani aondoke kwenye jamii anayoishi akatafute maisha sehemu atakayopewa nafasi yakupumua angalau kwa kuhoji kidogo. Kuhoji ni chakula kikuu cha ubongo, Uhuru huu ukipokwa uzaliwa Taifa mfu.
Sawa
 
Kuna mtu anaweza kusimama hadharani na kumkosoa Magufuli hadharani bila kuwa na mashaka na maisha yake?
Nakumbuka enzi za jk watu wanamjadiri jk hata kwenye mabasi. Wanamsema vibaya hata matusi. Baadae unamkuta jk kwenye zile speech zake mwisho wa mwezi anatabasam na hana noma.

Hivi sasa ukijaribu kukosoa hadharani mashabiki wa mkubwa wanakukamata kama mwizi wanakupeleka kutibiwa selo

[emoji1787]
 
“Dictatorships are like weeds, they grow almost everywhere, they don’t need a lot of conditions to survive. Democracy is like a rare flower that demands lots of preconditions in order to succeed” - Prof Yuval Harari
It is sad, mtu anaweza kuitetea DEMOKRASIA pasi kujua maana yake kamili.
 
Nakumbuka enzi za jk watu wanamjadiri jk hata kwenye mabasi. Wanamsema vibaya hata matusi. Baadae unamkuta jk kwenye zile speech zake mwisho wa mwezi anatabasam na hana noma.

Hivi sasa ukijaribu kukosoa hadharani mashabiki wa mkubwa wanakukamata kama mwizi wanakupeleka kutibiwa selo

[emoji1787]
Kwa hiyo uko selo gani sasa hivi?
 
Nakumbuka enzi za jk watu wanamjadiri jk hata kwenye mabasi. Wanamsema vibaya hata matusi. Baadae unamkuta jk kwenye zile speech zake mwisho wa mwezi anatabasam na hana noma.

Hivi sasa ukijaribu kukosoa hadharani mashabiki wa mkubwa wanakukamata kama mwizi wanakupeleka kutibiwa selo

[emoji1787]
Daah,umenikumbusha mbali sana!Huyu mtu amekuja kutuharibia nchi!Ana roho mbaya kama shetani!
 
Labda nyinyi mafisadi uliokuwa mmezoea kuiba mali ya taifa hili. Mpaka mnyooke ndiyo Rais Magufuli atastaafu urais!!
 
Back
Top Bottom