Tusiwatupie lawama Walimu wa Vyuo Vikuu. Mitihani ndio kipimo cha uelewa na namna mwanafunzi ataisadia jamii na Taifa lake

Tusiwatupie lawama Walimu wa Vyuo Vikuu. Mitihani ndio kipimo cha uelewa na namna mwanafunzi ataisadia jamii na Taifa lake

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Taifa linapokuwa na wahitimu wa chuo kikuu ambao hata wakikaa mitaani ni kama hawajamaliza form four ni aibu kwa taifa.

Ni lazima wapimwe kwa mitihani ambayo ina vigezo vya kimataifa.

Bahati nzuri dunia nzima masomo ni yaleyale tu.

Sasa kama vyuo vitawalegezea wanafunzi ili waonekane wamefaulu wakati hawajaiva ni aibu kubwa.

Ndio maana sasa hivi ni aibu kwa graduates wengi wa vyuo vikuu. Aibu kubwa.
 
Kwa nini walimu wa vyuo vikuu wasitupiwe lawama, wakati mitaala yao ni useless?
 
Hivi hao waliosoma vizuri siku za nyuma ana lipi jipya? Mbona hawana cha maana? Huyo Ndumbaro nje ya siasa amewahi hata kujulikana?
 
Wakati ule wa mwaka 2012 alama za ufaulu zikifanyiwa masihara kwa mujibu wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi watu wengi walikubaliana na upuuzi ule kwa mikono miwili. Watu wachache mno ndiyo walijitokeza na kuupinga utaratibu ule.

Kutokana na taarifa rasmi ya serikali kupitia wizara iliyokuwa yenye dhamana, iliuona utaratibu huo kuwa ni mzuri wenye mantiki katika upangaji wa alama za ufaulu kwa kidato cha nne na sita.

Hakuna aliyesumbuka kuwa katika siku zijazo wale waliopita katika viwango hivi vya ufaulu watakuja kutakiwa kufanya mitihani mingine katika fani zingine za kitaalamu. Haya sasa ndiyo matokeo ya kubeba watu kwenye mbeleko ili kutafuta kiki za kisiasa.

Vigezo ni lazima vizingatiwe katika mitihani ya kupima weledi ya watahiniwa katika "body of knowledge"
Utaratibu huu ni tofauti kabisa na ule uliopo katika kutafuta ufaulu katika shule na vyuo watahiniwa hao walipotoka, lengo la kufanya hivyo likiwa ni kulinda hadhi ya "profession" husika.

Hayo ndiyo matokeo ya uamuzi ule wa 2012. Watahiniwa wa namna hii ni lazima watakutana na mazingira magumu kama haya.
Screenshot_20221013-062157.jpg
 
Tatizo ni kwamba, kila taahira aliyeshindwa kushika tebo ya kuzidisha kwa kichwa anaona sehemu pekee ya kukimbilia ni kwenye sheria.
Law school andeleeni ku maintain standard hiyo hiyo mliyo I set
 
Taifa linapokuwa na wahitimu wa chuo kikuu ambao hata wakikaa mitaani ni kama hawajamaliza form four ni aibu kwa taifa.

Ni lazima wapimwe kwa mitihani ambayo ina vigezo vya kimataifa.

Bahati nzuri dunia nzima masomo ni yaleyale tu.

Sasa kama vyuo vitawalegezea wanafunzi ili waonekane wamefaulu wakati hawajaiva ni aibu kubwa.

Ndio maana sasa hivi ni aibu kwa graduates wengi wa vyuo vikuu. Aibu kubwa.
yaani kuanzia darasa ,la saba,form 4, na form six,nikupanua goli,ili ufauru uwe mzuri,bila kuangalia hao wahitimu,uje utegemee kuwatengeneza wakiwa vyuoni?hilo ni gumu,angalia kipindi cha nyuma angalau kulipo kuwa na ubora wa elimu kuanzia chini,hata huko juu kulitoa wahitimu wenye ubora.
 
Back
Top Bottom