Habari za mchana huu.
Naomba nizungumzie jambo moja lisilo zuri leo.
Kumekuwa na tabia ya kusimanga wanawake ambao hawajaolewa na kuwafanya wajione hawafai. Watanzania wenzangu hii tabia sio nzuri. Naomba tusiwasimange wanawake ambao hawajaolewa kwa maneno ya kejeli au dharau.
Kufanya hivyo kutawafanya wajione wana hatia kwa wao kuchelewa kuolewa na kunaweza kuwapelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi yaani kuolewa na mtu asiye sahihi kisa tu kupunguza masimango.
Tusiwasukume dada zetu, wadogo zetu au mabinti zetu kufanya maamuzi mabaya na ya haraka haraka eti kisa tu wanapaswa kuolewa. Hili suala sio tu linawaathiri mabinti zetu kisaikolojia lakini pia linaweza kuwasababishia kuharibu maisha yao kwa kufunga ndoa na watu wasio sahihi (violent person au asiejali familia) kwa sababu ya kuharakisha ndoa.
Wewe mwanamke ambao bado hujaolewa. Ndoa ni maamuzi ya maisha na ni maamuzi BINAFSI kuyafanya. Hakuna umri ambao si sahihi kuolewa. Huna haja ya kufanya maamuzi haya kwa sababu tu ya maneno wanayozungumza majirani zako.
Nimalize kwa kushauri kuwa, kutokuolewa kusikufanye ukataka kumkosea Mungu kwa kufanya ngono kabla ya ndoa. Mwanamke JITUNZE. Njia sahihi ya kutosheleza mahitaji ya kimwili kati ya mwanamke na mwanaume ni kupitia ndoa tu katika njia inayofaa na inayoendana na asili ya mwanadamu.