Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Tangu tupate uhuru wa bendera kutoka kwa Ufalme wa Uingereza, Tanzania tumekuwa tukiomba msaada wa kugharimia Chaguzi Kuu zote kutoka nchi marafiki na jumuia za kimataifa. Lakini uchaguzi wa mwaka huu imekuwa tofauti kabisa Serikali iliamua kugharimia, kitendo ambacho haiingii akilini kuwa ni cha busara.
Fedha ambayo imetumika kugharimia Uchaguzi huu ingeweza kutumika kugharimia miradi mingine ya maendeleo ili kuwapunguzia wananchi makali ya maisha na kujenga uchumi wa nchi.
Kwa jinsi ambavyo uchaguzi umeendeshwa na matokeo yake yanayoendelea kutangazwa, kwa vyo vyote vile Serikali ingepata lawama kubwa sana. Na kwa kuwa Serikali ilikuwa inafahamu jinsi itakavyosimamia uchaguzi kwa kufanya wizi, ulaghai na unyanyasaji wa wananchi wake kwa kuwapiga mabomu, risasi na marungu ikaona itumie fedha zake za ndani kupunguza hasira na lawama za kitaifa na kimataifa.
Jambo hili halikubaliki na ni dhuluma kwa Watanzania.