N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,308
- 12,812
MAPENDEKEZO YANGU: TUKITAKA KUJENGA UCHUMI WA UZALISHAJI, KUNA MAAMUZI MAGUMU LAZIMA TUANZE KUYAFANYA
Kuna mambo ambayo naamini kabisa tukiamua kuyafanya kwa nia ya dhati yanaweza kubadilisha namna uchumi wetu unavyofanya kazi.
Kwanza, tupange upya biashara zetu mijini.
Hii tabia ya kila nyumba inayojengwa lazima mbele iwe na fremu nne, tano au kumi za biashara nafikiri tunahitaji kuifikiria upya.
Mwisho wake kila mtaa unakuwa commercial area isiyopangwa.
Kwa nini tusijenge na kuimarisha masoko rasmi yenye miundombinu mizuri, halafu biashara nyingi za consumer goods zikajikita huko?
Maeneo ya makazi yabaki zaidi kuwa residential, huku tukiruhusu huduma muhimu za karibu kama maduka ya dawa, maduka madogo ya mahitaji ya lazima na huduma nyingine ambazo mwananchi anahitaji ndani ya neighbourhood.
Masoko yakijengwa vizuri, yakawa safi, salama, yana parking, vyoo, maji na miundombinu inayostahili, biashara nazo zinakuwa concentrated na Serikali inakuwa na urahisi wa kupanga miji na kusimamia shughuli za biashara.
Pili, turudi kwa nguvu kwenye viwanda.
Tumekuwa tukizungumza kuhusu Tanzania ya viwanda kwa miaka mingi.
Nadhani sasa tunahitaji kwenda hatua nyingine: Which industries are strategic to Tanzania?
Tutengeneze orodha kabisa.
Viwanda muhimu vilivyokufa au kudhoofika tuangalie namna ya kuvifufua.
Tujenge uwezo kwenye textiles, leather, pharmaceuticals, fertilizers, food processing, packaging, construction materials, spare parts na maeneo mengine ambayo tuna comparative advantage.
Tatu, kuna bidhaa nyingine honestly hatuna sababu ya kuendelea kuagiza.
Chopsticks, toothpicks, baadhi ya furniture, packaging materials, simple plastic products, sukari na bidhaa nyingine ndogondogo ambazo teknolojia yake siyo rocket science.
Kwa nini container itoke China kuleta bidhaa ambayo tunaweza kuizalisha Kibaha, Morogoro, Tanga, Mwanza au Mbeya? Kama tunalazimika kuileta iwe ni kwa vipindi vya uadimu au kama uzalishaji hautoshelezi tu!!
Hapa ndipo tunapopoteza foreign currency na wakati huohuo tunakosa nafasi ya kutengeneza ajira.
Badala yake tujenge mazingira yatakayofanya bidhaa hizo Made in Tanzania ziwe competitive kwa quality na price na ziteke soko la SADC.
Nne, hata relationship yetu na China na partners wengine ibadilike kidogo.
China ni strategic economic partner wetu na hilo halina ubishi. Lakini tunahitaji kufika mahali tuseme:
"Hii bidhaa msituuzie tu kutoka China; njoo uitengeneze Tanzania na pesa yako sharti iwekwe kwenye mabenki ya kitanzania."
Tunataka factories hapa. Tunataka joint ventures. Tunataka technology transfer. Tunataka Watanzania waingie kwenye supply chains.
Kwa baadhi ya bidhaa ambazo tuna soko la kutosha na malighafi zake zinapatikana hapa, direction iwe local production first badala ya importation forever.
Lakini kubwa kuliko yote kwangu ni hili:
Mwekezaji anayekuja Tanzania leo anatakiwa awe na uwezo wa kufanya projection ya miaka 10 au 20 mbele.
Ajue mfumo wa kodi.
Ajue mfumo wa leseni.
Ajue tozo.
Ajue masharti ya kuingiza mitambo.
Ajue sera ya sekta anayowekeza.
Na Serikali ikitaka kufanya major policy change, kuwe na consultation na reasonable transition period.
Tusijenge mazingira ambayo mtu anaweka USD milioni 50 leo halafu baada ya miaka miwili anaamka asubuhi anakutana na policy mpya inayobadilisha kabisa business model yake au Enforcements za regulatory bodies zisizomithirika na zisizofuata utaratibu wala kujali kwamba huu ni uwekezaji mkubwa.
Capital loves certainty.
Hata kodi ikiwa ipo, mwekezaji anaweza kuiweka kwenye calculations zake. Tatizo kubwa ni pale ambapo hawezi kutabiri kesho itakuwaje.
Kwa hiyo kwangu industrialisation yetu isimame kwenye nguzo chache rahisi:
Panga biashara → Jenga masoko rasmi → Fufua viwanda → Zalisha tunachoweza kuzalisha → Punguza unnecessary imports → Vutia technology transfer → Linda ushindani → Halafu zaidi ya yote, jenga predictable investment environment.
Tukifanya hayo kwa consistency kwa miaka 10–20, naamini kabisa tunaweza kubadilisha structure ya uchumi wetu kutoka kuwa taifa linalouza malighafi na kununua bidhaa zilizokamilika, kwenda kuwa uchumi unaozalisha, unaongeza thamani na unaouza bidhaa zake ndani na nje ya nchi. Kwa kufanya hivi Dira 2050 tutaifikia kama tunasukuma mlevi!
Ni mawazo yangu tu.
Wenzetu waliofanikiwa kwenye industrialisation walifanya nini ambacho sisi bado hatujafanya?
MWISHO KABISA
Tujifunze kwa Indonesia.
Indonesia walibadili approach yao: badala ya kuendelea kuuza malighafi na kuagiza bidhaa zilizoongezwa thamani, wakasukuma sera ya downstreaming; kwamba, rasilimali zao zichakatwe na kuongezewa thamani nchini.
Mfano mkubwa ni nickel; wakasukuma wawekezaji kujenga smelters na viwanda ndani ya Indonesia, hatua iliyovutia uwekezaji mkubwa hadi kwenye battery na EV supply chain.
Tanzania nasi tunahitaji mindset hiyo: unaweza kutaka soko letu na malighafi zetu, lakini kwa bidhaa tunazoweza kuzalisha hapa, njoo uweke kiwanda hapa.
Tusiuze malighafi na kununua bidhaa milele (Iwe mwiko kabisa).
Rasilimali zetu ziwe sababu ya viwanda kujengwa Tanzania, na kila anaezitaka rasilimali zetu aelewe kwamba atachakatia hapahapa iwe Tanzanite, Cobalt, Magogo, Samaki, mazao ya kilimo, ngozi nk

PREDICTABILITY YA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI
Hili nadhani ndilo jambo muhimu kuliko yote.Mwekezaji anayekuja Tanzania leo anatakiwa awe na uwezo wa kufanya projection ya miaka 10 au 20 mbele.