Kwa kweli na ki-UKWELI hali haitakuwa nzuri tena kama tulivyo zoea. Mabadiliko ni lazima yatakuwepo. Yanaweza kuwa mabaya au mazuri kutegemea mtizamo wa mtu. e.g. Subjective.
1. Kwa waliokuwa wanajiendea kuingia na kutoka kiholela Kenya bila ya pass sasa itakuwa sivyo tena. Utaratibu utabadilika.
2. Jeshi kusimamia Utendaji i.e. Hali ya Hatari manake hakuna MASIHARA tena. Ukienda kinyume unaweza kubutuliwa na hakuna pa kwenda kulalamika. Muda wa kuzurura/kutembea kwa Starehe utadhibitiwa sana au hakuna kabisa.
Huko kwa jirani(Kenya) sisi waTz tunayo maslahi binafsi mengi na muhimu e.g. Wapo Wanafunzi kutoka Tz wanaosoma Kenya, Wapo Wafanyabiashara wa kiTz hupeleka na hurudi na mizigo ya Bidhaa-(bidhaa, magari na madereva); huko Kenya waTz tuliweza kupata huduma za kiafya n.k, n.k
Kwa mantiki hiyo Watanzania (wabongo) waliokuwa wananufaika na kuwepo kwa jirani yetu; kwa vyovyote vile sasa wataathirika kutokana na Kutangazwa kwa HALI YA HATARI nchini Kenya.
Endapo hali itazidi kuwa mbaya tunategemea pia kupokea wakimbizi kutoka Kenya. Wakimbizi hao watahitaji huduma muhimu za kibinadamu - chakula, huduma za Afya na Malazi. Lakini pia wakimbizi watakuja na Tabia zao nzuri au mbaya yakiwemo na maradhi ya kuambukiza.
Kwa kuwa hali itakuwa ni Tete(Instability/unstable state), Maadui zetu wa ndani na nje ambao pia hatuwajui wanaweza kuitumia hali hiyo kufanya yao.
Wadau wataendeleza kwa kuchangia hoja.